Kuna kijana aliwahi niuliza kama nina mipango ya kugombea ubunge au urais, nikamjibu hapana.
Nikamuuliza yeye ana mpango huo,akajibu ndio.
Nikamuuliza atawafanyia nini wapiga kura wake akipata huo ubunge,akanijibu kusaidia kupaza sauti juu ya matatizo waliyonayo.
Nikamuuliza tena atafanya nini atakapopata ubunge,akasema atahakikisha anawajengea wazazi wake nyumba ya maana ,ananunua gari kali na kuwapeleka watoto wake shule nzuri.
Nikamwambia kati yangu mimi na yeye nani ana nafasi kubwa sana ya kuwa mbunge na kuwasaidia wananchi,akanijibu mimi.
Sababu gani,akaniambia mimi nimejitosheleza kwa kila kitu,hivyo sitakuwa bungeni kwa ajili ya mshahara,posho na marupurupu ya ubunge,hivyo nitawawakilisha vyema wananchi.
Nilichogundua ni masikini wachache sana sana ambao hawafikirii kujinufaisha wao wenyewe binafsi na familia zao kabla ya wananchi.
Umasikini ni laana, laana ambayo inatufanya tuwe wabinafsi.
Viongozi wote wanaofisadi ni muendelezo wa laana ya umasikini katika familia,jamii na koo zao.
Tupige vita laana ya umasikini kwa nguvu sana lakini tuhakikishe vita hiyo haituletei laana nyinginezo.