Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Safi
Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh Mbowe leo ameandika barua rasmi ya kutia nia ya kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Chadema.

Hii inafanya jumla ya wanachama walio tia nia kugombea nafasi ya Urais Tanzania kupitia Chadema kufikia wanne baada ya Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu kutangaza nia siku chache zilizopita.

My take
Kama kweli mh Mbowe ana nia ya dhati basi ni rasmi sasa Chama kitampitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyilo cha Urais, sidhani kama Kuna mtu atakuwa na ubavu wa kupiga kura ya hapana kumkataa mwenyekiti asipewe nafasi hiyo.
Tundu Lissu ajiandae upya kwa awamu nyingine.

Swali ni je mh Mbowe anatosha kwa nafasi hiyo ya Urais?

Ushawishi wake kwa watanzania ukoje?

Ana sera zenye nguvu za kushindana na Magufuli.?

Mwisho nitoe pongezi kwa Chadema kwa kuwa na Democrasia imara.
Safi sana! Ngoja sasa tusubiri MNYUKANO wa ndani ya CHADEMA kwa hao waliotia nia. Tundu Antipas Lissu angojee kuwa MGOMBEA MWENZA in absentia kwani sioni uwezekano wa yeye kurudi na kufanya kampeni in fresh come October 2020.
 
Back
Top Bottom