Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

Freeman Mbowe: Ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia

Huyo jamaa nafikiri ni muunga juhudi uchwara hata enzi ile ya awm5,alikuwa anatuchora kinara huku akitoa namba kisiri siri [emoji23]
Hao ndiyo mazuzu wanafanya kuunga mkono wakati majumbani mwao wanashindia kashata
 
Huyo makamu anatakatl kutuvurugia amani yetu wakati tunajua fika yeye akiona mambo yamemchachia anakimbilia ubalozi na kusindikizwa kwenda airport kukwea pipa kwenda ughaibuni hata familia yake haipo nchini. Ashindwe na alegee asituchafulie nchi yetu sisi wengine hatuna la kukimbilia.

Mnaficha kitu gani ngorongoro?
 
Usituongelee susi jiongelee wewe. Anafaa sana na hakika tutampigania na tutapigana naye hadi tone letu la mwisho
Aijakusemea wewe endelea naye mwenzako hachelewi kukimbilia ubalozi kisha kusindikizwa hadi ughaibuni wewe mwenzangu mimi tunabakia humu humu Tanzania. Garagabaho.
 
Eti ashugulikiwe!!!!
Alishindwa kumshughulikia yule sheitwan wenu itakuwa hawa wasaidizi wake?
Ashughulikiwe na wafuasi wake wanaofuata upepo kama wewe mwenzako hakawii kukimbilia ubalozini na kupelekwa airport kupanda ndege kurudi alikotoka wewe na mimi tunabakia hapa hapa.
 
Kuna nini Ngorongoro mpaka pawepo katazo kwa Lissu na waandishi wa habari.
Haya maswali Lissu alipaswa aziulize mamlaka husika badala ya kufunga barabara na wafuasi wake. Foolish pride, halafu anataka uongozi wa nchi na akili hiyo
 
Aijakusemea wewe endelea naye mwenzako hachelewi kukimbilia ubalozi kisha kusindikizwa hadi ughaibuni wewe mwenzangu mimi tunabakia humu humu Tanzania. Garagabaho.

Kwamba anakimbilia ubalozi mnapotaka kumwua? Mumiani wakubwa nyie.

Bure kabisa!
 
Aijakusemea wewe endelea naye mwenzako hachelewi kukimbilia ubalozi kisha kusindikizwa hadi ughaibuni wewe mwenzangu mimi tunabakia humu humu Tanzania. Garagabaho.
Anakimbia Risasi za Wauaji kama wewe.
 
Umaarufu au ulimbukeni
Ulimbukeni,??, wewe unaweza kujilinganisha na Lissu ata kwa 0,001%, Sarakasi zote hizi za kukamatwa ni kiwewe cha kumuogopa. Lissu ni mtu na nusu ingawa watu mmeshikiwa akili lakini huo ndiyo ukweli. Limbukeni ni nyie mnaobeba viatu vya watu lakini yeye shida yake ni haki kama ni umaarufu keshakuwa nao tangu kitambo.
 
View attachment 2744983

Tunalaani ukamataji, unyanyasaji, usumbufu unaofanywa na Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Mhe Tundu Lissu, viongozi wengine waandamizi wa ngazi mbalimbali, wanachama na wapenzi wetu huko Mkoani Arusha.

Kwa uzito huo huo, tunalaani uzuiaji wa mikutano yetu na shughuli halali za kisiasa huko Ngorongoro, Loliondo na Karatu.

Tuna hofu kubwa ya usalama wa watu wetu na ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia. Tunafuatilia kwa karibu na tunadai kuachiliwa haraka na bila masharti kwa watu wetu wote!

Freeman Mbowe
Mtandao wa X

Pia soma: Breaking News: - Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Mkishindwa kuzisoma na kuzielewa mbinu za watu wanaotapatapa wakati huu na kufanya makosa ya kuwapa mwanya, lawama itakuwa kwa chama chenu.

CCM wapo katika hali ngumu sana wakati huu. Watatumia kila njia inayowasaidia kujiondoa katika hali hiyo ngumu.

Waonyesheni waTanzania sasa, kuwa mmefikia ukomavu wa kujua mbinu mbovu na kuzishinda.

Mkiingia kwenye mitego ya kijinga inayowekwa na CCM wakati huu itakuwa wazi hamjawa na ukomavu wa kutosha.

Hili swala la Loliondo/Ngorongoro ni tufufu yenu yenye nguvu, lakini CCM wapo tayari kuligeuza kuwa udhaifu wenu mkubwa kama chama.

Msifanye papara, Makamu Mwenyekiti atatoka tu kama hakuna sheria iliyovunjwa. CCM hawana uwezo tena wa kupindisha sheria na dunia nzima isijue. Wanatafuta fursa chache kama hizi kujaribu kuhadaa dunia waonekane bado wanao uhalali kuwa watawala.
 
Back
Top Bottom