Pre GE2025 Freeman Mbowe: Naagiza ngazi zote za chama ziandae wagombea wa kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Napongeza maamuzi na maagizo ya Mkt Mbowe kushiriki chaguzi
kuendelea kususia uchaguzi ni kuendelea kukidhoofisha chama ,
Ni Bora kutumia Kila nafasi inayotokea
Uchaguzi utawaongezea nguvu upinzani hata Kama sio kwa kiwango tunachotamani

INGAwa naendelea na msimamo wangu wa kumshauri achie ngazi kwa heshima , aachie chama kitegemee Mifumo imara sio kiongozi imara
 
Hahaha

kaamua kukomaa na uwekezaji wa kwny Siasa unalipa sana
 
Katiba iliyopendekezwa mliigeuzia jina mkaiita Katiba inayodekezwa !!! Mkawa mnataka ile rasimu ya maoni ya warioba ndio iwe katiba kamili hivi mlikuwa serious??? Kuleni chuma hicho hakuna cha katiba mpya 😃😃

..hakuna Katiba itakayopendekezwa ambayo itaungwa mkono na kila mtu 100%.

..hoja yangu ni kwamba Ccm walikamilisha mchakato ktk bunge maalum na kupitisha Katiba pendekezwa.

..sasa haijulikani kwanini Ccm hawakuileta katiba hiyo kwa wananchi ili ipigiwe kura ya kukubaliwa, au kukataliwa.
 
Chadema mbona hamueleweki si mmesema hamtashiriki uchaguzi mkuu? Huku sultan aanasema mjiandae au hampo pamoja kwenye maamuzi?

Cc; Erythrocyte
 
 
Katiba mpya na tume huru zimepatikana!!?

Mbowe. Umefika bei!!?

Hakuna katiba wala time huru uchaguzi wa Nini huo!!?

RIP Tanzania!
 
Dai la Katiba mpya ni dai la Wanasiasa wajanja wajanja ambao hupenda kusingizia kuwa ni hitaji la Wananchi

kwa kuwa hao hao waliomshawishi Rais Msikivu kuwahi kutokea hapa Nchini Dr Kikwete aanzishe mchakato wa Katiba mpya ndio hao hao walimshinikiza asistishe asimalizie na kura ya maoni na akawasikilize

kipaumbele Chao hao WajasiriaSiasa ni ruzuku na sio Katiba mpya hivyo Katiba mpya imekosa mwamko na na msisitizo


Sasa hivi kipaumbele cha Freeman Mbowe ni kuhakikisha kila eneo lipate Mgombea mwenye Mvuto hata kama hawatoshinda anajua itasaidia kwny kuongeza fedha za Ruzuku …
 

..Kati ya Katiba Mpya na hii ya sasa ipi ina afadhali kwetu wananchi wa kawaida?

..Je, wanaong'ang'ania katiba iliyopo ruzuku sio matamanio na kipaumbele kwa chama chao?
 
..Kati ya Katiba Mpya na hii ya sasa ipi ina afadhali kwetu wananchi wa kawaida?

..Je, wanaong'ang'ania katiba iliyopo ruzuku sio matamanio na kipaumbele kwa chama chao?
Alieanzisha Mchakato wa Katiba mpya alikuwa Rais kutokea NLD au TLP?

Mwenyekiti wa mchakato wa Katiba Mpya Mzee Warioba ni NCCR Mageuzi ?

unajua Prof Mwesiga Baregu Mjumbe wa Tume ile Chama chake kilimtaka ajitoe kwmy mchakato ule?

unajua kuna vyama vilijitoa katika hatua za mwisho mchakato ule ukwame leo wanataka uendelee pale ulipoishia wakati enzi zile walitaka mchakato uanze upya ?
 

..mchakato haukukwama.

..bunge maalum lilikamilisha kazi yake na liliandika KATIBA PENDEKEZWA.

..hatua iliyotakiwa kufuata ni kuandaa kura ya maoni kukubali au kukataa Katiba Pendekezwa.

..kwasababu Ccm ndio wenye serikali, bunge, na tume ya uchaguzi, na hawakuitisha kura ya maoni, basi wanastahili lawama kwa kuitupilia mbali Katiba Pendekezwa.
 
Tususie uchaguzi bila katiba mpya, sasa hivi shiriki uchaguzi kwa nguvu zote, bila ya Katiba mpya?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…