Ila Samia atatumiaje hela za serikali/ wananchi kutoa msaada kwenye kanisa [la Mbowe]?
Mbowe naye atakubalije kupokea msaada wa kifedha toka kwa Rais wa nchi kwenda kwenye kanisa [lake]?
This is very bothersome on many levels!
Samia hajui tofauti kati ya serikali na dini?
Mbowe naye hajui tofauti kati ya dini na serikali?
Wote hawa wawili hawajui kuwa Tanzania/ serikali ya Tanzania haina dini?
Mbowe ni mwenyekiti wa chama chenye lengo la kuja kuongoza nchi na hajui kuwa serikali ya nchi haina dini?
Au wote wawili wanajua ila hawajali chochote?
Nakuelewa sana unavyosema hayo yote, na mimi ndiyo maswali yangu hayo.
Ila, nakupa possible take from Samia's rationale. Kibongobongo.
What is Sh 150 million kwenye jambo kubwa kama kujenga umoja wa kitaifa? Kwenye kuponya vidonda vya awamu ya tano, that is a bargain price.
Tena kwa kupitia kitu kizuri kitakachojenga watu kiroho kama kanisa?
I mean it's not like Samia amechangia nyumba ya kuishi Mbowe, hili ni kanisa ambalo watasali Watanzania.
After all, Mbowe alivunjiwa heshima na alifungwa muda mrefu for trumped up charges. Hapa serikali ni kama tunamlipa tu towards giving to a charity of his choice, KKKT. Mbowe hawezi kuishitaki serikali kudai fidia, tunamlipa fidia kwa njia nyingine tu.
Na hapohapo wananchi wanaona Samia mtu poa, anatoa sadaka mpaka kanisani kwa Mbowe.
Waislamu wanafundishwa kuishi vizuri na Wakristo.
CCM wanafundishwa kuishi vizuri na CHADEMA, wakileta ugomvi wanaambiwa nyie mnagombana nini mbona wenyeviti wenu damudamu mpaka Samia kachangia kujenga kanisa la kwa Mbowe.
Mbowe anaonekana big shot kafanikisha ujenzi wa kanisa kwa kumchangisha mpaka rais.
Samia anaonekana mtu wa maana sana, hana nongwa na mtu.
Everybody wins.
Na wewe kama una kanisa lako unajenga, mtafute Samia akuchangie kwa urefu wa kamba yako kama alivyosema mwenyewe.
Hapo vipi kibongobongo?