Pre GE2025 Freeman Mbowe nyamaza au Ingia CCM 100% maana wewe ni mtoa taarifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Do these people know the very situation on the ground or are just eaten from regime beneficiary?
 
Mkuu unamshtumu na kumsakama Mbowe kwenye andiko lako kama vile Mbowe ndiye Mkuu wa Kanisa la KKKT na ndiye mnufaika wa huo mchango.

Mbowe hajamlazimisha wa kumshurutisha Samia kuchangia, Samia kaamua kuchangia kiasi hiko kwa hiyari yake! Ulitaka Mbowe akatae, ili iweje?!

Samahani Mkuu, kwa maoni yangu I thought your awareness of the law was meant to clear the bush in your head but instead it seems it cultivated the bush in your head so densely and deepy!
 
"Church" is meant to represent religion.

The more appropriate term is "Separation of Religion and State".
Nadharia yenyewe ikoje hasa. Hebu ijazie nyama tuone huo utenganisho wa dini na dola ukoje...

Yaani tuelezee kuwa kunakuwa na kiashiria gani kuonesha kwamba hapa dini na Dola vimechangamana...
 

Kabla hata ya Samia, Mbowe anajitengenezea matatizo mengi kuchanganya siasa na dini.

Tayari kuna maneno mengi ya kidini katika siasa, majungu na maneno ya msingi, habari za Mfumokristo kuongoza nchi zinasemwa sana. Habari za kampeni za kisiasa kufanyika makanisani zinasemwa sana. Habari za CHADEMA kuwa ni chama cha Wakristo zinasemwa sana.Mbowe kujiweka kimbelembele kanisani tu ni tatizo. Kunachochea habari hizi.

Caesar's wife should be above suspicion. Mbowe anajipeleka kwenye religious political controversies na suspicion bila sababu.

Mbowe kama kiongozi wa kisiasa aliyejiweka kimbelembele kanisani, ni mnufaika wa huu mchango. Watu wanamuona big shot kamleta rais kuchangia kanisa, anatumia umaarufu huo kisiasa. Unafikiri akijinadi kafanikisha ujenzi wa kanisa mpaka kamleta rais, watu wamkubali kisiasa, watu hawatakuwa influenced?

Hivi huoni wanasiasa wanavyotumia dini kujikosha na kufanya kampeni za umaarufu hapa? Wote wawili Mbowe na Samia?

Hivi huoni Samia anavyojitengenezea mazingira ya kuwa na influence KKKT, kesho wakiwa na migogoro waende kwake awachagulie maaskofu chawa watakaotuambia "Samia chaguo la Mungu" kwa sababu za kupewa asali ya kutoka Ikuku?

Mbowe kamualika Samia. Samia hajajipeleka tu kwa kina Mbowe. Kuna makanisa mangapi yanahitaji ujenzi Tanzania? Kwa nini Samia kaenda kujenga kanisa la kwa Mbowe?

Kama hujui kusoma, hata picha huoni hapo?

Kanuni za rule of law and good governance zinataka nchi secular iendeshwe in a secular way, kusiwe na hata muonekano wa watu fulani au dini fulani kupendelewa. Sasa hivi serikali imejiingiza kujenga makanisa. Hii si kazi ya serikali. Kila mtu anayetaka kanisa lake lijengwe kwa mchango wa Ikulu wa Sh 150 milioni akijipanga apate mgao huo, rais hataweza kututimizia wote.

Hapa kuna muonekano wa Mbowe kupendelewa, kwa nini? Mbowe kahongwa ili awe mpole kwenye siasa.

Nyerere amekuwa rais kwa miaka 24. Alikuwa Mkatoliki kindakindaki.Tulikuwa tunamuona St. Peters Oysterbay kila siku asubuhi.Hakuwahi kuchangia ujenzi wa kanisa wala msikiti kwa namna hii. Kwa nini?

Alijua kanuni za Separation of Religion and State. Alijua hiki jambo ni scandal.

Mbowe hajui? Samia hajui?

Kama hawajui, hawafai kuwa viongozi, kwa sababu hawajui misingi muhimu ya uongozi katika a secular state.

Ama wanajua wanadharau tu?

Kama wanajua, ila wanadharau tu, hawafai kuwa viongozi katika a secular state. Kwa sababu wanadharau misingi ya Separation of Religion and State.
 
Aliyekutuma amekupoteza! Huna maana na ulisemalo ni uchawa wako huna mwelekeo!.
 
Nadharia yenyewe ikoje hasa. Hebu ijazie nyama tuone huo utenganisho wa dini na dola ukoje...

Yaani tuelezee kuwa kunakuwa na kiashiria gani kuonesha kwamba hapa dini na Dola vimechangamana...
Mkuu mbona nimekuwekea link pale post #108 inaeleza vizuri kutoka historia ya hii hoja?

Kifupi ninkwamba, dini na uongozi wa nchi vikichanganywa vinaleta maafa.

Ndiyo mwanzo wa ujinga wa nchi kujiingiza kwenye siasa za dini.

Ndiyo mwanzo wa Samia kuchangishwa mpaka akawa naninfkuence kwenye dini, serikali ikateka dini na kutumia dinibkwenye siasa. Ndiyo mwanzo wa Samia kuongeza wateule wake kutoka wakuu wa mikoa na mabalozi akaenda kuteua mpaka maaskofu kisiri na tukahubiriwa kuwa "Samia ni Chaguo la Mungu" makanisani, kutika kwa maaskofu chawa wa Samia.

Kwa upande mwingine, dini nayo inaweza kuteka serikali, tukaongozwa kidini, wenye dini na tusio na dini.

Ndiyo mwanzo wa maaskofu kumshauri rais afanye maamuzi si kwa misingi ya kimantiki, bali kwa misingi ya kidini.

Ndiyo mwanzo wa dini nyingi tofauti kuona mbona rais kafanya mchango kanisani, huyu rais kwani ni wa Wakristo tu, mbona anatubagua wengine?

Ndiyo mwanzo wa wasio na dini, au wenye dini tofauti kuona mbona pesa za kodi yetu zinatumika kwenye mambo ya dini kanisani, wakati sisi hatutaki hilo?

Kwa hiyo, kitu bora kabisa ni serikali kutojiingiza katika mambo ya dini kwa namna hii. Na kuepuka maneno yote hayo.

Nyerere alioewa tuhuma kwamba anapendelea mawaziri Wakatoliki. Wako wengi.Akajibu kuwa serikali yake hata haijui madhehebu/ dini za watu, hairekodi, kitu anachoweza kujua ni wanakula kiapo kwa kutumia mshahafu gani, na hata hilo haliwezi kumfanya ajue nani ni Mkatoliki.

Nyerere alielewa vizuri sana Separation of Religion and State, mpaka kwenye sensa alikataa kuuliza swali la dini. Akisema kazi ya kuhesabu watu kwa dini serikali imeziachia taasisi za kidini.

Alijua Separation of Religion and State ni nini.

Sasa tumetokaje kwa Nyerere aliyekataa serikali yake hata kuuliza watu dini zao katika sensa, kwa kuzingatia Separation of Religion and State, mpaka kwa Samia anayetoa shilingi milioni 150 kujenga kanisa?

Hawa viongozi wanavyosema wanamuenzi Nyerete wanamaanisha hilo kweli? Walimueleea Nyerere na sasa wanafanya makusudi kubomoa misingi mizuri aliyotuachia katika Separation of Religion and State? Au hawakumuelewa tangu mwanzo?
 
- Hivi ni wakati gani kiongozi wa kisiasa anatakiwa kutenganisha dini na siasa, ikiwa nae ni muumini wa dini/dhehebu fulani?

- Kwanini ionekane dhambi kwa kiongozi wa kisiasa kushiriki shughuli za kanisani kwake ikiwa anahusika? kujitenga ndio sheria? kwamba ni either uifuate siasa uachane na dini? kwamba sasa tunataka siasa zetu ziongozwe na wapagani?

●Suala la Nyerere kutojihusisha na michango mbalimbali, kwani aliwahi kutakiwa kufanya hivyo akakataa? au alikubali akafanya kwa namna ipi tofauti? au ni huu utaratibu wa sasa ndio haukuwepo wakati ule?

- "Siasa kuingia kanisani" huoni kama huu ni mtazamo wako tu hasa ulipozungumzia KKKT na urafiki wao na Samia, kwani kuna dhehebu lingine limewahi kutafuta mchango kwa Samia likanyimwa ili tumhukumu vizuri Samia na nia yake?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Tayari naambiwa na rafiki yangu mmoja Mzanzibari kuwa misikitini Zanzibar watu wamemsema sana Samia kwa kuchangia shilingi milioni 150 kujenga kanisa.

Haya maneno kajitakia mwenyewe, yasingekuwapo kama angezingatia "Separation of Religion and State"
 
Siasa haina rafiki wa kudumu.. Mbowe hajawah kuwa mpinzani na ana kadi ya ccm..
Wengi walio ktk umri wa Mbowe walikuwa wana CCM. Kuwa na kadi ya CCM haina maana ya kuwa mwanachama wa CCM. Kadi ya CCM kwa sasa ni kumbukumbu tu ya historia ya kisiasa.
 
Tayari naambiwa na rafiki yangu mmoja Mzanzibari kuwa misikitini Zanzibar watu wamemsema sana Samia kwa kuchangia shilingi milioni 150 kujenga kanisa.

Haya maneno kajitakia mwenyewe, yasingekuwapo kama angezingatia "Separation of Religion and State"
Hao watu wamemsema kwasababu hajazingatia hiyo "separation of religion and state" au wamemsema simply because amechangia ujenzi wa kanisa? vipi kama angechangia ujenzi wa msikiti, wangemsema pia?!

Hapa nakuona kama umeamua kujiingiza kwenye vichwa vya usiojua dhamira zao, kisha ukalazimisha fikra zako ziwe zao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

Rais wa 35 wa Marekani, John Fitzgerald Kennedy, alivyokuwa Seneta wa Massassuchets, akigombea urais wa Marekani, alipata tabu sana kusakamwa na watu waliokuwa na hofu kwamba atakuja kuendesha nchi kidini.

Matatizo hayo yalitokana nanukweli kwamba, Marekani ikikuwa haijawahi kupata rais Mkatoliki kabla yake, na Wamarekanibwengi walikuwa na hofu kwamba, kwa kuwa Papa wa Wakatoliki ana nguvu sana, Papa anaweza kutumia nguvu zake kanisani kumpangia rais wa Marekani nini cha kufanya.

Seneta Kennedy akaumizwa sana na kusakamwa huko, ikabidi aitishe mkutano nankutoa hotuba ya kuelezea msimamo wake kuhusu suala zima la kutenganisha dini na siasa.

Hii hituba huwa narudia sana kuisikiliza ninapokutana na hoja hii ya kutenganisha dini na uongozi wa nchi.

Hapa ninaweka kipande kidogo tu, ukiweza kuisikiliza hituba yote isikikize.

Kujibu maswali yako.

Wakati gani kiongozi anatakiwa kutenganisha dini na siasa ikiwa naye ni muumini?

Wakati wa maamuzi ya kazi hatakiwi kutumia dini. Mfano, kama kuna mpango wa kupunguza maambukizi ya HIV unaosema serikali ifanye kampeni ya kusambaza condom kuzuia maambukizi, na rais ni Mkatoliki, na Ukatoliki unakataza matumizi ya condom, rais hatakiwi kukataa serikali kufanya kampeni ya watu kutumia condom kwa sababu ya Ukatoliki wake. Hii ni public policy, anatakiwa kwenda na sera za serikali.

Ikiwa yeye mwenyewe kwenye maisha yaje binafsi anaona asitumie condom, kwa sababu yeye ni Mkatoliki, hapo anaruhusiwa. Kwa sababu ni maisha yake binafsi.

Kwa nini ni vibaya kiongozi wa siasa kushiriki shughuki za dini? Kwanza kiongizi anaweza kushiriki, Nyetere alienda kanisani kila siku. Kama Julius K Nyerere. Lakini hakuenda kama rais. Piki, kushiriki kama rais kunajenga mgongano wa siasa kuingizwa kanisani. Tumeona Magufukibalikuwa anaingia kanisani nankuchujua mic na kuhubiri, sasa rais anaweza kuteka kanisa akaweka siasa kanisani. Hilo ni jambo baya sana linaloweza kuketa mgawanyiko wa kidini katika siasa.

Nyerere kama aliombwa akakataa au hakuombwa hatuwezi kujua kwa sababu hatukuwa naye muda wote, kitu muhimu ni kwamba hakuchangia.

Habari za Siasa kuingia kanisani na Separationnif Religion and State ni suala refu sana, limeanza zamani sana, limezungumzwa karne nankarne, limehutubiwa na Seneta Kennedy kabla mimi sijazaliwa, kwa hivyi, si kitu ambacho nibwazo langu tu.

Tatizo Watanzania wengi si wafuatikiaji wa Historia, hawajasoma haya mambo, nikiyaongelea leo mimi, wengine ndiyo kwanza wanayasikia, wakati ukisoma historia unakuta haya ni masomo ambayo wenzetu wamejifunza miaka 500 iliyopita.

Nimeelezea mengi hapo juu. Video ya hotuba ya Kennedy pia itasaidia kujibu zaidi.

Tatizo, lugha ya Kennedy wangapi wanaielewa?

Kuna gap kubwa sana kuongea na mtu kuhusu "Separation of Religion and State" ikiwa hata Kiingereza hakielewi.


View: https://youtu.be/LAvHHTt2czU?si=4iJczUsT7rlxRNGV
 
Mbowe ni msanii wa siasa za Chedema jamaa anapiga mpunga tu, ndio maana ni ngumu sana kuachia hichi kiti cha Uenyekiti.
 
Mkuu,

Watanzania wengi hata hiyo "Separation of Religion and State" hawaijui. Ndiyo maana hata hapa napata shida kuielezea.

Wengi inakuwa kama ndiyo wanaisikia mara ya kwanza. This is such a basic tenet pf a secular state.

Hao Wazanzibari wengi wanapinga kwa sababu Samia kachangia kanisa, angechangia msikiti wasingepinga wao, Wakristo wangelalamika Samia mdini, kachangia msikiti hajachangia kanisa.

Which is part of my point.

Serikali ikijiingiza kuchangia kujenga nyumba za dini, inaleta manenomaneno mengi ya manung'uniko.

Ikichangia kanisa, waislamu wanalalamika.

Ikichangia msikiti, wakristo wanalalamika.

Ikichangia KKKT, hata RC watalalamika.

Ikichangia dini yoyote, atheists tutalalamika.

Kwa hivyo, wenye busara waliona hili tatizo, wakasema kuwe na "Separation of Religion and State". Serikali isichangie kujenga nyumba yoyote ya dini.

Isipochangia, hakuna msingi wa mtu yeyote kulalamika.

Nyerere msomi wa falsafa alilijua hili akaliepuka. Ndiyo maana huwezi kusikia Nyerere katumia hela za serikali kachangia kujenga nyumba ya ibada kwa namna hii.
 
Aliyechangia hizo milioni 150 ni Samia kiongozi wa serikali na nchi au Samia kama raia binafsi?

Na hizo hela zimetoka wapi? Hazina au akaunti binafsi ya Samia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…