Napata shaka na ufahamu wako yaani bado mh raisi unamfananisha na mbowe? Raisi amekuwa waziri kwa miaka zaidi ya kumi na kazi aliyoifanya mpaka vipofu wanaijua mbowe haya uyo mbowe amefanya Nini tusiende mbali niambie Jimbo kwake amefanya nini? Kumfananisha magufuli na mbowe kiutendaji/ uzoefu / utawala hawalingani sembuse kufananisha cheo Cha uraisi na mbowe? Ni sawa na mbingu na ardhi
Yaani nakushukuru kwa kunikumbusha! Magufuli amekuwa waziri miaka 20 halafu bado anaongea kisukuma ili wengine watafasiri? Kweli kabisa kafanya mengi mno. Ufisadi mkubwa kwenye wizara ya ujenzi. Amesimamia UPORAJI MKUBWA WA NYUMBA NA VIWANJA VYA SERIKALI. CCM wamefanya uharamia mkubwa nchi hii, lakini nadhani hili la kupora viwanja prime vya serikali, likisimamiwa na nani kama siyo mporaji nambari wani? John Joseph Pombe Magufuli? Hilo limetia fora. Wezi wakubwa nyie msio na aibu! Ndio maana watanzania ni mafukara wa kutupa chini ya CCM.
Kwenye wizara ya UVUVI, Magufuli aliwatia umaskini wavuvi kwa kuchoma nyavu zao. Serikali ingeweza kabisa kutoa elimu ya nyavu, kisha ikatoa nyavu zinazotakiwa bure au kwa kuwakopesha, halafu ikazuia uingizwaji wa nyavu mbaya, baada ya hapo ndio ingekuja operesheni kwa wakorofi wachache. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwakomoa na kuwafukarisha watanzania, uharamia na ubabe ndio ulitumika. Akiwa Rais, Magufuli amerudia tena zoezi hilo, ambalo waziri Luhaga Mpina amelisimamia kwa Ukatilivwa viwango vya Adolf Hitler , ikabidi Magufuli ampe sifa za pekee kwa kumwita KICHAA MWENZANGU! Mashetani hayo yanapongezana, huku katika vijiji vya wavuvi wameacha vilio.
Magufuli amesimamia bomoabomoa ya kikatili na kusababisha vifo vingi maeneo ya Kimara, huku akizuia ubomoaji usukumani Mwanza. Akiamini kwamba wakazi wengi kimara - Mbezi ni wa kaskazini, ambao kosa lao ni kupambania maendeleo. Basi.
Magufuli anapora fedha za masikini watanzania na kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato, ambao akitoka madarakani utakuwa pori la popo na fisi.
Siasa za Magufuli za miundombinu kwanza badala ya kilimo kwanza (kilimo cha kweli, sio kejeli ya Kikwete), zimesababisha ufukara mkubwa kwa watanzania, kuwafanya waathirike zaidi sana na madhara ya korona katika uchumi, na mafuriko.
Mbowe hana serikali, lakini amewajibika vema katika kuimarisha upinzani bora. Wajibu wa kuleta maendeleo ni wa serikali inayokusanya kodi. Mbunge anawasilisha maoni ya wananchi bungeni, anaisimamia na kuikosoa serikali, anashiriki kupanga bajeti na usimamizi kupitia kamatiza Bunge. Pia mbunge anashiriki kutunga sheria, na kusimamia na kushauri katika mambo ya kitaifa na kimataifa. Rais Magufuli anafanya jitihada kubwa kukwamisha maendeleo kwenye majimbo yanayoongozwa na wapinzani, huku anadai maendeleo hayana vyama!