Freeman Mbowe, ni wakati wako sasa wa kuachia ngazi kwa heshima, siasa za kuonewa huruma hazitoifikisha mbele CHADEMA

Tatizo nililoligundua kwako ni uwezo mdogo wa akili ulionao na hilo naamini sio ugonjwa ni kipaji tu ulichojaaliwa.

Nakusisitiza tena jifunze kujadili hoja katika mada na kuzijibu hiyo ndio njia nzuri zaidi yakukuza akili yako na kuondoa iko kipaji chako cha ujinga.

Hilo lakuanzisha chama kingine ni hoja nyingine ambayo ungepaswa kuianzishia mada ili wadau wajadili.

Pia ondoa ujinga akilini kwako kuwa sio kila anaetaka Mbowe akae pembeni ni mtu wa CCM wengine ni wanachama na wapenzi wa CDM haswaa.

Jifunze kuficha upumbavu mbele ya hadhira ili ujifunze kwa wenzio.
 
Wewe hapo una uwezo? upi? kupitia hizi coment? au una uwezo mwingine haujauonyesha humu?

Unachekesha sana,
 
Nisha kuuliza ni lazima upinzani utoke CDM? hakuna vyama vingine? kama Mbowe hafaia si kuna Vyama vingine? huo ushauri ushautoa pia kwingine?

Au wewe si unaweza ingia frint line? au umezaliwa kutoa tu ushauri ukiwa. yuma ya keybord?

Yaani kuna watu wamezaliwa kutoa ushauri tena ushauri wa kijinga
 
Kwani ni lazima wanao ongoza watokee CDM? Humu mnajifanya wajasiri on the ground hamuonekani.

Kama CDM haifai je hamuwezi anzisha chama kipya na CDM ikajifia zake?
Taifa limejaa wajinga sana
Huku kunijibu mara mbili mbili inaonesha namna gani maneno yangu yamekuingia.

Maandishi unayoandika hapa yanaonesha wewe ni mtu wa namna gani.

Watu wanaleta hoja wewe unaleta taarabu hivi kwa akili za namna hii kweli zinaweza kusaidia CDM kukua.

Matatizo unayoona ya CCM yanachangiwa na udhaifu wa vyama vya upinzani tulivyonavyo.

Kila nchi unayoona imefanya mabadiliko yakuvitoa vyama vya zamani ni ķwasababu viongozi wa vyama pinzani walionesha nguvu yao ya ushawishi.

Haujiulizi kwanini Chadema kabla ya 2015 ilikuwa ikiitisha maandamano wanafanikiwa na sasa hivi inashindikana.Kipindi iko katibu mkuu ni Dk.Slaa.

Haujiulizi kwanini Chadema kabla ya 2015 ilikuwa na nguvu sana vyuoni na sasa hivi haipo hiyo nguvu.

Nakusisitiza timia akili kama unayo usitumie kichwa kusukia nywele au kuvaa heleni tu.
 
Wewe hapo una uwezo? upi? kupitia hizi coment? au una uwezo mwingine haujauonyesha humu?

Unachekesha sana,
Siunaona sasa.

Wenzio tunajadili vitu vyenye akili timamu wewe unaonesha ujinga wako.

Ndugu jifunze kuficha upumbavu wako mbele za watu itakusaidia.

Kama kweli unaakili basi utajua kuwa unaandika pumba sana.
 
Unaonekana umeshapandisha sukari maana hadi kuandika umeanza kulewa,Frint line ndio unamaanisha nini.

Unapouliza kuwa hakuna vyama vingine kwahiyo unaamaanisha haujui kuwa hapa nchini tuna vyama vingi mfu na CDM ndio chama cha upinzani chenye nguvu Tanzania nzima.

Kama wewe ni mtetezi wa Mbowe hapa jukwaani basi anaemtetezi mwenye akili ndogo sana.

Kwahiyo wewe hauoni hoja ya mleta mada zaidi yakuandika mipasho tu.Haujaona hata mleta mada kamtaja Lissu hivi unadhani angekuwa haipendi Chadema angemtaja Lissu.

Kama haumkubali Lissu awe mwenyekiti CDM unamuona hana uwezo mzuri,je huo ujasiri wakuaminisha watu kuwa anaweza kuongoza Tanzania mliupata wapi.

Hapa ninachokiona wafuasi wa CDM wa aina yao wanaamini Mbowe ndio anaakili zaidi ya wote lakini bado wanaleta mgombea uraisi Lissu na wanamsifia majukwaani.

Yaani Lissu mnamuamini kuwa anaweza kuongoza Tanzania nzima yenye makabila,dini tofauti na watu tofauti tofauti lakini hamumuamini kama anaweza kuongoza Chama ambacho hakina nguvu Tanzania nzima.Mnajielewa kweli mnachopambania.
 
Machawa wa Mbowe wanapita Kama hawaoni uzi🤣🤣🤣
Chadema ni Kama NGOS ya kichaga
 
Unachokisema kwa kiasi fulani kina ukweli ndani yake hata mimi mwanzo kwa 100% Nilikuwa napinga kwa nguvu zote Mbowe kumpisha mtu mwingine wanaye mwamini ktk Chama kushika nafasi yake, kwasababu watu walio wengi walio kuwa wanataka Mbowe aachie madaraka walikuwa waasimu wake wa CCm na chama kilikuwa kina fanya vizuri. Hata hivi sasa chama bado kipo vizuri lakini ameshindwa kupambana na hujuma zinazofanyiwa chama chake na mara nyingi hakubaliani na wenzake kuchua mikakati mikali ya maamuzi kwasababu yeye ni mwanasiasa na mfanya bishara akifeli kwenye siasa biashara zina mbeba. Mwanzoni alikuwa na mikakati mizuri sana ya kukijenga chama na alitumia lasirimali zake nyingi pamoja na marafiki zake kukifikisha chama hapo, Mimi nadhani nikipindi cha Yeye kuwa mshauri wa chama kama Vile alivyo mtei au zito kwenye ACT alafu anaweza akurudi tena baada ya mapumziko kama ataitajika ila sijui anahofia nini kuwaachia wenzake waendeleze hilo gurudumu najua anakijua vizuri hicho chama na anawajua nje ndani viongozi wake wote, kulikuwa na malalamiko sana Mbowe alipo mchagua mashinji awe katibu ila alipongezwa sana alipo mchagua mnyika kuwa katibu. Sidhani kama itakuwa vibaya kwa yeye kwa sasa kuwaachia wengine madaraka, watu wanao weza kushika uwenyekiti kwa sasa CDM wapo wengi siyo Lisu, mnyika, wenje, Na wengine wengi tu sijawataja. Ila mchakato unapaswa kuwa mkali sana na wasiri kwasababu CDM kwa sasa nchini inachukuliwa na serikali kama kundi la hamas hujuma inaweza ikapenyezwa ili kukosa kiongozi Bora, kamati kuu ndiyo ipewe mandate yakupendekeza wagombea na kuwagrade kabla yakuwapeleka halmashauri kuu na mkutano mkuu na Mwenyekiti asiwe mmoja wapo wakutafuta mrithi wake hapa nina maana yangu
 
Tundu lisu hana charisma ya kuongoza taasisi kama chama. Lisu ni individualist (selfish) anayejiangalia yeye binafsi kabla ya mtu mwingine yeyote, hawezi kuongoza chama. Kama mnataka chama kife basi mpeni lisu huo uongozi.
Udhaifu kwa mwanadamu ndiyo ubinadamu ukitaka mtu perfect kwa asilimia mia itabidi utafute malaika nadhani umemtaja Lisu kwa sababu unadhani ananafasi kubwa ktk kupendekezwa, Lisu ni mpenda Democrasia na ni mtu anayewaheshimu watu wanaye muheshimu lakini akijua huna nidhamu hachelewi kukuvua nnguo hadarani
 
Sasa kama hauko Intrested ishu za CDM unakomaa nazo za nini? Au umezaliwa kuja kutoa ushauri kwa CDM?
Upinzani ni ideology, upinzani unaweza hata anzia ndani ya CCM au nje kabisa ya vyama vya siasa.
Povu lote hili ni kwa sababu Mbowe ametajwa kwenye huu uzi, au kuna shida tu nyingine za kimaisha zinakusumbua! Watu wamechangia uzi kwa staha, wewe unatukana na kufoka foka tu kama mwendawazimu.

Jifunze kujenga hoja. Huna sababu ya kujionesha kama wewe ni mtoto uliyekosa maadili kwenye makuzi yako.
 
Tundu lisu hana charisma ya kuongoza taasisi kama chama. Lisu ni individualist (selfish) anayejiangalia yeye binafsi kabla ya mtu mwingine yeyote, hawezi kuongoza chama. Kama mnataka chama kife basi mpeni lisu huo uongozi.
Wewe wasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…