Elections 2015 Freeman Mbowe atoa msimamo mzito kuhusu wanaoasi mageuzi

Una nchi wewe?loliondo ilishauzwa wewe bado upo usingizini.Hujitambui ndiyo tatizo.Shukuru shule za kata za lowasa

Kwenye mafanikio hapakos pingamiz, na msafala wa mamba kenge hawakosi, kama yesu alikuja kukimboa wanadamu lakini ndani ya hao wanadamu wakamsaliti yuda na pilato, ila alipo kufa wengne wakasema hakika huyu alikuwa mwana wa mng, he!!! Inashangaza sana goja wachukuwe nchi uone, ww hapo hata hutaongea utajuta yote haya unayoyatamka saiv, maana hujijuwi, tupo ambao hatubadiliki....
 
Jumanne, Dr. Slaa alitoa hoja nzito zilizohusiana na kukeukwa kwa taratibu la LOWASSA kukaribishwa Chdema na Ufisadi wa Lowassa. Jambo la kushangaza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe akiwa kwenye mkutano wa Kampeni huko Sumbawanga, kaibuka na MAJIBU MEPESI kwelikweli, kwamba CHADEMA ni kama treni ya kwenda Kigoma, abiria wanashuka na wengine kupanda vituoni. Kauli hii ya Mbowe inaamanisha, Dr. Slaa ameshuka na Lowassa amepanda. Hii kauli ya Mbowe ni sawa, lakini anasahau kuwa Kwenye treni siyo Abiria tu wanaopanda, bali hata VIBAKA.
Kwa Slaa kuondoka CHADEMA na Lowassa kuingia, ni sawa na Treni Kushusha abiria halali na kupandisha KIBAKA
 
Wakati chadema ikitapa tapa kujinasua kwenye mgogoro wa kisiasa wa chama hicho, taarifa za ndani zinasema Mbowe kasema Slaa ataendelea kupata haki zake zote mpaka atakapoandika barua ya kujiuzulu. Habari za ndani zinasema ndani ya chadema kuna mpasuko mkubwa haswa baada ya watu wengine kuanza kulalamikia maamuzi ya chama kufanyw kw kumshirikisha gwajima wakati wao hawakupata nafasi hiyo, maandamano yanatabiriwa kutokea kila kona ya nchi. Mbowe katoa waraka kuwa Slaa asijibiwe, kama ni majibu yaelekezwe ccm anaodai ni wadhamini wake

Wewe utakuwa unaandamana kutokea upande upi kuelekea upande upi?
 
mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), freeman mbowe, amesema chadema siyo mali yake wala mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama.

Kutokana na hali hiyo, amesema kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na wenzao ndani ya chama hicho, watu hao wataachwa chama kiendelee kusonga mbele.

Mbowe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wananchi wa mji wa sumbawanga, mkoa wa rukwa, waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa ukawa kupitia chadema, edward lowassa, uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi nduwa.

“makamanda najua kuna watu wamekuwa wakiniuliza juu ya kauli iliyotolewa jana (juzi) na aliyekuwa katibu mkuu wetu, dk. Wilbrod slaa.
“napenda niwaambie kuwa mwaka 1992 tulipoanzisha chadema, ilikuwa ni kama safari ya treni kutoka dar es salaam hadi kigoma. Tulipoanza safari hiyo na kufika pugu, abiria wengine walishuka na wengine wakapanda na tulipofika morogoro, abiria wengine wakashuka na wengine wakapanda na mwaka huu oktoba 25 safari yetu itafika kigoma.

“chadema siyo mali yangu, wala siyo mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama, anayedhani chadema ni mali yake, ataondoka, chama atakiacha.
“kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu wa chadema viliamua lowassa ndiye awe mgombea wa urais kupitia chadema pamoja na ukawa.
“sasa, kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na sisi, hatuna muda wa kupoteza, tutawaacha, tutasonga mbele,” alisema mbowe na kushangiliwa.

Kwa mujibu wa mbowe, watanzania wanahitaji mabadiliko na ili mabadiliko hayo yafikiwe ni lazima kila mmoja ashiriki kadiri atakavyoweza.
Wakati huo huo, mbowe alisema kutokana na muda mfupi wa kampeni uliopangwa na tume ya taifa ya uchaguzi (nec), mgombea wao wa urais na mgombea mwenza wake, duni haji, hawataweza kufika majimbo yote nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema wamelazimika kuunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuzunguka nchi nzima.
“nchi yetu ina majimbo 215 tanzania bara na ina majimbo 50 zanzibar. Katika hali ya kawaida, mgombea urais na mgombea mwenza wake hawataweza kuyafikia majimbo yote kabla ya tarehe ya uchaguzi.

“kwa hiyo tumeunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuanzia wiki ijayo ili maeneo atakayoshindwa kufika mgombea urais na mgombea mwenza, vikosi hivyo vifike,” alisema mbowe.

aliwataja baadhi ya watakaokuwa katika vikosi hivyo kuwa ni aliyekuwa mbunge wa arusha mjini, godbles lema, aliyekuwa mbunge wa ubungo, john mnyika, aliyekuwa mbunge wa nyamagana, ezekiah wenje, aliyekuwa mbunge wa mbeya mjini, joseph mbilinyi na aliyekuwa mbunge wa kawe, halima mdee na yeye mwenyewe.

chanzo: mtanzania

mwandishi

balile na kupenei at work.
 
Sumu ya mende aliyopulizia dr slaa; lazima kila mende atatoka. Kaanza mbatia, rostam, sasa mbowe.

Oct lini , tufunge gufuri au tufungue kufuri
 
Tutasikia na kuona mengi hivi sasa na zaidi baada ya uchaguzi. Tuvute subira.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Chadema siyo mali yake wala mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama.

Kutokana na hali hiyo, amesema kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na wenzao ndani ya chama hicho, watu hao wataachwa chama kiendelee kusonga mbele.

Mbowe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nduwa.

“Makamanda najua kuna watu wamekuwa wakiniuliza juu ya kauli iliyotolewa jana (juzi) na aliyekuwa Katibu Mkuu wetu, Dk. Wilbrod Slaa.
“Napenda niwaambie kuwa mwaka 1992 tulipoanzisha Chadema, ilikuwa ni kama safari ya treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma. Tulipoanza safari hiyo na kufika Pugu, abiria wengine walishuka na wengine wakapanda na tulipofika Morogoro, abiria wengine wakashuka na wengine wakapanda na mwaka huu Oktoba 25 safari yetu itafika Kigoma.

“Chadema siyo mali yangu, wala siyo mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama, anayedhani Chadema ni mali yake, ataondoka, chama atakiacha.
“Kamati Kuu, Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chadema viliamua Lowassa ndiye awe mgombea wa urais kupitia Chadema pamoja na Ukawa.
“Sasa, kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na sisi, hatuna muda wa kupoteza, tutawaacha, tutasonga mbele,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Kwa mujibu wa Mbowe, Watanzania wanahitaji mabadiliko na ili mabadiliko hayo yafikiwe ni lazima kila mmoja ashiriki kadiri atakavyoweza.
Wakati huo huo, Mbowe alisema kutokana na muda mfupi wa kampeni uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mgombea wao wa urais na mgombea mwenza wake, Duni Haji, hawataweza kufika majimbo yote nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema wamelazimika kuunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuzunguka nchi nzima.
“Nchi yetu ina majimbo 215 Tanzania Bara na ina majimbo 50 Zanzibar. Katika hali ya kawaida, mgombea urais na mgombea mwenza wake hawataweza kuyafikia majimbo yote kabla ya tarehe ya uchaguzi.

“Kwa hiyo tumeunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuanzia wiki ijayo ili maeneo atakayoshindwa kufika mgombea urais na mgombea mwenza, vikosi hivyo vifike,” alisema Mbowe.

Aliwataja baadhi ya watakaokuwa katika vikosi hivyo kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema, aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje, aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na yeye mwenyewe.

Chanzo: Mtanzania

Mbona hakuna UKAWA hapa. Wote hao ni Chadema hili changa la macho.
 
8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.

9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.

11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.
 
Mbele kwa mbele.

Slaa aendelee kula Mihogo. Siku akizinduka atakuta tayari Lowassa ndiye Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote Tanzania.
 
slaa anakipaji cha aina yake, kukubali kuacha ukatibu mkuu wa chama chake na kuwa kondomu ya magamba hicho ni kipaji.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Chadema siyo mali yake wala mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama.

Kutokana na hali hiyo, amesema kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na wenzao ndani ya chama hicho, watu hao wataachwa chama kiendelee kusonga mbele.

Mbowe alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipohutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nduwa.

“Makamanda najua kuna watu wamekuwa wakiniuliza juu ya kauli iliyotolewa jana (juzi) na aliyekuwa Katibu Mkuu wetu, Dk. Wilbrod Slaa.
“Napenda niwaambie kuwa mwaka 1992 tulipoanzisha Chadema, ilikuwa ni kama safari ya treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma. Tulipoanza safari hiyo na kufika Pugu, abiria wengine walishuka na wengine wakapanda na tulipofika Morogoro, abiria wengine wakashuka na wengine wakapanda na mwaka huu Oktoba 25 safari yetu itafika Kigoma.

“Chadema siyo mali yangu, wala siyo mali ya mtu yeyote bali ni mali ya wanachama, anayedhani Chadema ni mali yake, ataondoka, chama atakiacha.
“Kamati Kuu, Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chadema viliamua Lowassa ndiye awe mgombea wa urais kupitia Chadema pamoja na Ukawa.
“Sasa, kama kuna mtu na mkewe wana mawazo tofauti na sisi, hatuna muda wa kupoteza, tutawaacha, tutasonga mbele,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Kwa mujibu wa Mbowe, Watanzania wanahitaji mabadiliko na ili mabadiliko hayo yafikiwe ni lazima kila mmoja ashiriki kadiri atakavyoweza.
Wakati huo huo, Mbowe alisema kutokana na muda mfupi wa kampeni uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mgombea wao wa urais na mgombea mwenza wake, Duni Haji, hawataweza kufika majimbo yote nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema wamelazimika kuunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuzunguka nchi nzima.
“Nchi yetu ina majimbo 215 Tanzania Bara na ina majimbo 50 Zanzibar. Katika hali ya kawaida, mgombea urais na mgombea mwenza wake hawataweza kuyafikia majimbo yote kabla ya tarehe ya uchaguzi.

“Kwa hiyo tumeunda vikosi vinne vya kampeni vitakavyotumia helkopta nne kuanzia wiki ijayo ili maeneo atakayoshindwa kufika mgombea urais na mgombea mwenza, vikosi hivyo vifike,” alisema Mbowe.

Aliwataja baadhi ya watakaokuwa katika vikosi hivyo kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema, aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje, aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na yeye mwenyewe.

Chanzo: Mtanzania

Mapovu yana mtoka
 
Jumanne, Dr. Slaa alitoa hoja nzito zilizohusiana na kukeukwa kwa taratibu la LOWASSA kukaribishwa Chdema na Ufisadi wa Lowassa. Jambo la kushangaza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe akiwa kwenye mkutano wa Kampeni huko Sumbawanga, kaibuka na MAJIBU MEPESI kwelikweli, kwamba CHADEMA ni kama treni ya kwenda Kigoma, abiria wanashuka na wengine kupanda vituoni. Kauli hii ya Mbowe inaamanisha, Dr. Slaa ameshuka na Lowassa amepanda. Hii kauli ya Mbowe ni sawa, lakini anasahau kuwa Kwenye treni siyo Abiria tu wanaopanda, bali hata VIBAKA.
Kwa Slaa kuondoka CHADEMA na Lowassa kuingia, ni sawa na Treni Kushusha abiria halali na kupandisha KIBAKA

Dr Slaa ameibuka kuvuruga ili watu waache kufanya kampeni wahangaike naye. Mbowe ameligundua hilo, wacheni tusonge mbele.
 
Well said mheshimiwa Chairman, lakini naomba unithibitishie kweli Chadema ni chama cha wananchi, nashtuka kusikia hii

statement, manake kama kweli Chadema ni chama chetu sote kwanini wakati mnafanya maamuzi yenu ya kimafia

hamkutaka hata japo kutujuza. Mkaamua kuua UKAWA halisi ambayo ilikuwa na maono na malengo halisi ya kuliokoa taifa

hili.

Mr. Chairman kwanini hiki chama mmewapa watu wengine ambao hata misingi na malengo ya chama hawayajui.

Mr. Chairman kwa jinsi nijuavyo Chadema kilikuwa mtari wa mbele kupinga ufisadi na kulikuwa na makamanda wakina Dr.

Slaa, ZZK, John Mnyika na wengine, lakini kwa nini sasa hivi hatusikii hata japo mkigusia tu ufisadi? na hata kuukemea.

Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa ni wazi kabisa Chadema kimekuwa ni chama cha watu wachache, waliopumbaza

watanzania wengi kwa kauli mbiu ya mabadiliko. Watanzania wengi hasa vijana wanaonekana wazi kabisa kushindwa

kujitambua na kufuata tu makundi bila hata ya kupambanua mambo. Ni wazi ualisia wa Chadema umezidi kupotea.

#BRINGBACKOURCHADEMA

Chadema ni ya wanachama wote hata anayeingia leo ana haki sawa kwa ushahidi huu;

Slaa mwenyewe sio mwanzilishi, alihama kutoka CCM na alikaribishwa bila masharti na akafikia kuwa Katibu

Tutumie akili, mtu mmoja au wawili wakijitoa kwa kutokubaliana na wengi kwenye vyombo halali vya chama au muungano,kipi bora wawaache waende na wao waendelee au wafanye nini??

Kwa wanademokrasia hamuogopi mtu anayetoa masharti magumu kwa wenzake wanaotaka kujiunga na chama, unaposema mtu aje na wabunge,wenyeviti na makatibu hiyo ni kwa katiba ipi??

Kila mtu anahaki ya kikatiba kujiunga na chama chochote bila mashrti na ana haki ya kugombea na kuchaguliwa uongozi.
 
Mi namkubali sana Mh Mbowe kwa sababu yeye huwa anaangalia maslahi ya chama kwanza. Alipoona kwamba kwa wakati huo Slaa alikuwa na influence, alimwachia agombee na chama kikapiga hatua kubwa. Kwa sasa amesimama na Lowassa, naamini mtashuhudia maajabu yake OCtober 25. Kuna watu ni educated but not intelligent!
 
Chadema ni ya wanachama wote hata anayeingia leo ana haki sawa kwa ushahidi huu;

Slaa mwenyewe sio mwanzilishi, alihama kutoka CCM na alikaribishwa bila masharti na akafikia kuwa Katibu

Tutumie akili, mtu mmoja au wawili wakijitoa kwa kutokubaliana na wengi kwenye vyombo halali vya chama au muungano,kipi bora wawaache waende na wao waendelee au wafanye nini??

Kwa wanademokrasia hamuogopi mtu anayetoa masharti magumu kwa wenzake wanaotaka kujiunga na chama, unaposema mtu aje na wabunge,wenyeviti na makatibu hiyo ni kwa katiba ipi??

Kila mtu anahaki ya kikatiba kujiunga na chama chochote bila mashrti na ana haki ya kugombea na kuchaguliwa uongozi.

Imeaminishwa hivyo kuwa Chadema ni ya wanachama, ila hao wanachama au mashabiki wamewekwa kwa mtaji tu wa

watu flan flan. Ndio maana hata ukirudi nyuma kwa wale waliojitoa Chadema mwanzoni wakina ZZK na wenzie hili ndio

lilikuwa tatizo kubwa la Chadema, yaani hamna free of speech, mwenyekiti anaangalia maslahi yake na ya watu wake basi

wanafanya maamuzi.

ZZK alijaribu kuhoji baadhi ya vitu vya msingi akaonekana ni msaliti. Kwa vile wengi tumeichoka CCM ndio maana vitu vya

msingi kama hivi tunajifanya hatuvioni, lakini hatujui madhala gani makubwa yatakuja kutokea mbeleni tukiikabidhi nchi

kwa kikundi flan cha watu.
 
kwa kweli waacheni. wamezidi sasa, silaaaaaaaaaaaaaa, zitooooooooo, kitilaaaaaaaa,
ila kwa slaa du! aliposhushwa zitto alicheka mbaya, sasa naye kashukia pale nguruka kwenye samaki ale samaki ili akipata gari lingine arudi dar, hahaahah
 
Wakati chadema ikitapa tapa kujinasua kwenye mgogoro wa kisiasa wa chama hicho, taarifa za ndani zinasema Mbowe kasema Slaa ataendelea kupata haki zake zote mpaka atakapoandika barua ya kujiuzulu. Habari za ndani zinasema ndani ya chadema kuna mpasuko mkubwa haswa baada ya watu wengine kuanza kulalamikia maamuzi ya chama kufanyw kw kumshirikisha gwajima wakati wao hawakupata nafasi hiyo, maandamano yanatabiriwa kutokea kila kona ya nchi. Mbowe katoa waraka kuwa Slaa asijibiwe, kama ni majibu yaelekezwe ccm anaodai ni wadhamini wake

Ndugu yangu - maneno yako yanakidhi sheria ya mitandao???
 
Back
Top Bottom