Huwa najiuliza hivi huyu jamaa Freeman Mbowe tangia akiwa kijana anahubiri demokrasia kwenye hii nchi mpaka amezeeka haoni vizuri lakini yeye mwenyewe ndani ya chama chake ni diktekta wa uenyekiti tangia akalie hicho kiti ni miaka ya mtu mzima Sasa lakini jamaa hataki kupisha mtu mwingine akalie hicho kiti.
Huyu jamaa tunakuwa na wasiwasi nae asije chukua nchi halafu yakawa mambo ya Mugabe kujimilikisha Mali na kukataa kutoka madarakani, Mbowe hataki kuachia uenyekiti sababu anajua pesa za ruzuku ya chama ni tamu nawaambieni watanzania mkitaka CCM itoke madarakani anzeni na diktekta Mbowe, huyu jamaa hafai kuwa mwenyekiti hata kama chama kaanzisha baba yake, kiufupi Mbowe kazeeka na ni tapeli tu.