Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
- Thread starter
- #81
sawa,Mimi mtu akiniuliza mawazo yangu kuhusu usanii huu wa uchaguzi nitasema yafuatayo;
Ni heri yale aliyofanya Jerry Rawlings wa Ghana 1979 yatokee hata hapa.
Rawlings akiwa afisa wa jeshi la anga kijana 1979 aliongoza mapinduzi na akairudisha serikali ya kiraia mwaka uliofuata.
Alipoona ujinga wa serikali ya kiraia umerudi tena 1981 akapindua tena na kufuta vyama vyote vya siasa, ikaundwa katiba ya kidemokrasia mpya kabisa kisha baada ya muda uchaguzi ukaitishwa na akajiuzulu jeshini na kugombea kiraia na kushinda mihula miwili.
Bila kutokea wa kuivunjilia mbali CCM na vikaundwa vyama vingine upuuzi hauwezi kuisha nchi hii.
Na ni wajibu wa vijana kujua kuwa bila kukiondoa kizazi hiki cha ccm madarakani na katika mifumo yetu hatutoboi kama nchi.
TUWAONDOE na kuifuta siasa hii ya kushika hatamu milele
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
ngoja tumsubiri huyo tukiwa tunag'aa macho na kulalamika tu 🐒