Tetesi: Freeman Mbowe kugombea Urais kupitia CHADEMA 2025

Kuelekea uchaguzi mkuu kumpata mgombea mpya ndani ya ccm huwa kuna makundi makundi ya wagombea ndani ya chama chao. Vipi kwa chadema hakuna makundi makundi ya wagombea wanaowania kupitishwa na chama hicho kugombea urais?
Ongeazea neno "ili wapate ruzuku ya kupiga kampeni maana wanajua kabisa hawashindi kwa namna yoyote"
 
Kama ni kweli basi upinzani unauzwa tena kwa mara nyingine. Nimechoka kabisa
 
Vipi kisomo cha Mbowe kikoje? Je anayo degree? Amesoma wapi? Nafikiri hiki kigezo ni kigumu kwake
 
Vipi kisomo cha Mbowe kikoje? Je anayo degree? Amesoma wapi? Nafikiri hiki kigezo ni kigumu kwake
Kwani mwanzo alivyogombea alikuwa amesoma wapi? Au ulikuwa darasa la pili hukumbuki.
Anyway hayo ni maoni ya mleta mada tu, mimi naona agombee yule yule wa 2020(TL), tatizo hata akigombea nani kutoka upinzani, ccm wanaiba kura.
 
Kuelekea uchaguzi mkuu kumpata mgombea mpya ndani ya ccm huwa kuna makundi makundi ya wagombea ndani ya chama chao. Vipi kwa chadema hakuna makundi makundi ya wagombea wanaowania kupitishwa na chama hicho kugombea urais?
Yapo makundi zaidi ya mawili chamani humo yanayojipambanua na yanayobainishwa na wajumbe na wanachama wenyewe mathalani,

kundi moja likiaamini katika uzalendo likijiita patriotic na hawa wanajipa umuhimu zaidi eti ndio wenye chama,

na kundi jengine ni lina sura ya kipuppet hawa wanaonekana ni intruders ambao wamestukiwa na kuonekana wanamaslahi binafsi wanatumwa na vibaraka kuvuruga chama na nchi kulingana na mienendo yao....

na kundi lingine ni wale wasio na uhakika miongoni mwa hayo makundi mawili. Hili limegubikwa na udiaspora ulopasuka. Kundi hili lina fedha na linataka kutumia pesa kuinfluence mgombea wao ambae ni Dr Slaa apewe nafasi iyo ingawa hayupo chamani hivi sasa
 
Vipi kisomo cha Mbowe kikoje? Je anayo degree? Amesoma wapi? Nafikiri hiki kigezo ni kigumu kwake
ndio anayo Shahaada ya kwanza ya Utawala, bachelor of Public Administration alioipata chuo kikuu huko uingereza.
Anavyovigezo vyote vya kitaaluma, uzoefu kijamii na kisiasa...
 
Ndie pekee mwenye uungwaji mkono mkubwa wa wajumbe wa ndani na nje ya nchi miongoni mwa wanachama wake.
Huyu aliahidi uenyekiti mwisho mwaka huu, na mwaka karibu unakatika bila kutoa tamko rasmi la kuachia ngazi, wala kubadilisha mawazo. Hivi humo chamani kumbe kuna watu bado wanamwamini na kumuunga mkono? How can we trust a dude who doesn't stand on his word?
 
Kwani mwanzo alivyogombea alikuwa amesoma wapi? Au ulikuwa darasa la pili hukumbuki.
Anyway hayo ni maoni ya mleta mada tu, mimi naona agombee yule yule wa 2020(TL), tatizo hata akigombea nani kutoka upinzani, ccm wanaiba kura.
ni kweli anafaa ila kwasasa unaweza mfananisha au kumlinganisha na Martin Fayulu wa DRC....
Haaminiki.

Leo hii yupo salama na hatishiwi maisha, ila sasa akishindwa uchaguzi tu, utaskia eti anatishiwa maisha, hayapo salama, wanataka kumkamata na kwahivyo anakwea pipa na kutokomea ughaibuni na kuungana na familia alozawadiwa huko
 
Ongeazea neno "ili wapate ruzuku ya kupiga kampeni maana wanajua kabisa hawashindi kwa namna yoyote"
suala la kushinda uchaguzi wa jumla ni jambo jengine kwanza ushinde chamani
 
Haijalishi nani atagombea. CCM inashinda kiti cha urais hata iweje, wengine wagombee tu ili wapate nafasi za viti maalum.
ushindi wa Rais uchaguzi wa jumla ni suala jengine, hapa anazungumzwa huyu muungwana chamani mwake kwamba ndie atakae kua kinara kupambana na wengine kuingia ikulu ya chamwino...
 
Mkuu hebu acha masihara basi, unaachaje kumunga mkono boss wako kuwa mgombea urais. Maajabu haya!
kuna ngoma moja hivi inaitwa utaipenda ya Hussein Machozi, video yake ukiiangalia inachekesha sana Ndio inamuhusu sana huyo muungwana πŸ’
 
Afrika tungeachana na mambo ya chaguzi tu, kwa sababu we know what is going to happen...

Mfano hapo DRC Congo, Tsishekedi wa enzi zile siye huyu wa sasa..
mambo si yanabadilika mkuu hata mbowe wa sasa sio wa wakati ule the man is prepared, organized, bold and committed ukilinganisha na awali
 
The guy is talented tuache masiala
he is still relevant and significant in political scene mbaya sana yaani ukilinganisha na wengine....

The gentleman is more πŸ”₯ and very smart
 
Alishamtaja hapo chini, japo alichoandika ni kama kinalenga kuwasikia wale wanaopanga kwenda na makamu wake katika uchaguzi mkuu watasemaje.
huna hakika muungwana,? ni kama ndio nini
 
Pamoja na kwamba siungi mkono mleta hoja , lakini ni dhahiri Una mawazo duni mno !
ndiyo mawazo yake hayo mkuu,
na wewe vilevile huo ndio mtazamo wako dhidi ya wazo lake,
and you are all very right to enjoy freedom of speech, and freedom of expressions
 
Sisi Tupo na Peter Msigwa na Tundu Liau
wanafaa na ni haki yao but this time round kuna ugumu mkubwa sana kwenye kura za wajumbe hasa kutoka Zanzibar kuna mtu mkubwa na maarufu sana atakosa kabisa kura kutoka Zanzibar kisha atakwama kusonga mbele.......

kwa jinsi alivyo atajiengua chamani akiamini ni faulo πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…