Pre GE2025 Freeman Mbowe: Nitatoa uamuzi wa kugombea Uenyekiti siku ya Jumamosi saa 5 asubuhi

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Nitatoa uamuzi wa kugombea Uenyekiti siku ya Jumamosi saa 5 asubuhi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba Mwenyekiti wa Chadema anayemaliza muda Wake, atazungumza na Dunia kupitia Waandishi wa Habari muda wowote kuanzia sasa.

Usiondoke JF kwa Taarifa zaidi
nipo hapa kwenye balcony, plz tuonane kamanda 🐒
 
Usiondoke JF kwa Taarifa zaidi
18 December 2024
Mamia Wafurika kitongoji cha Mikocheni Jijini Dar, mitaa ya Nyumbani kwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa

View: https://m.youtube.com/watch?v=2ENVr1NAuJg
Wajumbe wa mabaraza, Wanachama, wapenzi, mashabiki kutoka mikoa yote wanena mazito leo Mikocheni jijini Dar es Salaam nyumbani kwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anayemaliza muda wake mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe ..
 
Baada ya miaka mingi kupita, leo Wacha na Mimi nichangie kidogo kuhusu yanayoendelea Chadema.

Ukitaka mabadiliko lazima uoneshe Nia ya kubadilika na si kuendelea kufanya mambo Yale yale. Wananchi wengi wamekatishwa tamaa na namna upinzani unavyokabiliana na serikali dhalimu ya CCM.

Kuna matukio mengi yamefanyika kutoka mwaka 2015 Mpaka leo ambayo yamerudisha nyuma Ari na morali ya wananchi kushiriki katika demokrasia na kwa kiasi kikubwa wamekata tamaa.

Mtu mmoja ambaye walau ameonesha kuwa na msimamo wa kukabiliana na hali tangu kipindi hicho kwa mtazamo wangu ni TAL. Huyu mtu hakika anaonesha wazi wazi ana Nia thabiti ya kuleta mabadiliko kwani Hana hata chembe ya hofu kwa Yale anayoamini yanaweza kuleta haki.

Nilidhani CDM wameliona hili kama sie watu ambao tupo nje ya CDM vile ambavyo tumeweza kuona. Nashangaa ndani ya CDM hawataki mabadiliko ilhali wanataka mabadiliko ndani ya nchi, hapa tunashangazwa wengi.

Haileti picha nzuri kuona TAL anapingwa wazi wazi na kuanza kuonekana kama ni mtu Baki wakati ameweka rehani uhai wake kusaidia vugu vugu la mabadiliko kupitia CDM.

Wengi tungependa ashike nafasi ya kuu pale CDM tuone namna Gani ataleta mbinu mpya za kukabiliana na CCM.

Mbowe amepata muda wa kutosha na kwa kweli mbinu zake hazijatosha kabisa kukabiliana na CCM ambao wanatumia Dola kuendelea kubaki madarakani.

CDM msichezee fursa hii tena, manalo jukumu la kuonesha Jamii kuwa mnaweza kubadilika kulingana na mazingira na kusaidia Jamii ya Tanzania ambayo imebaki bila msaada kwa ukoloni wa CCM.

Ahsante
 
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba Mwenyekiti wa Chadema anayemaliza muda Wake, atazungumza na Dunia kupitia Waandishi wa Habari muda wowote kuanzia sasa.

Usiondoke JF kwa Taarifa zaidi
Tutegemee atatangaza kutochukua fomu busara imwongoze kufanya maamuzi magumu
 
Back
Top Bottom