Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.
Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.
Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.
Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.
Updates 10.01.2025
Freeman Mbowe ameanza kuzungumza na Taifa na anaeleza kwa kirefu uanzishwaji wa Chadema, wapi ilipotoka na ilipo, magumu aliyopitia kupigania demokrasia na utawala bora
Pia anazungumzia nyakati ngumu chama hicho kimepitia hasa katika utawala wa Rais Magufuli na jinsi alivyohakikisha chama kinaendelea kufanya kazi hata katika mazingira magumu yaliyokuwepo
Kuhusu uasisi wa Chadema Freeman anasema;
"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.
"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.
"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.
Magumu anayokumbuka;
"Kumekuwa na ugumu wa kukiendesha Chama baada ya kufungiwa kwa miaka Saba. Kwa miaka hiyo Saba tulishindwa kufanya majukumu ya kisiasa kwahiyo nyingi za Chama zilikwama.
"Tulianza kufanya shughuli za Chama Tarehe 4, Machi 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kwamba like zuio haramu la kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake limeondolewa pale ndipo tulianza kukipanga Chama upya.
"Tulijikuta katika kipindi kigumu sana cha miaka miwili kukipanga Chama chetu kuanzia ngazi ya Vitongoji kule chini mpaka kufika ngazi ya Taifa, tukajikuta ndani ya Serikali za Mitaa, huku tukifanya chaguzi ndani ya Chama na mwaka huu tuna uchaguzi mkuu na kwa sababu tunajua kalenda ya sheria ya vyama vya siasa inatulazimisha lazima tupate viongozi wapya ili Chama kiwe halali"
Akizungumzia wanaoropoka na kutoa tuhuma bila ushahidi;
"Huwezi ukaibagaza taasisi ambayo unataka kuiongoza kwamba imejaa rushwa, halafu ukiambiwa baba hebu toa mfano mmoja wa rushwa na wewe ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama kuhusu hiyo rushwa. Ilezee dunia ione, unatoka tu Mama Abdul, Abdul.. Mambo ya kihuni! Sitaki sana kwenda kwenye engo hiyo ila wenye CHADEMA yao wataamua, taasisi yao iko salama kiasi gani?
Awaomba vijana wa Diasspora waache matusi;
"Kwenye kampeni hizi naona kuna kikundi cha watu wachache wasiozidi 30 wanaojiita diaspora wakati diaspora ina watu wengi kwa maelfu tusije tukawachafua kwa kikundi cha watu wachache wanaoshinda mitandaoni kutukana"