Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.
Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.
Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.
Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.
Updates 10.01.2025
Freeman Mbowe ameanza kuzungumza na Taifa na anaeleza kwa kirefu uanzishwaji wa Chadema, wapi ilipotoka na ilipo, magumu aliyopitia kupigania demokrasia na utawala bora
Pia anazungumzia nyakati ngumu chama hicho kimepitia hasa katika utawala wa Rais Magufuli na jinsi alivyohakikisha chama kinaendelea kufanya kazi hata katika mazingira magumu yaliyokuwepo
Kuhusu uasisi wa Chadema Freeman anasema;
"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.
"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.
"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.
Magumu anayokumbuka;
"Kumekuwa na ugumu wa kukiendesha Chama baada ya kufungiwa kwa miaka Saba. Kwa miaka hiyo Saba tulishindwa kufanya majukumu ya kisiasa kwahiyo nyingi za Chama zilikwama.
"Tulianza kufanya shughuli za Chama Tarehe 4, Machi 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kwamba like zuio haramu la kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake limeondolewa pale ndipo tulianza kukipanga Chama upya.
"Tulijikuta katika kipindi kigumu sana cha miaka miwili kukipanga Chama chetu kuanzia ngazi ya Vitongoji kule chini mpaka kufika ngazi ya Taifa, tukajikuta ndani ya Serikali za Mitaa, huku tukifanya chaguzi ndani ya Chama na mwaka huu tuna uchaguzi mkuu na kwa sababu tunajua kalenda ya sheria ya vyama vya siasa inatulazimisha lazima tupate viongozi wapya ili Chama kiwe halali"
Akizungumzia wanaoropoka na kutoa tuhuma bila ushahidi;
"Huwezi ukaibagaza taasisi ambayo unataka kuiongoza kwamba imejaa rushwa, halafu ukiambiwa baba hebu toa mfano mmoja wa rushwa na wewe ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama kuhusu hiyo rushwa. Ilezee dunia ione, unatoka tu Mama Abdul, Abdul.. Mambo ya kihuni! Sitaki sana kwenda kwenye engo hiyo ila wenye CHADEMA yao wataamua, taasisi yao iko salama kiasi gani?
Awaomba vijana wa Diasspora waache matusi;
"Kwenye kampeni hizi naona kuna kikundi cha watu wachache wasiozidi 30 wanaojiita diaspora wakati diaspora ina watu wengi kwa maelfu tusije tukawachafua kwa kikundi cha watu wachache wanaoshinda mitandaoni kutukana"
Amshangaa Mzee Slaa;
"Akina Dkt Wilbroad Slaa ambao walikimbia CHADEMA wakaenda Chama cha Mapinduzi wakapewa na zawadi ya ubalozi, eti leo naye amekuwa ndiye mpiga debe mkubwa wa Makamu Mwenyekiti wangu kutaka apewe Mwenyekiti wa chama na kubeza na kutweza watu wengine wa vyama vingine vya siasa.
: Kwanini nilikutana na Samia mara tu baada ya kutoka gerezani?
Mbowe: "nilifuatwa gerezani na Mufti pamoja na Maaskofu, wakaniambia serikali imeamua haina nia tena ya kuendelea na kesi ya ugaidi. Nikawajibu mimi sikujishitaki, wao ndiyo walionishitaki na wanajua wenyewe kwanini walinishitaki. Nikawaambia kama wameamua wenyewe kufuta kesi basi sawa. Wakaniambia lakini Mhe Rais anaomba mkutane mfanye kikao na sisi tunaomba mkutane. Sasa umefuatwa na Mufti pamoja na Maaskofu, wanakwambia ukutane na Rais, mimi siwezi kuwa na jeuri ya kuwakatalia viongozi wa dini. Nilipokutana na Rais alitaka tufanye mazungumzo ya kufanya maridhiano. Nikamwambia Mhe Rais mimi ni kiongozi wa Chama, siwezi kufanya maridhiano binafsi. Ngoja kwanza nikazungumze na wenzangu katika Chama. Ndipo tukafanya kikao cha Kamati Kuu, Chama kikabariki na timu yetu ya kwenda kwenye maridhiano ikaundwa. Na upande wa pili nao wakaunda timu yao iliyokuwa chini ya Mhe Kinana. Mazungumzo yakaanza. Mpaka hapo hakuna uamuzi wowote binafsi kutoka kwa Mbowe uliokipeleka Chama kwenye vikao vya maridhiano. Yalikuwa ni maamuzi ya Chama"
Mbowe asema hamwogopi Lissu;
"Hakuna mtu ambaye ni tishio kwangu, hata nikishindwa haitakuwa shida, ni sehemu ya demokrasia ambayo tumeijenga kwamba chama chetu kina kila aina ya ubaya na uzuri ni jambo jema na mimi nafarijika sana nimeijenga taasisi, ina onekana ina mvuto. Ni taasisi kubwa. Hata Lissu akishindwa na wengine wote walioshindwa tunawahitaji. Tunahitajiana pamoja na tofauti zetu"
Kuhusu Uchaguzi wa chama;
"Ndoto yangu katika uchaguzi huu ni kwamba utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki, na utarushwa mubashara. Hakuna kitakachofanyikia chumbani, vyote itakuwa ni wazo. Mtu atanyanyuka na kwenda kupiga kura wazi. Baada ya hayo yote wapiga kura halali wakisema Mwenyekiti inatosha naomba upumzike, nitawashukuru na nitampongeza, nitamtakia heri na kumkumbatia aliyenishinda na pia kuwataka wale wote waliokuwa wananiunga mkono tofauti zetu ziishie pale, na wamuunge mkono aliyeshinda ili tuweze kwenda mbele kwa ajili ya kuijenga taasisi na demokrasia katika nchi yetu "
Asipochaguliwa atafanya nini;
"Ndoto yangu katika uchaguzi huu ni kwamba utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki, na utarushwa mubashara. Hakuna kitakachofanyikia chumbani, vyote itakuwa ni wazo. Mtu atanyanyuka na kwenda kupiga kura wazi. Baada ya hayo yote wapiga kura halali wakisema Mwenyekiti inatosha naomba upumzike, nitawashukuru na nitampongeza, nitamtakia heri na kumkumbatia aliyenishinda na pia kuwataka wale wote waliokuwa wananiunga mkono tofauti zetu ziishie pale, na wamuunge mkono aliyeshinda ili tuweze kwenda mbele kwa ajili ya kuijenga taasisi na demokrasia katika nchi yetu
Amzungumzia Tundu Lissu;
"Lissu anagombea na mimi nagombea tafsri yake ni nini? Ni fahari wawili hawakai zizi moja. Kuna fahari wawili ndani ya CHADEMA. Ukiangalia 'trend' za ndani ya Chama Lissu amekuwa ana 'act' kama mwenyekiti wa chama na kutoa matamko kutoa kauli kama kama mwenyekiti wa chama wakati ni ni msaidizi wangu bila hata bila hata kuni 'Consult' mwenyekiti wake