Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Freeman Mbowe kuzungumza na Taifa Ijumaa, Januari 10, 2025

Kupitia mikononi mwa Mbowe sio hoja ya kufanya Mbowe aendeleea kuwa mwenyekiti.Hata akiwa nje ya uongozi anaweza kufanya watu wapitie Bado mikononi mwake.Achia kiti Mbowe bila kuingia kwenye box ili uheshimike zaidi.
 
Bora atangaze kustaafu uenyekiti ili aendelee juwa na heshima. Ukiona viongozi wenzako wanampigia chapuo makamu wako ufahamu kuwa imani kwako imekwisha.
Ni kwel. Maana hata ukishinda ,utafanyaje nao kazi hali wamekuonyesha kuwa wanataka kufanya kazi na mtu mwingine na sio wewe?
 
Mbowe ni pandikizi la ccm lililo lewa madaraka kama maccm.
Sasa kama mwamba ni pandikizi, hata Lissu akishinda, si inamaana kwamba jamaa atakua bado anapenyeza info kwa ccm maana bado atabaki kwenye inner circle za cdm!!
 
Sasa hapa mbowe anafanya kampeni au nini? Naona anaishia tu kumponda na kumsigina lissu tu
 
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kesho Ijumaa tarehe 10/01/25 anatarajiwa kuzungumza na Taifa kupitia Clouds Media kuanzia saa 12 asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast.

Freeman Mbowe mwanasiasa mwenye mvuto zaidi kwa sasa hapa nchini anatetea nafasi yake ya uenyekiti katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Freeman Mbowe amejitofautisha na wapinzani wake kisiasa kwa jinsi alivyo mnyenyekevu, anayechagua maneno ya kuzungumza, anayeheshimu viongozi wenzake, asiyetoa shutuma bila mpangilio, anayetambua mchango wa wenzake, asiyetoa siri za chama na asiyeropoka hovyo.

Kwa mujibu wa tafiti kupitia wajumbe kadhaa wa Mkutano mkuu kote nchini Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura zote za wajumbe.

Molemo Media Itakuwa live kuwaletea mazungumzo ya Freeman Mbowe na Taifa.

Updates 10.01.2025

Freeman Mbowe ameanza kuzungumza na Taifa na anaeleza kwa kirefu uanzishwaji wa Chadema, wapi ilipotoka na ilipo, magumu aliyopitia kupigania demokrasia na utawala bora

Pia anazungumzia nyakati ngumu chama hicho kimepitia hasa katika utawala wa Rais Magufuli na jinsi alivyohakikisha chama kinaendelea kufanya kazi hata katika mazingira magumu yaliyokuwepo

Kuhusu uasisi wa Chadema Freeman anasema;

"Mimi nilikuwa miongoni kwa waanzilishi wa CHADEMA. Kipindi hicho nilikuwa mdogo sana kati ya watu 10 tulioanzisha Chama hiki. Nilikuwa na umri wa miaka 30.

"Nilikuwa nafanya biashara na familia yetu ilikuwa ya Wafanyabiashara na Mzee wangu baada ya vuguvugu la Uhuru alikuwa kwenye siasa aligombea ubunge 1965 alikuwa rafiki wa karibu na Mwl Julius Nyerere. Sisi familia yetu ilikuwa ikifanya biashara kabla ya uhuru wa nchi yetu.

"Niliingia kwenye siasa nikawa nafanya vyote, siasa na Biashara"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA.

Magumu anayokumbuka;

"Kumekuwa na ugumu wa kukiendesha Chama baada ya kufungiwa kwa miaka Saba. Kwa miaka hiyo Saba tulishindwa kufanya majukumu ya kisiasa kwahiyo nyingi za Chama zilikwama.

"Tulianza kufanya shughuli za Chama Tarehe 4, Machi 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kwamba like zuio haramu la kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake limeondolewa pale ndipo tulianza kukipanga Chama upya.

"Tulijikuta katika kipindi kigumu sana cha miaka miwili kukipanga Chama chetu kuanzia ngazi ya Vitongoji kule chini mpaka kufika ngazi ya Taifa, tukajikuta ndani ya Serikali za Mitaa, huku tukifanya chaguzi ndani ya Chama na mwaka huu tuna uchaguzi mkuu na kwa sababu tunajua kalenda ya sheria ya vyama vya siasa inatulazimisha lazima tupate viongozi wapya ili Chama kiwe halali"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
Hi ni aibu kuandika upupu huu! hakuna ata mmoja anaekuunga mkono ata kwenye comment!
 
Anazungumzia kundi lao la whatsaap lilianzishwa na wenje members wakiwa ni wenje, yeye, lema, msigwa, mnyika, lissu, anasema aliomba kujitoa kutokana kipindi kigumu alichopitia cha kupoteza mali zake, shamba lake lakini hao washikaji walimkatalia kujitoa
 
Back
Top Bottom