Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Mbona nilisikia hajafika kule wanapo ita mlimani na sifa ya Raisi kikatiba ni Lazima awe na jiwe (Degree) angalau moja - iliyo patikana kwenye Chuo Kikuu cha hapa nchini ila kama ni Chuo cha nje ya nchi lazima kiwe kinatambuliwa na TCU
Acha mizengwe,
Sifa ni kujua kusoma na kuandika.
 
Ni haki yake, lakini kwa sasa Lissu ndio moto Wa kuotea mbali...
Lissu, kwa sababu nyingi tu...; pamoja na kwamba wote hawa tokea CHADEMA ni bora kuliko tulivyo sasa.

Uwezekano wa kuwa 'mkakati' maalum wa chama nayo inaweza kuwa sababu mhimu ya watia nia hawa tunaowashuhudia wakitangaza.
 
Una akili sana.Mbowe hana mpango wa uraisi bali lengo ni kuongeza hamasa na pia kuonyesha demokrasia ndani ya CHADEMA ilivyo na hasa pale atapokosa hiyo nafasi yeye kama mwenyekiti na huo utakuwa ni uthibitisha kuwa yeye si dikteta kama inavyosemwa na ma-CCM na ndio maana kakosa licha ya yeye kuwa mwenyekiti.

CHADEMA ina watu very strategic katika kufanya siasa.
Mkuu mbona unaandika kitu ambacho wewe mwenyewe hukiamini
 
CHADEMA chini ya mwamba Mbowe ni chama imara na chenye mikakati iliyokomaa. Hayo yanayotokea ya kutangaza NIA Ni kupima joto la hali ya hewa ya uchaguzi na kiwango cha kukubalika cha kila mmoja lakini ndani ya chama wanajua fika ni nani watamsimamisha. Hii ni tofauti sana na fisiemu ambapo mtoto na mkubwa wote ni kambale.

Mapambio ya kumsifu JPM ni uongo na uzandiki mtupu. Ni kumuahadaa msukuma wanayemchukulia kama ni mshamba wa kisiasa. Moyoni wanamtukana sana na kumlaani maana wafia chama hajawatendekea haki ya kulisha matumbo yao kama walivyotarajia. Badala yake JPM kawapa shavu walionunuliwa kutoka upinzani na wabunge wake aliowateua na kuwapa uwaziri. Ni yale majamaa yaliokotwa jalalani.
 
Africa tutakuwa watu wa ajabu sana,ni nchi moja tu barani Africa inayoongozwa na DJ, nayo ni Madagascar chini ya andry Rajoelina sasa naona DJ mbowe anataka atembelee nyota ya DJ mwenzake wa Madagascar.

Anajidanganya,Tanzania bado sana hatujafikia kiwango cha kuongozwa na DJ ,yeye akafufue tu club billcannaz yake,huko atapiga mpunga mrefu sana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Huyo DJ peke yake anasumbua ccm yote hadi wanataka kumuua.
 
Kama ni kweli basi ile mbinu yake ya kushambuliwa ilikuwa ni kumtoa Lisu kwenye mjadala.

Haiwezekani Lisu angee mchana then usiku mbowe avamiwe?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Itakuwa kapiga fungi tena, maana ni kichekesho cha karne kwa sasa
 
Acha mizengwe,
Sifa ni kujua kusoma na kuandika.
nafikiri unaongelea Udiwani
Rais wa Nchi awe na sifa ya kusoma na kuandika? you are not serious
Hiyo ilibadilishwa tangu enzi ya Mkapa; Lazima awe na Degree Moja na kuendelea...
 
moja ya sifa ya kuwa Rais ni angalau kuwa na degree hivi huyu jamaa si nilisikia ni form four au huwa ni story tu mkuu?
Huyo jamaa namjua toka enzi za ujanani alipokuwa anafanya kazi kwenye klabu ya baba yake maarufu kama "Mbowe" mwishoni mwa miaka ya sabini jijini Dar. Sijui kama ana degree yeyote ile.
 
kwa hiyo moja kwa moja hii hapa ni danga toto, mwisho wa siku anajifanya kujiengua wakati hana sifa hata za kuwa rais wa JMT.
Huyo jamaa namjua toka enzi za ujanani alipokuwa anafanya kazi kwenye klabu ya baba yake maarufu kama "Mbowe" mwishoni mwa miaka ya sabini jijini Dar. Sijui kama ana degree yeyote ile.
 
Kosa lingine hili chadema, ila ngoja tuone labda itatumika kama kiki kumbust Lissu, otherwise huu ni utopolo
 
Back
Top Bottom