MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Chadema siyo mali yake wala mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama.
Kutokana na hali hiyo, amesema kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na wenzao ndani ya chama hicho, watu hao wataachwa chama kiendelee kusonga mbele.
Mbowe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nduwa.
"Makamanda najua kuna watu wamekuwa wakiniuliza juu ya kauli iliyotolewa jana (juzi) na aliyekuwa Katibu Mkuu wetu, Dk. Wilbrod Slaa.
"Napenda niwaambie kuwa mwaka 1992 tulipoanzisha Chadema, ilikuwa ni kama safari ya treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma. Tulipoanza safari hiyo na kufika Pugu, abiria wengine walishuka na wengine wakapanda na tulipofika Morogoro, abiria wengine wakashuka na wengine wakapanda na mwaka huu Oktoba 25 safari yetu itafika Kigoma.
"Chadema siyo mali yangu, wala siyo mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama, anayedhani Chadema ni mali yake, ataondoka, chama atakiacha.
"Kamati Kuu, Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chadema viliamua Lowassa ndiye awe mgombea wa urais kupitia Chadema pamoja na Ukawa.
"Sasa, kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na sisi, hatuna muda wa kupoteza, tutawaacha, tutasonga mbele," alisema Mbowe na kushangiliwa.
Kwa mujibu wa Mbowe, Watanzania wanahitaji mabadiliko na ili mabadiliko hayo yafikiwe ni lazima kila mmoja ashiriki kadiri atakavyoweza.
Wakati huo huo, Mbowe alisema kutokana na muda mfupi wa kampeni uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mgombea wao wa urais na mgombea mwenza wake, Duni Haji, hawataweza kufika majimbo yote nchini.
Kutokana na hali hiyo, alisema wamelazimika kuunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuzunguka nchi nzima.
"Nchi yetu ina majimbo 215 Tanzania Bara na ina majimbo 50 Zanzibar. Katika hali ya kawaida, mgombea urais na mgombea mwenza wake hawataweza kuyafikia majimbo yote kabla ya tarehe ya uchaguzi.
"Kwa hiyo tumeunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuanzia wiki ijayo ili maeneo atakayoshindwa kufika mgombea urais na mgombea mwenza, vikosi hivyo vifike," alisema Mbowe.
Aliwataja baadhi ya watakaokuwa katika vikosi hivyo kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema, aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje, aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na yeye mwenyewe.
Chanzo: Mtanzania