Tetesi: Freeman Mbowe kugombea Urais kupitia CHADEMA 2025

Tetesi: Freeman Mbowe kugombea Urais kupitia CHADEMA 2025

Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Mtu mjinga tu ndio anaweza kushiriki hizi chaguzi za kishenzi.
ni sawa furahia uhuru wa kutoa maoni ila zingatia unawajibika kutokuvuka mipaka....

wajinga tutashiriki uchaguzi kikamilifu chaguzi hizi unazodai za kishenzi, ila ile jambo muhimu ni usituletee fujo, mihemko na ghadhabu zako kwenye ujinga wetu....

Hilo la kwanza,
hiyo kulia lia na kubwekabweka ukae nayo nyumbani hatuna muda nayo na wala hatuwezi hangaika nayo
 
Anauzika na kunadika kirahisi sana kwa wananchi na anazungumzwa vizuri sana ndani na nje ya nchi..

Hayupo wa kumshinda kwa mvuto wa kisiasa, uwezo wa kiuchumu na ushawishi katika ujengaji hoja na kujieleza.
Ana mtaji wa uhakika wa kura za wajumbe ndani ya chama chake na wananchi nje ya chama chake.

Ni mzalendo wa kweli na makini. Mstahimilivu mwenye staha, weledi na subra.

Anaaminika pakubwa ndani na nje ya Chama chake zaidi ya mwanachama mwingine yeyote humo chamani.

Ndie pekee mwenye uungwaji mkono mkubwa wa wajumbe wa ndani na nje ya nchi miongoni mwa wanachama wake.

Wapo wengine wenye nia ya kuomba kuteuliwa na chama kugombea urais katika chama hicho. Yes well and good, ni haki yao, wana uwezo wao na ni viongozi wazuri tu, kasoro yao ni moja tu miongoni mwao wanaungwa mkono na baadhi ya wajumbe diaspora tu na sio mahali pengine popote. Na wengine hawana ushawishi miongoni mwa wajumbe ndani ya chama kabisa.

Kwa ushauri wangu inafaa wasubiri na kujijenga zaidi hasa kwenye kujieleza kwa staha humu nchini.

He can seat and negotiate with others. He can manage and mobilize opposition into one team, voice, mission, vision and win elections easily than anyone in opposition.

Hakuna mwenye uwezo huo zaidi ya muugwana huyu na statesman Freeman A. Mbowe


Mungu Ibariki Tanzania.
Katiba mpya bora kwanza !
Mengine porojo tu. !
 
Hii safi sana, aligaragazwa na Kikwete, sasa agaragazwe na Mama Samia.
kanuni moja muhimu sana katika siasa ni kamwe usimuanderate wala kumdharau mpinzani wako kwa namna yeyoyote ile,

you never know what will happen to voters mindsets and decion on election day 🐒
 
Huyo ni waziri mkuu huko mbeleni ni swala la muda TU!

Kwa kawaida waziri mkuu ni Rais Wa Tanganyika!
He deserves nakubali...

Na actually nafasi ya Naibu Waziri Mkuu imeundwa kwa madhumuni hayo ya serikali ya umoja wa kitaifa kama maandalizi, meaning kwamba Waziri Mkuu atatoka Upinzani then Naibu Waziri Mkuu kutoka tawalani
 
Ni mzalendo wa kweli na makini. Mstahimilivu mwenye staha, weledi na subra.
Mkuu Tlaatlaah , kwanza naunga mkono hoja, pili tatizo ni huyu...
Wapo wengine wenye nia ya kuomba kuteuliwa na chama kugombea urais katika chama hicho. Yes well and good, ni haki yao, wana uwezo wao na ni viongozi wazuri tu, kasoro yao ni moja tu miongoni mwao wanaungwa mkono na baadhi ya wajumbe diaspora tu na sio mahali pengine popote. Na wengine hawana ushawishi miongoni mwa wajumbe ndani ya chama kabisa.
Chadema ina tatizo la watu kujimilikisha kugombea urais!. Angalia hapa nilisema nini Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA nilisema
Lissu alipoulizwa kuhusu yeye kugombea urais 2025 alijibu kwanza katiba, alipobanwa sana akasema ndio atagombea!. That was a mistake!. Kwa vile Chadema bado hawajafanya kikao chochote cha kumteua mgombea wake wa urais wa 2025, hakuna ubaya wowote kwa mwana Chadema yeyote kuwa a wishful thinker kugombea urais 2025 lakini kutamka kwenye TV kuwa yes nitagombea wakati hakuna kikao chochote kilichomteua ni very dangerous!.

He who pays the piper, may call the tune!, whoever is paying the Chadema piper ndio may call the tune, nani agombee Chadema ili usimsumbue yule Malkia wetu, ikitokea sio Lissu, na huku Lissu ameisha tangaza kugombea, huko ndani kutakalika?.

Paskali
mtu keshajitangaza hadi kwenye TV kuwa ni yeye atagombea urais wa JMT kwa tiketi ya Chadema 2025, halafu leo chama kisimteue yeye humo ndani kutakalika?.
Niliwahi kuwauliza CHADEMA humu, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Jingine, huyu mgombea pendekezwa wako, anamheshimu sana Mama, iwapo CCM itamsimamisha mwanamke, Mama, huyu ataweza kweli kumchallenge Mama?. Kwenye hili mimi nimeshauri Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Last but not least, kuna hoja ya ukabila vipi?,
P
 
Back
Top Bottom