Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Nadhani tusikilize atakayoongea kesho labda anazo sera zake zingine nje ya Katiba ya Chadema, lakini kumbuka kwamba sera zote za Chadema ziko ndani ya Katiba yake na miongozo yake, miongozo hii haikutungwa na mtu mmoja.

Ukitaka kuleta jambo jipya ni lazima uombe kwa Kamati kuu kubadili Katiba na useme kwanini
Jibu hoja Acha kuweweseķa? Ina maana anataka miaka 5 mingine ili atufanyie kipi?
Kama hana agenda,hoja au maono atupishe tu
 
Anazungumzia kundi lao la whatsaap lilianzishwa na wenje members wakiwa ni wenje, yeye, lema, msigwa, mnyika, lissu, anasema aliomba kujitoa kutokana kipindi kigumu alichopitia cha kupoteza mali zake, shamba lake lakini hao washikaji walimkatalia kujitoa
Kupoteza mali na group la WhatsApp vina uhusiano gani?
Atakuwa kachanganyikiwa huyo
 
Sasa huu ni muda wenu wa kunadi sera za mnaowaunga mkono na kumwangusha, ni nafasi nzuri ya kushawishi wapiga kura kwamba Jamanii eeee!! Mbowe hana sera mchagueni huyu mtu wetu sera zake hizi hapa.

Msipoteze muda siku zinaisha
Lisu alisema agenda zake akichaguliwa.
Huyu bwana wenu Mobutu mbona hasemi sera zozote zaidi ya masimango eti ya kusaidia watu hiki na kile?
Amechoka akili na amechokwa
 
Akiulizwa maswali na watangazaji wa clouds wa PB anarukaruka kama maharage yanayochemka jikoni. anasema anatuhumiwa tu bila ushahidi
 
Anazungumzia kundi lao la whatsaap lilianzishwa na wenje members wakiwa ni wenje, yeye, lema, msigwa, mnyika, lissu, anasema aliomba kujitoa kutokana kipindi kigumu alichopitia cha kupoteza mali zake, shamba lake lakini hao washikaji walimkatalia kujitoa
Daaahhhh...mwamba anajishushia heshima sana kama amefikia kutafuta cheap sympathy kwa kukumbushia mali alizoibiwa ambazo sasa hiv mama abdul ndio kamlipa mabilion ya fedha kama fidia na yeye akaamua kukitoa cdm kama kulipa fadhila
 
Anasema viongozi wa dini walimuomba akaongee na rais kuhusu muafaka, kufanya maridhiano, anasema yeye ni nani hata akatae? Lissu alikuwa uhaibuni wakati anatoka gerezani na kwenda ikulu
 
Mbowe kiukweli namkubali,ila kwa hili anachemka!Kaulizwa Swali kwamba wakati wa kujadili vyama vingi,ilionekana kwamba wengi wakisema wanataka chama Kimoja,wachache wakisema wanataka vyama vingi.Kama ni hivyo na Wewe Mbowe usitumie mfumo huo wa wengi wanakutaka, wachache hawakutaki.Jibu la Mbowe ooh wengine wanakimbia nchi.Tundu Lissu huko ubelgiji si alienda kwa akili ya matibabu.Hoja dhaifu ya Mbowe.
Kama kwel kasema haya bas sasa mwamba akili ilisha chochora kabaki box tupu
 
Anasema kuhusu kutengeneza maridhiano yeye ni wa kwanza kufanya hivyo na lissu ni wa pili kufanya hivyo, ikaundwa kamati ya watu watano kuunda kamati ya maridhiano, watano wa ccm na watano wa chadema jumla kumi. Hoja waachiwe huru wafungwa wa kisiasa na wale waliokimbia nchi warudi
 
Anasema mtu kupingana na yeye ni haki yake ya msingi, amewapa watu wake fursa ya kusema, kujadili na hataki asujudiwe
 
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.

Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.

Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.

Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.

Updates 10.01.2025

Freeman Mbowe ameanza kuzungumza na Taifa na anaeleza kwa kirefu uanzishwaji wa Chadema, wapi ilipotoka na ilipo, magumu aliyopitia kupigania demokrasia na utawala bora

Pia anazungumzia nyakati ngumu chama hicho kimepitia hasa katika utawala wa Rais Magufuli na jinsi alivyohakikisha chama kinaendelea kufanya kazi hata katika mazingira magumu yaliyokuwepo

Kuhusu uasisi wa Chadema Freeman anasema;

"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.

"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.

"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.

Magumu anayokumbuka;

"Kumekuwa na ugumu wa kukiendesha Chama baada ya kufungiwa kwa miaka Saba. Kwa miaka hiyo Saba tulishindwa kufanya majukumu ya kisiasa kwahiyo nyingi za Chama zilikwama.

"Tulianza kufanya shughuli za Chama Tarehe 4, Machi 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kwamba like zuio haramu la kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake limeondolewa pale ndipo tulianza kukipanga Chama upya.

"Tulijikuta katika kipindi kigumu sana cha miaka miwili kukipanga Chama chetu kuanzia ngazi ya Vitongoji kule chini mpaka kufika ngazi ya Taifa, tukajikuta ndani ya Serikali za Mitaa, huku tukifanya chaguzi ndani ya Chama na mwaka huu tuna uchaguzi mkuu na kwa sababu tunajua kalenda ya sheria ya vyama vya siasa inatulazimisha lazima tupate viongozi wapya ili Chama kiwe halali"

Akizungumzia wanaoropoka na kutoa tuhuma bila ushahidi;

"Huwezi ukaibagaza taasisi ambayo unataka kuiongoza kwamba imejaa rushwa, halafu ukiambiwa baba hebu toa mfano mmoja wa rushwa na wewe ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama kuhusu hiyo rushwa. Ilezee dunia ione, unatoka tu Mama Abdul, Abdul.. Mambo ya kihuni! Sitaki sana kwenda kwenye engo hiyo ila wenye CHADEMA yao wataamua, taasisi yao iko salama kiasi gani?

Mwamba rasmi katika cap simba:

Gfq-SyFXwAAhuk9.jpeg


Ggy4VqEWcAEdkcH.jpeg
 
Back
Top Bottom