Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Kwa hiyo Mbowe alidhania kuachiwa kufanya mikutano ya hadhara ni ndiyo ruhusa ya kuvunja sheria??View attachment 2744983
Tunalaani ukamataji, unyanyasaji, usumbufu unaofanywa na Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Mhe Tundu Lissu, viongozi wengine waandamizi wa ngazi mbalimbali, wanachama na wapenzi wetu huko Mkoani Arusha.
Kwa uzito huo huo, tunalaani uzuiaji wa mikutano yetu na shughuli halali za kisiasa huko Ngorongoro, Loliondo na Karatu.
Tuna hofu kubwa ya usalama wa watu wetu na ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inarejesha Utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia. Tunafuatilia kwa karibu na tunadai kuachiliwa haraka na bila masharti kwa watu wetu wote!
Freeman Mbowe
Mtandao wa X
Pia soma: Breaking News: - Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Uwache tu huo utawala wa mabavu uendelee kuliko huu ujinga anaoendekeza Lisssu. Umeambiwa na Polisi hakuna kwenda Ngorongoro, unakaidi. Unategemea Polisi wacheke na nyani?