Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

View attachment 2744983

Tunalaani ukamataji, unyanyasaji, usumbufu unaofanywa na Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Mhe Tundu Lissu, viongozi wengine waandamizi wa ngazi mbalimbali, wanachama na wapenzi wetu huko Mkoani Arusha.

Kwa uzito huo huo, tunalaani uzuiaji wa mikutano yetu na shughuli halali za kisiasa huko Ngorongoro, Loliondo na Karatu.

Tuna hofu kubwa ya usalama wa watu wetu na ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia. Tunafuatilia kwa karibu na tunadai kuachiliwa haraka na bila masharti kwa watu wetu wote!

Freeman Mbowe
Mtandao wa X

Pia soma: Breaking News: - Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Acheni matusi kwenye mikutano yenu na mukome kudhalilisha dini ya kiislamu na waislamu lakini pia muache ubaguzi kuwadhalilisha wazanzibari na jengeni hoja kwenye majukwaa muimarishe chama chenu muvune wanachama wapya ili uchaguzi ukiwadia tuone malengo ya chadema msiwe kama ngombe

Tundu Lissu zamani alikuwa mjengaji mzuri wa hoja na tukimkubali sana lakini sasa ni kama ameishiwa na maneno, anahubiri demokrasia ya nchi za ulaya iwe exercised Tz ili mashoga waoane hilo jambo kwa utamaduni wetu na kwa maarisho ya dini yetu halikubaliki.
 
Back
Top Bottom