Wadau, amani iwe kwenu.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wana CHADEMA wakihoji ukimya wa viongozi wa chama hicho katika kuzungumzia suala la kupotea kwa Ben Saanane. Maoni ya wana CHADEMA wengi ni kwamba pamoja na kuelekeza lawama kwa Jeshi la Polisi kutokana na kuizika miili ya watu saba bila ya kufanyiwa uchunguzi, mzigo mkubwa anashushiwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe. Ben kapotea huku Bosi wake Mbowe anaendelea kuponda raha huko Ulaya. Hajashtushwa na wala hataki kushtushwa na kupotea kwa Ben Saanane. Kwa wadhifa wa Ben Saanane, haiingii akilini kuona Bosi wake akiendelea kuponda raha huko Ulaya badala ya kusitisha safari yake kuungana na ndugu na marafiki wa Ben kumtafuta. Jawabu la haraka haraka ni kwamba Mbowe anajua nini kinaendelea juu ya kupotea kwa Ben.
Mapema leo asubuhi, ndugu yangu Malisa Godlisten Joseph amehoji kwa uchungu mkubwa sana and I can feel, kitendo cha Gazeti la Tanzania Daima ambalo kwa mujibu wa Malisa ni kwamba ni gazeti lao kutoipa kipaumbele taarifa ya kupotea kwa Ben kama ilivyoelezwa kwenye Press Conference ya Umoja wa Kuhoji Tanzania. Kwa mujibu wa Malisa, Gazeti la Tanzania Daima limeipuuza Taarifa yao na badala yake wamempamba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwa Bado yupo yupo CCM. Malisa anasema kuwa hata gazeti la Kada wa CCM, Majira limewapiku Tanzania Daima.
Nikuhakikishie ndugu yangu Malisa kuwa haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya. Yamepangwa na kupangika. Awali nilipofichua uhusika wa Mbowe juu ya kupotea kwa Ben mlinishambulia na kuniona kuwa ni mchonganishi. Sasa yamewakuta. Akili imeanza kuwarejea na sasa mnaungana na Lizaboni kimya kimya.
Wapo pia wanaosema kuwa Freeman Mbowe anastahili kuhojiwa kutokana na upotevu wa Ben. Naungana nao moja kwa moja kwani familia yake iliwajibika ila Mbowe na viongozi wenzake hawakuwajibika na hawapo tayari kuwajibika.
Kurasa zao za facebook hakika zimechafuka. Mashambulizi kwa Mbowe yamepamba kila kona. Wapo wanaosema waziwazi lakini wengine wanahoji kimya kimya. Mwisho wa siku akili itawarejea na wataanza kupaza sauti.
Nimalizie kwa kusema kuwa kabla hujamtafuta mbaya wako nje ya nyumba, jaribu kutafakari kwa kina mahusiano yako na watu wa ndani ya nyumba yako.
View attachment 445613 View attachment 445614 View attachment 445615