Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Mbowe awezagi kuficha tamaa yake. Busara na hekma anazo lakini kuficha tamaa yake huwa hawezi.
Bad move.
 
Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh Mbowe leo ameandika barua rasmi ya kutia nia ya kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Chadema.

Hii inafanya jumla ya wanachama walio tia nia kugombea nafasi ya Urais Tanzania kupitia Chadema kufikia wanne baada ya Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu kutangaza nia siku chache zilizopita.

My take
Kama kweli mh Mbowe ana nia ya dhati basi ni rasmi sasa Chama kitampitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyilo cha Urais, sidhani kama Kuna mtu atakuwa na ubavu wa kupiga kura ya hapana kumkataa mwenyekiti asipewe nafasi hiyo.
Tundu Lissu ajiandae upya kwa awamu nyingine.

Swali ni je mh Mbowe anatosha kwa nafasi hiyo ya Urais?

Ushawishi wake kwa watanzania ukoje?

Ana sera zenye nguvu za kushindana na Magufuli.?

Mwisho nitoe pongezi kwa Chadema kwa kuwa na Democrasia imara.
Nadhani tunahangaika mno na mambo yasiyotuhusu. Haya mambo tuwaachie wenyewe waamue wanavyoona inafaa kwao. After all, kwenye ushindani kila mmoja anajaribu bahati yake. Kuna wanaojaribu na wanapita na kuna wanaojaribu na wanashindwa. Lakini wasiojaribu wanashindwa 'absolutely'.
 
Nadhani swala la.Mbowe kuchukua form ya kugombea urais lipo kimkakati zaidi, nia yake sio kugombea ila kuna namna wanataka kuweka mambo sawa, nina uhakika hatapitishwa kwa kura za maoni na hii ni wamepanga ili kiondoa dhana ya kwamba mwenyekiti ni dikteta
Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh Mbowe leo ameandika barua rasmi ya kutia nia ya kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Chadema.

Hii inafanya jumla ya wanachama walio tia nia kugombea nafasi ya Urais Tanzania kupitia Chadema kufikia wanne baada ya Tundu Lissu, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu kutangaza nia siku chache zilizopita.

My take
Kama kweli mh Mbowe ana nia ya dhati basi ni rasmi sasa Chama kitampitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyilo cha Urais, sidhani kama Kuna mtu atakuwa na ubavu wa kupiga kura ya hapana kumkataa mwenyekiti asipewe nafasi hiyo.
Tundu Lissu ajiandae upya kwa awamu nyingine.

Swali ni je mh Mbowe anatosha kwa nafasi hiyo ya Urais?

Ushawishi wake kwa watanzania ukoje?

Ana sera zenye nguvu za kushindana na Magufuli.?

Mwisho nitoe pongezi kwa Chadema kwa kuwa na Democrasia imara.
 
Mbowe aliwahi kugombea miaka ya nyuma na hakufanya vyema sana. I thought msimu huu angewaachia wengine na kufacilitate process kama Chairman?

Well, ndio demokrasia hii japo ninadhani wapiga kura wanaweza kuona aibu kumsukumia nje mwenyekiti wao.
 
Kura za Kilimanjaro, Sijui kama hii ndiyo sababu au imetokea tuu Mbowe akaamua kugombea, lkn ukweli ni kwamba Kilimanjaro ndiyo ngome kuu ya chadema na bila ya Kilimanjaro hakuna chadema labda Kimara/Kibamba na Tegeta Kibaoni lkn bado haitoshi kuipa chadema kura za kutosha.

Hivyo Kilimanjaro ni kufa na kupona kwa chadema, na nahisi Mbowe & Co. wanalijua hilo kwamba wakimuweka mtu kama Tundu Lisu hawezi kupata kura za kutosha Kilimanajaro hivyo ili kuokoa chama basi ni lazima Mbowe ajitoe kafara kwa kuupoteza Ubunge ili kuokoa chadema angalau Kilimanjaro, Kimara/Kibamba, vinginevyo wakimuweka Tundu Lisu hawatapata hata theluthi ya kura walizopata Kilimanjaro Uchaguzi uliopita, ...
 
Mbowe hajawekwa kugombea urais bali ni mmoja kati ya watu 4 waliochukua form ya kuwania nafasi kugombea urais na ni mkakati wa kuwashuhulisha mataga ili mfungue thread kama hizi za kujifariji 🤣
 
Ni haki yake kikatiba, sisi tunamtakia kila la heri katika mpambano na Yohana.
 
Back
Top Bottom