Hasa kwa Lissu. Lissu amekuwa anapulizia moto wakati Mbowe hajasema chochote bali kusisitiza umoja katika chama. Nadhani imani ya Lissu ni kuwa baada ya uchaguzi Mbowe atasamehe na kusahau kila kitu na kuungana nae katika kutibu majeraha yaliyotokea. Sidhani kama itakuwa hivyo. Nadhani yafuatayo yatafuata:
1. Mbowe atatangaza kutogombea halafu atakaa pembeni.
2. Mnyika na makamu wake bara wataachia ngazi ama Lissu atateua watu wengine wa kuchukua nafasi zao.
3. Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu nao wataachia ngazi.
4. Uongozi mpya utaweka wazi ubadhirifu na ufisadi mkubwa unaofanywa na Mbowe na sekretariat yake ( tayari trial ballons za kuhujumiwa kwa laptop zimerushwa).
5. Timu mpya ya wapiganaji yenye uwezo wa kupambana na CCM pamoja na serikali yake itaundwa.
6.Mazungumzo ya maridhiano yatazikwa rasmi na watanzania wataingia barabarani kwa wingi kushinikiza Katibu Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na kutimuliwa kwa wakina Halima.
Yetu macho.
Amandla...
..kwenye Power Breakfast Tundu Lissu alisema mchango wa Freeman Mbowe katika kupigania mageuzi na demokrasia unapaswa kuandikiwa vitabu.
..makamu wawili wanachaguliwa na mkutano mkuu, na Katibu Mkuu nadhani anapendekezwa na Mwenyekiti.
..John Mnyika ameonekana kutokuwa na furaha katika chama tangu tukio la kumleta Lowassa. Sijui tatizo lake ni nini haswa.