Pre GE2025 Freeman Mbowe nyamaza au Ingia CCM 100% maana wewe ni mtoa taarifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu kwanza, nakuheshimu kwa hoja na michango yako mingi humuni jukwaani.

Kwenye hoja hii na tofautiana nawe uliposhindwa kutofautisha kati ya Samia na Serikali ya Samia.

Itapendeza ukiweka hizo link za hoja zako za zamani kuliko maneno mengi! Ziweke hapa kama anavyofanya ndugu Pascal Mayalla!

Mkuu Mbowe angesema serikali imetoa mchango, hoja yako ingekuwa na nguvu! Na ungekuwa right jinsi ya mchango wako.

Naomba usikilize upya sauti ya mbowe au usome vizuri nukuu ya Mbowe kwenye Gazeti la mwananchi; Mbowe kasema mchango umetoka kwa Samia na familia yake!

Mkuu usichanganye mada!
 

Umekubalinkwamba hoja zako za hypocrisy zilikuwa baseless na za jazba tu?

I anticipated your lot in my reply to Nyani Ngabu posts #136 and #138

Samia na familia yake wana biashara gani ya kugawa sh milioni 150 willy nilly hivi? Wamei declare kwenye fomu za maadili ya uongozi?

Unahakikishaje mchango umetoka kwa Samia na familia yake na si mifuko ya serikalini?

Mchango huu unatoa mu9nekano gani? Justice must not only be done, it must also appear to be done. Unaeleea maana yake?

Rais na Mbowe hawatakiwi tu kuepuka rushwa, wanatakiwa pia kuepuka hata muonekano wa rushwa. Unaelewa maana yake?

Wanaompinga Mbowe wakisema Mbowe kalishwa asali na Samia ili anyamaze kwenye siasa, Mbowe atakataa vipi?

Kwani kitu kuwa kibaya ni lazima kiwe na sheria ya kukikataza? Mbowe huyuhuyu na chama chake si kati ya watu wanaosema rais ana mamlaka makubwa sana yapunguzwe? Sasa leo rais akitumia mamlaka yake vibaya kuchangia makanisani kinyume na misingi ya nchi isiyo na dini hawaoni kwamba rais ana mamlaka makubwa anayoyatumia bila breki?

Hao mawaziri wote wametenda kosa lilelile la kuchanganya dini na siasa, two wrongs do not make a right. Unaambiwa Samia kaua, kuua ni jambo baya. Unamtetea kwa kusema mbona Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu na wao wameua? Hapo hujamtetea rais wala hao mawaziri, umeonesha tu kuwa uongozi wote ni uozo uleule.

Mkuu, mimi nimeongelea concept ya Separationnof Religion and State, hapo biashara inahusikaje? Mfanyabiashara ana pesa zake binafsi, si za serikali. Mfanyabiashara hana nafasi ya uongozi serikalini, kwa nini unamuingiza hapa kwenye issue ya Separation of Religion and State?

Hivi unaeleea hata hoja inayoongeleea na mimi hapa au unarukia kiushabiki tu?

Wapi nimesema wafanyakazi wa kawaida wasio viongozi wasichanganye kazi na dini? Mbona unataka kuleta issues ambazo mimi sijazitaja popote na kuzifanya kuwa issue zangu?

Stick to my issue. Uongozi wa nchi kujiingiza kwenye dini. Sasa hapo mfanyabiashara na mfanyakazi wa kawaida asiye kiongozi anaingia vipi?

Unaweza kufuatilia mada kimantiki na kusoma kwa ufahamu? Au unawayawaya tu kiushabiki?
 
Samia ana biashara gani kutoa mshahara wake wa mwaka mzima kama sadaka kanisani?

Kuhusu links, angalia mfano mmoja huu hapa nikikemea rais Magufuli kuchangia shilingi milioni 10 kwenye ujenzi wa kanisa.

Kwa hili utaona niko consistent.

Angalia post #100 na #103 #107 na kuendelea kwenye huu uzi naweka link hapa chini. Usiniseme kwamba mimi nafiki wakati hata hujachunguza consistency yangu, utajikuta wewe ndiye mnafiki kwa kuniita mimi mnafiki.

 
June 7 2020

Kiranga wrote
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kiranga said:
Rais anatakiwa ajiondoshe kwenye muonekano wa kupendelea dini au madhehebu fulani.

Rais anatakiwa ajiondoe kwenye muonekano wa kupendelea kutumia pesa zisizojulikana chanzo chake.

Rais anatakiwa ajiondoe kwenye muonekano wa kupendelea kutumia pesa za serikali kwenye mambo ya dini.

Rais anatakiwa ajiondoe kwenye muonekano wa kupendelea kutumia pesa zilizovuka mapato yake halali yanayojulikana.

Kote humo Magufuli kaharibu.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Hapo Magufuli alikuwa kachangia shilingi milioni 10 tu kwenye ujenzi wa kanisa.

Nimesimamia hapo hapo kumsema Magufuli, nimesimamia hapo hapo kumsema Samia. Consistently.

Tuhuma zozote za unafiki dhidi yangu ni za kijinga, zimefanywa kwa jazba, bila hata uchunguzi mdogo tu kujiridhisha.
 
👍
 
Mizania

Mkuu, kuwa muungwana tu uniombe radhi kwa kuniita hypocrite kwa jambo ambalo hukulifanyia uchunguzi na ushahidi niliouweka hapa unaonesha wazi kuwa sipo huko na nimesimama na msimamo wangu thabiti kupinga marais wanaotoa pesa makanisani,kutoka utawala wa Magufuli mpaka wa Samia.

Kubali tu kuwa hapa ulikosea na ulinipaka matope kwa jazba bila kufanya uchunguzi wa kutosha.

Umetaka link, nimekuwekea.

Nitake radhi mkuu nijue hatushindani kwa ligi isiyo na heshima wala tija.
 
🙏 My honest apologies Mkuu!
 
Hahahaa.

Hii imenikumbusha watu ambao huwa wanadai kimakosa kwamba sikuwahi kumkosoa/ kumpinga Rais Magufuli alipokuwa madarakani.

Kuna siku nikaorodhesha mada karibu 10 nilizoanzisha mwenyewe [achilia mbali michango yangu kwenye mada zilizoanzishwa na wengine ambamo nilikuwa namkosoa pia] ambazo nilikuwa nampinga na/au kumkosoa.

Wengi wa hao watu ama walipotea tu au walihamisha magoli.

Nikahitimisha kuwa watu wengi wa aina hiyo huwa ni trolls tu ambao siku hizi wala siwajibu tena.

Magufuli katawala kwa miaka 6. JF humu kuna mamilioni ya posts.

Mtu anatoa wapi ujasiri wa kusema flani hajawahi kumpinga kiongozi flani kana kwamba kayapitia mabandiko yote ya huyo mtu ambaye anadaiwa kutokuwahi kumpinga huyo kiongozi flani?

Some of these people are just trolls who get a kick out of making things up!
 
Inashangaza sana mtu anahitimisha hivyo. Hilo lina onesha aina fulani ya one track mindedness iliyopo hapa.

The false dichotomies, the manufactured mutual exclusivity, kwamba, ukimsema Samia, basi wewe lazima utakuwa mfuasi wa Magufuli.

Bila kujua kwamba kuna watu wengine tunatazama kanuni, bila kujali mtu.
 
Kazi kweli kweli !!
 
So much outcry about Mr. Mbowe, what does it mean?
 
Luv this..
Truth hurts but ndio ukweli

Mbowe anazingua sana

Opposition bongo ni uongo uliotukuka
Chadema kila siku press conference tuuu na safari zisizo na kikomo kama mnakimbiza mwenge wa kutulaghai

Lissu John Heche sukumeni hili gurudumu otherwise msiendelee kuwadanganya wananchi.
Mnawapa matumaini yasiyowezekana.
 
Maneno mengi ya Wala ulojo haya....!! Hivi tunaelekea kupindi Cha uchaguzi inawezekanaje mwenyekiti na mgombea wa CCM akampa fedha mwenyekiti wa chadema ati apeleke kanisani!!. Vipi Mbowe hakufikiria Kama hiyo inamuongezea credit mgombea pinzani?, Mbowe kawaribisha wale covid 19 Kuna uhusiano gani nao? Chama kina mgogoro na covid19 mwenyekiti ana mahusiano nao?. Upuuzi mkubwa.
 
Ukipitia commenr za uzi huu utagundua kuwa raia wengi hapa TZ hawana uwezo wowote kwa kureason mijadala na matukio tena.

Yaani kwakua mtu fulani ni mwana CDM anaamini kwamba Mbowe hawezi kukosea na hapaswi kukosolewa, vivyo hivyo akiwa mwana CCM anaamini kwamba SHH hapaswi kukosolewa.


Huu uzi umenionyesha akina LUCAS MWASHAMBWA wengi sana wa upande wa CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…