Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh Mbowe leo ameandika barua rasmi ya kutia nia ya kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Chadema.

Hii inafanya jumla ya wanachama walio tia nia kugombea nafasi ya Urais Tanzania kupitia Chadema kufikia wanne baada ya Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu kutangaza nia siku chache zilizopita.

My take
Kama kweli mh Mbowe ana nia ya dhati basi ni rasmi sasa Chama kitampitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyilo cha Urais, sidhani kama Kuna mtu atakuwa na ubavu wa kupiga kura ya hapana kumkataa mwenyekiti asipewe nafasi hiyo.
Tundu Lissu ajiandae upya kwa awamu nyingine.

Swali ni je mh Mbowe anatosha kwa nafasi hiyo ya Urais?

Ushawishi wake kwa watanzania ukoje?

Ana sera zenye nguvu za kushindana na Magufuli.?

Mwisho nitoe pongezi kwa Chadema kwa kuwa na Democrasia imara.
 
Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh Mbowe leo ameandika barua rasmi ya kutia nia ya kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Chadema.

Hii inafanya jumla ya wanachama walio tia nia kugombea nafasi ya Urais Tanzania kupitia Chadema kufikia wanne baada ya Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu kutangaza nia siku chache zilizopita.
Ni jambo jema!
 
Africa tutakuwa watu wa ajabu sana,ni nchi moja tu barani Africa inayoongozwa na DJ, nayo ni Madagascar chini ya andry Rajoelina sasa naona DJ mbowe anataka atembelee nyota ya DJ mwenzake wa Madagascar.

Anajidanganya,Tanzania bado sana hatujafikia kiwango cha kuongozwa na DJ ,yeye akafufue tu club billcannaz yake,huko atapiga mpunga mrefu sana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Hoja ni nini hapo mkuu?
 
Back
Top Bottom