Freeman Mbowe: Scotland Yard ya Uingereza ichunguze Matukio ya Utekaji na Uuaji nchini

Freeman Mbowe: Scotland Yard ya Uingereza ichunguze Matukio ya Utekaji na Uuaji nchini

Usipojifunza historia unapata laana ya kuirudia.

Uelewa wako mwisho wake ni hapo
ICJ ipo kwa sababu ipi?
Umeuliza swali la kipuuzi ndio maana nakuita bumunda, eti Scotland Yard wakikuta watuhumiwa nani wa kuwapeleka kwenye mkono wa sheria.. si swali la kipuuzi kabisa
 
Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?"
Nilikuwa nashangaa hata mimi. Mifumo yote inasapoti mambo jayo ni ngumu sana kuwaepuka watekaji
 
Sometimes wapinzani hua wanaongea vitu havimake sense.

Ni taifa gani sovereignty linaalika nchi nyingine kufanya uchunguzi kwenye nchi yake?

Scotland yard wakisema wahusika ni mtu huyu, nani anatakiwa kumuwajibisha huyo mtu? Scotland yard au mahakama za Tanzania?

Hii drama waliwahi kuiraise muda fulani ikafifia naona wameanza nayo upya

Sio kitu kibaya kuwa na tume huru ya uchunguzi. Unaweza kutumia Scotland yard au tume ya majaji ya jumuiya ya Madokla, au ya umoja wa Mataifa.
 
relax tu gentleman,
hakuna taifa lolote la kistaarabu duniani hususan kutoka ng"ambo linaweza kuthubutu au kupoteza muda au kukiuka sheria za kimataifa kuingilia mambo ya ndani ya nchi ingine,

tena kwa kuskiliza tu madai ya hisia na mihemko yanayotolewa na mtu amabae ana record ya kihalifu tena ugaidi kabisa, ambao ni tishio la kiusalama duniani kote,

lakini zaidi sana ambae anashukiwa kua ni miongoni mwa wenye mikono yenye damu za watu dhidi ya yanayoendelea ndani chama chake mwenyewe :pulpTRAVOLTA:

infact,
katika masuala ya ulinzi na usalama, Tanzania inaaminika zaidi duniani uklinganisha hata na hicho kunachoombwa kuja kufanya uchunguzi ambacho kwakweli si muhimu na hakuna haja wala sababu hata moja ya kuja jumu nchini:pulpTRAVOLTA:
Hujui unachozungumza, hao askari unaozungumzia ndio kama yule shahidi tena koplo mzima kesi ya Mbowe anaulizwa terrorism ni nini anajibu ni masula ya kitalii, hao ndio wachunguze matukio haya?

Tukio la kulipuliwa ubalozi 1998 Dar es salaam na Nairobi, askari wa Tanzania walikamata wanywa gongo na vibaka eti ndio magaidi, FBI wanakuja wanasema waachieni hakuna gaidi hapo hata mmoja, hao ndio wa kuchunguza hio kesi na unawapamba eti kiulinzi tupo mbali?

Punguza uchawa mkuu, jamaa ni weupe.
 
Kichwa cha habari na content mbona tofauti
Unajuwa kusoma na kuelewa kilicho andikwa?

Au ndiyo sababu siku zote wewe huweka alama ya 'like' kwa kila bandiko, ilhali hujui kilicho andikwa humo?

Watu wawili wanaandika juu ya jambo moja wakipingana, wewe unakuja kuweka 'like' kwa kila mmoja wao! Inaingia akilini hiyo?
 
Vipo baadhi ya vifo vilivyowahi kuleta taharuki nchini ikiwemo kifo cha marehemu chacha wangwe aliyepata ajalli eneo la pandambili nje kidogo ya Jiji la Dodoma.
Hakukuwahi kuwa na tume au timu maalumu ya kuchunguza kifo au ajali hii.
Tunapochunguza ya zamani tunaweza kupata mwangaza wa yanayojiri sasa.
Huu ni ushauri huru kwa vyombo na Viongozi wetu katika kupambana na taharuki za kijamii.
 
Inawezekana sana. Na wakati ni maridhawa kabisa.

Viongozi wote wa CHADEMA ni muhimu waelewa jambo moja muhimu sana wanapo tangaza mipango ya utekelezaji wa wa mambo wanayo taka yafanyike. Kwa mfano maandamano.

Ni lazima watambue kwamba hakuna nchi yoyote ambayo wananchi wake wote hujitokeza mbele kuunga mkono harakati za kuleta mabadiliko.
Mageuzi huletwa na juhudi za watu wachache sana walio jitoa mhanga na kupania liwalo na liwe.

Kwa hiyo, kazi kubwa kwa viongozi hawa ni kufanya kazi na wanachama wao kwa karib zaidi, na waTanzania wengine ambao wanachukizwa na vitendo hivi vilivyopo sasa.
Wanachama na wapenzi wa CHADEMA na waTanzania wengine wakiungana pamoja; hakika mabadiliko yatapatikana.

Lakini ni lazima watu hawa wawe tayari kusimama na Chama chao kwa kila hatua na kila aina ya misukosuko itakayo tokea.

Watu milioni mbili/tatu nchi hii hawawezi kukosekana kuleta mageuzi haya..
 
Hujui unachozungumza, hao askari unaozungumzia ndio kama yule shahidi tena koplo mzima kesi ya Mbowe anaulizwa terrorism ni nini anajibu ni masula ya kitalii, hao ndio wachunguze matukio haya?

Tukio la kulipuliwa ubalozi 1998 Dar es salaam na Nairobi, askari wa Tanzania walikamata wanywa gongo na vibaka eti ndio magaidi, FBI wanakuja wanasema waachieni hakuna gaidi hapo hata mmoja, hao ndio wa kuchunguza hio kesi na unawapamba eti kiulinzi tupo mbali?

Punguza uchawa mkuu, jamaa ni weupe.
unaejua punguza makasiriko kidogo basi halafu elezea mambo kwa utaratibu bila mihememko wala hitimisho la ghadhabu kwenye majadiliano muhimu sana kama haya....

kwanza yule muungwana chairman alikua ametumia kinywaji gani kwanza?

chama chake kina sera za mambo ya nje kweli?

ana record za kigaidi na uchochezi,
anapanga kuuhaini kupindua serikali ya kidemokrasia kimabavu,

halafu ati anataka taasisi za nje kuvuja sheria za kimataifa kuja kuingilia uhuru wa mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa hisia na mihemko ya mtu alie tumia kinywaji cha kusisimua akili ?

hakuna kitu kama hicho bana na haiwezekani kutokea hasa kwenye dunia ya leo.

you can't paint Tanzania badly like that in the face of the world unless you have personal issues or mental probablems 🐒
 
"Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?"

"Sasa baada ya mashauriano ya viongozi wa ngazi zote hizi, tumekubaliana, watu pekee ambao tuna imani wanaweza kuja kufanya uchunguzi wa haki katika nchi yetu, iwe lazima ni chombo cha kimataifa cha uchunguzi, na kipekee tumependekeza chombo kinachoitwa Scotland Yard kutoka jeshi la polisi la Uingereza kuja kufanya uchunguzi huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Septemba 11, 2024 Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

PIA SOMA
- News Alert: - Freeman Mbowe: Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho
Hapa kijani na mwenyekiti wao matumbo moto wanajiskia kuhara kila wakati,mfumo umeoza.
 
Wafanye na uchunguzi wa kwa nini yeye ana uenyekiti wa kifalme miaka nenda rudi yeye ni mwenyeki
Nyerer alipo kua mwenyekiti zaidi ya miaka 20 mlifanyia wapi uchunguzi,

Hao kina lipumba wa cuf ama cheyo wa udp mmeshamaliza kuwafanyia uchunguzi?
 
"Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?"

"Sasa baada ya mashauriano ya viongozi wa ngazi zote hizi, tumekubaliana, watu pekee ambao tuna imani wanaweza kuja kufanya uchunguzi wa haki katika nchi yetu, iwe lazima ni chombo cha kimataifa cha uchunguzi, na kipekee tumependekeza chombo kinachoitwa Scotland Yard kutoka jeshi la polisi la Uingereza kuja kufanya uchunguzi huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Septemba 11, 2024 Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

PIA SOMA
- News Alert: - Freeman Mbowe: Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho
 
ali Kiba Mwanafalsafa wakizazi hichi alisema shule ya msingi mtu anakuibia penseli alafu anajifanya kuitafutana wewe
 
Back
Top Bottom