Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna watu wakifa kwa kweli unaona ile mantiki ya Mungu alimpenda zaidi. Maana mtu anapendwa sana na wanadamu wenzake, lakini gjafla hamnaye tena.View attachment 2834847
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba , Viongozi wakuu wa Chadema , Tundu Lissu na Freeman Mbowe leo 06/12/2023 , Wamebahatika kuwa miongoni mwa watu waliohudhuria Ibada ya mazishi ya Askofu Kweka .
Akizungumza kwa Taabu kwenye ibada hiyo kutokana na kujawa na Majonzi makubwa , Freeman Mbowe amemtaja Askofu Kweka kama sehemu ya familia yake , kutokana na kuwa karibu mno na Wazazi wake , huku akimtaja kwamba ndiye aliyemfungisha ndoa na ndiye aliyeongoza Mazishi ya Mama yake na Baba yake .
Mbowe amemtaja Baba Askofu Dr Kweka kuwa mfano wa kuigwa na kwamba matendo yake yatadumu milele .
Baba wa huruma mtazame kwa jicho la huruma mtumishi wako huyo aliyeyatoa maisha yake kwaajili ya kukutumikia. Pale alipopungukiwa, aishuhudie huruma yako maana wewe ni Bwana wa msamaha.