Freeman Mbowe kuitwa Mandela wa Tanzania ni sawa?

Freeman Mbowe kuitwa Mandela wa Tanzania ni sawa?

Kwa upande wang naona sio sawa na vigezo nimeandika hapo juu.
Hiyo ni tafsiri yako, iwapo ulikuwa mmoja wa watoa wazo la ubambikiaji, ina maana ulikuwa na chuki kwa mhusika, hivyo lazima utengeneze uhalali wa ulichokifanya, hivyo sitakushangaa kwa mabaya yote utakayoyasema dhidi ya unayemchukia.
 
Kwa kauli ya Mbowe aliyosema kwamba eti kwa miaka mitano ya Magufuli hakutaka watu wa kabila lake waajiriwe Serikalini,, inaonesha wazi ni mtu anaepigania maslahi ya Jamii yake na si Watanzania, hvyo hafai hata kidogo kumfananisha na shujaa aliyepigania maslahi ya wazawa ktk taifa lake la South África

Kwa kauli ile inatosha kuonesha the motion behind ya kiongozi huyu na chama chake kwa ujumla

Mbaya zaidi alipofiwa na Kaka yake alisema hataki watu wakusanyike kwenye msiba kuepusha maambukizi ya Corona huko kwao, ila baada ya mazishi akaelekea Mwanza kuhamasisha mikusanyiko ya kongamano la katiba.

Kwamba hawa wa nyumbani niwaepushe na corona ila hawa wapuuzi wengne wacha wakajifie tu
 
Ufinyu wa jinsi ya kuyaona mambo, ukanda na ukabila ulitanda Tena Bila kificho, hats kauli za wazi zilijithihirisha, kuwa ni zamu ya ukanda fulani, wengine ilishatosha.
 
..Mandela aliitwa Gaidi na serikali ya SA.

..Mbowe anaitwa Gaidi na serikali ya TZ.

..Ni sahihi Mbowe kuitwa Mandela wa TZ.
 
Hiyo ni tafsiri yako, iwapo ulikuwa mmoja wa watoa wazo la ubambikiaji, ina maana ulikuwa na chuki kwa mhusika, hivyo lazima utengeneze uhalali wa ulichokifanya, hivyo sitakushangaa kwa mabaya yote utakayoyasema dhidi ya unayemchukia.
Swala la kubambikiana linatoka wapi mkuu. Hapa tunajadili sifa zao kama zinafanana.
 
Kwa kauli ya Mbowe aliyosema kwamba eti kwa miaka mitano ya Magufuli hakutaka watu wa kabila lake waajiriwe Serikalini,, inaonesha wazi ni mtu anaepigania maslahi ya Jamii yake na si Watanzania, hvyo hafai hata kidogo kumfananisha na shujaa aliyepigania maslahi ya wazawa ktk taifa lake la South África

Kwa kauli ile inatosha kuonesha the motion behind ya kiongozi huyu na chama chake kwa ujumla

Mbaya zaidi alipofiwa na Kaka yake alisema hataki watu wakusanyike kwenye msiba kuepusha maambukizi ya Corona huko kwao, ila baada ya mazishi akaelekea Mwanza kuhamasisha mikusanyiko ya kongamano la katiba.

Kwamba hawa wa nyumbani niwaepushe na corona ila hawa wapuuzi wengne wacha wakajifie tu

..kati ya kongamano la Chadema, na mechi ya ligi kuu uwanja wa Kirumba, kipi kinaweza kueneza covid kwa watu wengi?

..siku ambayo kongamano la Chadema ilikuwa lifanyike kulikuwa na mechi ya ligi kuu uwanja wa kirumba Mwanza.
 
Kwanz kabisa napenda kuwasalimu kwa jina la alietuumba, ambae ni muweza wa visivyowezwa. Ama baada ya salam napenda nijielekeze katika mada yangu ili kila mwenye uwezo thabiti wa kuchangia aweze kuchangia.

Mada hii ni nzito na inawafaa zaidi wale ambao akili zao zipo huru, hazijafungwa wala kuhifadhiwa ndani ya mfuko wa mwanasiasa yoyote. Maana kuna watu ambao tayari wameshawakabidhi wanasiasa akili zao, kiasi kwamba hawawezi kuwa na wazo lolote kinyume na wale wanaomiliki akili hizo.

Twende sasa... Ndugu zangu kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumfananisha mwenyekiti wa Chadema taifa mh Mbowe na aliekuwa mpambanaji wa kweli na mpigania uhuru wa Afrika kusini hayati Nelson.

Ingawa kila mtu anaweza kuwa na mawazo au mtizamo wake lkn kwangu mimi naona kuwa watu hao wanakosea sana. Naweza kutaja baadhi ya sababu zinazofanya nikatae kukubaliana na watu hao.

Sababu hizo ni :

[1] Hayati Nelson alikuwa tayar kuwapambania wa South Africa wote bila kujali rangi zao, makabila yao, dini zao, vyama vyao na itikadi zao. Wakati mh Mbowe anaonekana kupambania zaidi masilahi yake, masilahi ya baadhi ya ndugu zake, watoto wake na tumbo lake.

[2] Hayati Nelson alihamasisha mapambano akiwa mstari wa mbele na familia yake. Mh Mbowe alikuwa na tabia ya kuhamasisha mapambano au maandamano, huku yeye na familia yake wakitimkia Afrika kusini au Dubai kula bata nk.

[3] Hayati Nelson alijitolea kila alichonacho kusaidia mapambano, ili wananchi wake wapate uhuru wao. Mh Mbowe akitoa hata sh1000 ujue siku ruzuku akiingia tu anakata hela yake kwa kisingizio cha kukidai au kukikopesha chama.

[4] Mwisho kabisa wakati mzee Nelson amefungwa jela takriban miaka 27, wananchi wake na wanaharakati mbali mbali wa ndani na nje ya nchi yake walionekana kuguswa, na kumpambania kwa njia mbali mbali. Bongo toka mh Mbowe afungwe ni week ya tatu tu sasa, lkn tayar ashaanza kusahaulika mapema sana utafikiri hakuna mwanasiasa anaeitwa mbowe nchini.

So hizo ndio sababu za mimi kupingana na watu hao wanaojaribu kufananisha nguvu za gari na treni. Haya ndugu zangu mwenye vigezo vya kumlinganisha mh mbowe na aliekuwa mzee wetu hayati Nelson anakaribushwa kuchangia na kuweka vigezo vyake hapa. Asanteni.
To give him the title "Mandela of Tanzania" is to elevate demon's character to that of an angel.
 
Back
Top Bottom