Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Hivi kuna chama cha upinzani cha kuishinda CCM kwa sasa? Kwa mikakati ipi hasa? Mwaka 2015 walibadilishia gia angani, wakakaribisha mafisadi ndani ya umoja wao wa UKAWA. Wananchi waliwaunga mkono sana mwaka ule, ila wamewavunja moyo waliowaunga mkono kwa kufanya maamuzi ambayo hayakuwa na tija. Waache tamaa na ubinafsi
Wakae chini, waangalie walipojikwaa na kupanga mikakati thabiti ya muda mfupi na mrefu ya kushinda uchaguzi. Kukishinda chama kilicho na dola na ambacho kimekaa madarakani kwa miaka mingi si jambo rahisi.