Hapana. Siyo kuja "kuwajulisha", tunawahimiza muwe tayari kwa hiyo hatua inayo fuatia baada ya kura zinazo ibiwa.
Ngoja nikueleze kitu kipya (nadahani ni kipya).
CCM akiona mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa sana kwenye kupiga kura, hatathubutu hata mara moja kufanya ujinga alio zoea kuufanya.
Ukisusa na kukaa nyumbani, tayari CCM anaihesabu kura yako ya kumkubali.
Kwa hiyo mkuu 'Tindo', si angalau hata ni bora kujitokeza tu kuonyesha umoja wako na hao watakaoshiriki kupiga kura, ili kumfanya CCM anywee, kuliko kubaki tu umekaa nyumbani ukisubiri njia mbadala, ambayo hata mwanzo wake haufahamiki?