Freeman Mbowe ni zaidi ya Dikteta

Freeman Mbowe ni zaidi ya Dikteta

daza steven

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
359
Reaction score
358
Yaani ukitofautiana kidogo tu na Mbowe uje nje. Haya yametokea baada ya kuwaengua wabunge wote wa CUF na James Mbatia katika baraza la mawaziri vivuli bungeni yeye kama mnadhimu mkuu wa kambi rasimi ya upinzani bungeni. Hili limekuja kutokana na kutofautiana kisiasa katika vyama hivi, wakati wote ni wapinzani na ni wabunge na ni watanzania.

Tofauti kabisa na Dr. Magufuli katika chama chake, yeye ni tofauti hata watu waliokuwa wanampinga na wanamtukana mitusi amewaweka kumsaidia hili kujenga nchi sasa huyu dicteta Freeman kama angechukua nchi na tabia yeke ya visasi siingekuwa balaa na wapinzani wake wangetamani dunia ipasuke waingie, huyu jamaa licha ya kuwa mwenyekiti wa maisha pia ni mkabila.

Zito alipishana nae kisiasa alifukuzwa kama mwizi katika chama na mchango wake wote ulisaaulika kabisa, Kitila Mkumbo walipishana naye baadaye alikimbilia CCM kwa usalama wake na sasa anajenga nchi. Fredrick Sumaye alitofautiana na Mboye yeye yaliyomkuta kila mtu aliona yaani Mh. Sumaye macho yalimtoka kama fundi saa. Kuna mtu alikuwa anaitwa Chacha Wangwe huyu alitofautiana na dicteta Mboe baadae aliuwawa katika kifo cha kutatanisha.

Tunamshukuru Mungu kwa kulipenda taifa hili la Tanzania kwa kuendelea kuiruhusu CCM itawale hadi hapo kitakapotokea chama ambacho mwenyekiti wake si mwenyekiti wa maisha kama Freeman Mbowe, kwani ni hatari kwa taifa kuwa na mwenyekiti anaemiliki chama yaani chama chake hatari sana. Nikweli watu wengi wanaupenda upinzani lakini hawajapata kiongozi mzuri wa kuwafikisha watakako kufika.

Ikumbukwe kuwa sababu kubwa ya kuletwa na kulazimiswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi ni kubadilishana vijiti katika uongozi yaani democrasia. Sasa angalia kwa dicteta Freemani Mboe yeye sasa anakariabia miaka 30 sasa katika kiti. Je, ipi maana ya mfumo wa vyama vingi ambapo yeye amekuja kuleta demaocrasia wakati ni dicteta hata Nkuruzinza amejirekebisha. Na ukitaka kuona balaa jifanye unautaka uwenyekiti wa Chadema ndiyo utauona mziki wake utaitwa majina yote mabaya hili upigwe na utaweza kuijua vizuri Redbregedia Nyekundu.

Mshaurini jamani huyo jamaa abadilike kutofautiana kisiasa si uadui awarudishe wabunge wa CUF na Mbatia hili kujenga upinzani imara, huo utakuwa ukomavu wa kisiasa katika kujenga upinzani imara na Ukawa kuwa imara hili wachukue siku moja.
 
Kwa akili zako fupi, unajiona umetoa point ?!. Elimu ya mashaka na propaganda uliyomezeshwa ni mzigo kwako .

Udhaifu unaouona ktk vyama vya upinzani , ni mkakati maalumu uliotengenezwa na watawala . Katiba yetu mama ni mbovu . Hivyo katiba ya vyama haziwezi kuwa nzuri. Kwa sababu katiba ya nchi imeacha mwanya huo makusudi.

Vyama vyote ikiwemo Ccm havina utaratibu mzuri wa kupata viongozi. Na kama unabisha jaribu kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti ccm uone.

Odhis *
 
Lakini kwa kutumia busara-"Prudence" Mh. Mbowe angewaacha wamalizie muda wao wa uwaziri kivuri. Angejua kwamba baada tu ya kumaliza bajeti june 2020 ni kama bunge linavunjwa. Kwanini sasa amekosa subira kwa mambo madogo kama haya.

Kwanza haitakiwi kuonyesha hasira hata kama Mbowe ametofautiana nao hawa Mbatia kwa kwenda kwao ikulu juzi. Mbowe mbona yeye elienda Mwanza siku ile akaonana na rais na akapewa nafasi azungumze na wananchi na wenzake wote wapinzani hawakwenda.

Sasa hao aliowachagua watafanya kazi kwa miezi mingapi? labda 3. Uongozi unahitaji hekima sana na subira.
 
Mtoa mada acha kuvuta bangi
Hapana sio kuvuta bangi ana point. Mh. Mbowe anasema kwa mfano eti CUF ilishakuwa na migogoro sasa mbona hizo tofauti za CUF ni za zamani sana labda huyo wa CUF ametolewa kafara tu kusudio ilikuwa ni mbatia tu.
 
Kuna ujinga wa kudai chacha aliuawa na mbowe kwanini kama ushahidi upo polisi wameendelea kumwacha huyo muuaji uraiani hili suala ni kuipaka matope polisi,na aibu kwenu nyie mnao lipwa hizo B7, suala la kubadilisha uongozi wa cdm ni la wana cdm wenyewe juzi kulikuwa na uchaguzi lkn mbowe aliibuka mshindi ww ulitaka achaguliwe juma baada ya uchaguzi dau lake lipande na ikitokea aunge mkono juhudi,pata picha mwenyekiti wa chama kama cdm akiunga mkono juhudi.
 
Hapana sio kuvuta bangi ana point. Mh. Mbowe anasema kwa mfano eti CUF ilishakuwa na migogoro sasa mbona hizo tofauti za CUF ni za zamani sana labda huyo wa CUF ametolewa kafara tu kusudio ilikuwa ni mbatia tu.
Mbowe kasemea wapi? hebu weka hiyo link hapa tuione.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo hapo unamtukana kwa kile alichokiandika na huku mwishoni unamsupport kuwa vyama vyote..... hebu rudia ulicho malizia hpo mwishoni odhis, ulikuwa huna haja ta kumtolea matusi kma unajua ttzo lililopo kwenye vyama...
Kwa akili zako fupi, unajiona umetoa point ?!. Elimu ya mashaka na propaganda uliyomezeshwa ni mzigo kwako .

Udhaifu unaouona ktk vyama vya upinzani , ni mkakati maalumu uliotengenezwa na watawala . Katiba yetu mama ni mbovu . Hivyo katiba ya vyama haziwezi kuwa nzuri. Kwa sababu katiba ya nchi imeacha mwanya huo makusudi.

Vyama vyote ikiwemo Ccm havina utaratibu mzuri wa kupata viongozi. Na kama unabisha jaribu kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti ccm uone.

Odhis *

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi anapaswa kuwa na subra sasa hao wamekosea nini mpaka wafurushwe katika kipindi hiki kifupi ambacho kingeweza kuvumilika?
Kwani utake utake mazungumzo na mtu halafu umpangie huyo mtu jinsi ya kufanya hayo mazungumzo kwa jinsi unavyotaka wewe ?
 
Lakini kwa kutumia busara-"Prudence" Mh. Mbowe angewaacha wamalizie muda wao wa uwaziri kivuri. Angejua kwamba baada tu ya kumaliza bajeti june 2020 ni kama bunge linavunjwa. Kwanini sasa amekosa subira kwa mambo madogo kama haya.

Kwanza haitakiwi kuonyesha hasira hata kama Mbowe ametofautiana nao hawa Mbatia kwa kwenda kwao ikulu juzi. Mbowe mbona yeye elienda Mwanza siku ile akaonana na rais na akapewa nafasi azungumze na wananchi na wenzake wote wapinzani hawakwenda.

Sasa hao aliowachagua watafanya kazi kwa miezi mingapi? labda 3. Uongozi unahitaji hekima sana na subira.
Ni vigumu kujadiliana na watu wa aina ya wafuasi wa Mbowe. Uchaguzi wa 2015 Mbowe mwenyewe alijua hawawezi kushinda ila alikuwa akitengeneza pesa. Ajabu wafuasi walielewa watashinda tu! Wanamuona kama mtu mwenye maono, lakini ukweli ni kwamba ni mtu asiyekuwa na ABC za dunia ya siasa. Kuna wakati niliwahi kuandika juu ya mazoea. Kazi unayoanza utotoni au chakula unachokula tangu utotoni ni vigumu ukubwani ukiache.

Mbowe tangu ujanani na hadi uzeeni aliendesha Casino. Ndani tulishuhudia kila aina ya uchafu na vituko. Leo hii anawezaje kuendesha chama kwa misingi ya demokrasia? Ndani ya Casino alilindwa na baunsa, siyo sheria! Unadhani ataheshimu mtu ambaye anampinga. Siamini kama anaelewa anakoelekea na huenda ukimuuliza atasema anajenga chama.
 
Kwa akili zako fupi, unajiona umetoa point ?!. Elimu ya mashaka na propaganda uliyomezeshwa ni mzigo kwako .

Udhaifu unaouona ktk vyama vya upinzani , ni mkakati maalumu uliotengenezwa na watawala . Katiba yetu mama ni mbovu . Hivyo katiba ya vyama haziwezi kuwa nzuri. Kwa sababu katiba ya nchi imeacha mwanya huo makusudi.

Vyama vyote ikiwemo Ccm havina utaratibu mzuri wa kupata viongozi. Na kama unabisha jaribu kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti ccm uone.

Odhis *
Wewe unyumbu uko damuni hutakaa uzinduke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kwa kutumia busara-"Prudence" Mh. Mbowe angewaacha wamalizie muda wao wa uwaziri kivuri. Angejua kwamba baada tu ya kumaliza bajeti june 2020 ni kama bunge linavunjwa. Kwanini sasa amekosa subira kwa mambo madogo kama haya.

Kwanza haitakiwi kuonyesha hasira hata kama Mbowe ametofautiana nao hawa Mbatia kwa kwenda kwao ikulu juzi. Mbowe mbona yeye elienda Mwanza siku ile akaonana na rais na akapewa nafasi azungumze na wananchi na wenzake wote wapinzani hawakwenda.

Sasa hao aliowachagua watafanya kazi kwa miezi mingapi? labda 3. Uongozi unahitaji hekima sana na subira.
Kukosa subira ndiyo sifa ya madikteta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie binafsi bado najiuliza alichofanyiwa Benard Membe ni Udikteta ama ni Demokrasia kwenye vyama vya siasa? Kubadilisha Baraza kivuri kama ni Udikteta, basi hata kuondolewa kwa akina Makamba, Nape na Mwigulu ni Udikteta pia.
Nini maoni yako mtoa mada!

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamaanisha Chadema ni madikteta kama ccm?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom