Gift mzalendo
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 1,856
- 2,417
Napongeza maamuzi na maagizo ya Mkt Mbowe kushiriki chaguziAkihutubia kwenye mkutano wa BAWACHA, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe emetoa agizo kwa Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika kuhakikisha ngazi zote za chama nchi zima zinaandaa viongozi wa kugombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025. Viongozi hawa wawe na sifa za kushinda uchaguzi.
"Niwaagize mama zangu, rudini kwenye majimbo yenu kakipangeni chama, kila kitongoji, kila kijiji, kila mtaa. Hakuna kitongoji ambacho kitapita bila kupingwa na CHADEMA katika uchaguzi ujao, hakuna"
Mbowe ameongeza kuwa viongozi wazembe ambao hawataweka watu wa kugombea nafasi za uongozi kwenye chaguzi zijazo watachukuliwa hatua.
Amesema macho yote ya watanzania yapo kwa CHADEMa hivyo ni lazima wasimamishe viongozi kwa kila ngazi.
"Naagiza, na siyo kwa BAWACHA peke yake, katibu mkuu tafadhari na mfumo mzima wa mabaraza yote ya chama, kila kiongozi ahakikishe kila nafasi inayogombewa katika serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, lazima CHADEMA iweke mgombea, na siyo mgombea tu wa kujaza nafasi, mgombea wa ushindani wa kushinda."
Amewataka kwenda kusuka chama kwa nguvu ili waizike CCM kwenye chaguzi zijazo.
kuendelea kususia uchaguzi ni kuendelea kukidhoofisha chama ,
Ni Bora kutumia Kila nafasi inayotokea
Uchaguzi utawaongezea nguvu upinzani hata Kama sio kwa kiwango tunachotamani
INGAwa naendelea na msimamo wangu wa kumshauri achie ngazi kwa heshima , aachie chama kitegemee Mifumo imara sio kiongozi imara