Baada ya miaka mingi kupita, leo Wacha na Mimi nichangie kidogo kuhusu yanayoendelea Chadema.
Ukitaka mabadiliko lazima uoneshe Nia ya kubadilika na si kuendelea kufanya mambo Yale yale. Wananchi wengi wamekatishwa tamaa na namna upinzani unavyokabiliana na serikali dhalimu ya CCM.
Kuna matukio mengi yamefanyika kutoka mwaka 2015 Mpaka leo ambayo yamerudisha nyuma Ari na morali ya wananchi kushiriki katika demokrasia na kwa kiasi kikubwa wamekata tamaa.
Mtu mmoja ambaye walau ameonesha kuwa na msimamo wa kukabiliana na hali tangu kipindi hicho kwa mtazamo wangu ni TAL. Huyu mtu hakika anaonesha wazi wazi ana Nia thabiti ya kuleta mabadiliko kwani Hana hata chembe ya hofu kwa Yale anayoamini yanaweza kuleta haki.
Nilidhani CDM wameliona hili kama sie watu ambao tupo nje ya CDM vile ambavyo tumeweza kuona. Nashangaa ndani ya CDM hawataki mabadiliko ilhali wanataka mabadiliko ndani ya nchi, hapa tunashangazwa wengi.
Haileti picha nzuri kuona TAL anapingwa wazi wazi na kuanza kuonekana kama ni mtu Baki wakati ameweka rehani uhai wake kusaidia vugu vugu la mabadiliko kupitia CDM.
Wengi tungependa ashike nafasi ya kuu pale CDM tuone namna Gani ataleta mbinu mpya za kukabiliana na CCM.
Mbowe amepata muda wa kutosha na kwa kweli mbinu zake hazijatosha kabisa kukabiliana na CCM ambao wanatumia Dola kuendelea kubaki madarakani.
CDM msichezee fursa hii tena, manalo jukumu la kuonesha Jamii kuwa mnaweza kubadilika kulingana na mazingira na kusaidia Jamii ya Tanzania ambayo imebaki bila msaada kwa ukoloni wa CCM.
Ahsante