Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Karibu bwana Mbowe
Unafikiri wewe ndiyo mwanasiasa wakwanza Tanzania?
Hata nusu ya Mtikila au Mrema bado hujafikia!
Utakamatwa na utafungwa, kama Segerea umeona bustani ukafiri ni shamba, sasa utaenda Kitqengule uone shamba lenyewe
Na nakuhakikdishia baada ya hapo utajifunza kuheshimu mamlaka

1. Waliowafunga akina mtikila na akina mtikila wapo wapi?

2. Ukifaham kanuni ya haki ya kufa na kuishi haibaguwi basi Muogope Mungu.

No one will survive forever na hapo wenye hekima huitafuta haki sio tu watendewe wao bali kulihuwisha Taifa kuwa la AMANI, HAKI NA UTENGAMANO.
 
Mbowe amedai wakati alipokuwa shambani hapo gerezani Segerea ndipo aliposikia milio ya risasi za bunduki.

Nimejiuliza tu Segerea gerezani kuna shamba pale?

Anayejua Tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Tume huru ina vigezo gani?

Haifuati matakwa ya rais, hilo ni moja na kubwa. Kitendo chochote cha tume kuona kuna figisu isimtangaze mshindi, na iwe na nguvu ya kukiondoa chama chenye mizengwe kwenye uchaguzi. Wajumbe wa tume wasiondolewe kwa utashi wa rais bali kwa tume maalumu inayoaminika na itakayoundwa na vyama vyote, viongozi wa dini na majaji wenye kukubalika na wasio na utata wowote.
 
Kwani shamba nini ?
Jinsi ujuavyo bwashee tofaut zake min?
Ila bwashee tuache tujadili corona nasio hotuba ya mtu
Kuijadili ni kuongeza hofu kwa baadhi ya watu.

Cha muhimu ni kufuata maelekezo yaliyotolewa na wizara ya afya bwashee.

Sisi wa Dsm tumeshapewa mwongozo na mkuu wa mkoa wetu!
 
Mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA NA WAANDISHI, Machi 16,2020.


====
Updates
View attachment 1389820

“Watanzania walifikiri mashtaka yetu yanahusika na kumuua Akwilina, hatuwezi kufunga faili la kesi ile bila kujua hatma ya Akwilina”.Mhe.Mbowe.

“Waliohusika wasiachwe wakacheza na maisha ya watanzania, hawa watu wachukue hatua mkononi kuwajua askari wote waliomuua Akwilina" Mhe.Mbowe.

“Mimi nikiwa jela kule nikiwa shambani zimepigwa risasi zaidi ya 13, za moto,wanapambana na Halima Mdee, Ester Bulaya, na Jesca Kishowa, hawa ni wamama, hata katika sheria za magereza wanaoruhusiwa kushughulika na wanawake ni wanawake tu, lakini hapa ni wanaume wenye vifua, wenye silaha, wanamshughulikia Halima wamemuweka mtu kati”. Mhe. Mbowe.

Mimi na viongozi wenzangu waandamizi tulipohudhuria sherehe za Uhuru uwanja wa Kirumba Mwanza nilipopewa nafasi ya kusalimia na nikamtaka rais aone ulazima wa kutengeneza maridhaino kuleta maridhiano… alisema nimesikia”.Mhe.Mbowe.

Sisi tulipoyataka maridhiano ya Kitaifa hayakuwa kielelezo cha uoga, ilikuwa kielelezo cha kuitaka amani katika nchi yetu kwa sababu tunaona tunakokwenda siko…”.Mhe.Mbowe.
''Natangaza rasmi kuwa kuanzia mwezi ujao wa nne tutaanza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima bila kujali kuna katazo la Rais Magufuli na tuko tayari kwa lolote, tumekuwa waungwana vya kutosha na sasa hatutarudi nyuma kwenye hili'' - Freeman Mbowe

"Nawatangazia viongozi wote wa Chadema nchi nzima kuanzia Majimbo, Kanda, Kata, Vijiji na Mitaa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima, kwanza ni kudai tume huru na pili ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu"
"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema
tumekuelewa baba...tupo tayari kufa kwa ajili ya haki...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu bwana Mbowe
Unafikiri wewe ndiyo mwanasiasa wakwanza Tanzania?
Hata nusu ya Mtikila au Mrema bado hujafikia!
Utakamatwa na utafungwa, kama Segerea umeona bustani ukafiri ni shamba, sasa utaenda Kitqengule uone shamba lenyewe
Na nakuhakikdishia baada ya hapo utajifunza kuheshimu mamlaka
Mamlaka pekee ni ya wananchi.

Usitishe watu hapa bwege wewe!
 
Haifuati matakwa ya rais, hilo ni moja na kubwa. Kitendo chochote cha tume kuona kuna figisu isimtangaze mshindi, na iwe na nguvu ya kukiondoa chama chenye mizengwe kwenye uchaguzi. Wajumbe wa tume wasiondolewe kwa utashi wa rais bali kwa tume maalumu inayoaminika na itakayoundwa na vyama vyote, viongozi wa dini na majaji wenye kukubalika na wasio na utata wowote.
Watachaguliwa na nani na nani atawalipa mishahara yao na gharama zingine bila kuathiri dhamira na wajibu wao?
 
Kama serikali itatangaza hatua za dharura dhidi ya ugonjwa wa Corona ikiwemo kuzuia mikusanyiko ya umati wa watu..nawasihi viongozi wa kisiasa kuacha mara moja mikutano hiyo.

Kimsingi cdm hawataki kufanya mikutano kama tendo la jazba, bali haki yao kikatiba. Iwapo kutakuwa na huo ugonjwa bado hata mimi siwashauri cdm kufanya mikutano yao kwani ni kwa ajili ya usalama wa watu wao pia. Ila sio ccm wafanye kisha cdm wazuiwe, hilo halitakubalika. Kama ni kutii cdm wametii sana, na sasa ni muda wa kila mmoja kuingia shambani kuandaa shamba.
 
Watachaguliwa na nani na nani atawalipa mishahara yao na gharama zingine bila kuathiri dhamira na wajibu wao?

Swali zuri sana, kuanzia sasa vyama vya siasa vitapendekeza majina mawili mawili. Kisha hao wataingia kuwachagua majaji watano, viongozi wa dini watano, na watu watano mbalimbali toka haki za binadamu na asasi nyingine huru. Kundi hili ndio litamchagua mwenyekiti wa tume na wasaidizi wake, na ndio litalotoa muundo wa tume. Kulipwa watalipwa na pesa za umma na sio kwa mapenzi ya rais. Fungu la kuwalipa litakuwa kisheria na sio hisani ya mtu yoyote.
 
Kifo cha akwilini kimeiingizia serikali m 350 pasipo kuhusisha wahusika wakuu wa vurugu zile waliokingiwa kifua yaani mkuregenzi, polisi waliokuwa zamu na mbunge aliyeuza utu wake.
 
Back
Top Bottom