Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe usiwanyime wengine Ubunge kisa wewe hujashinda

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe usiwanyime wengine Ubunge kisa wewe hujashinda

Kuna taarifa zinasambaa kuwa CHADEMA hakitachagua wabunge wa viti maalumu kwenye uchaguzi huu huku wakijua kabisa kuwa ipo kisheria.

Kutochaguliwa wabunge waliokuwa wabunge miaka 10 kutoka CHADEMA katika uchaguzi huu akiwepo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe isiwe ndio kigezo cha kuwaminya wengine wasiingie Bungeni.

Mbona mlipochaguliwa hakuna aliyelalamika kuwa Lowassa ameibiwa hivyo mkasusa kwenda Bungeni mwaka 2015.

Waachieni na wengine wakafanye kazi za ubunge pia mbona Trump kafungasha mizigo huko White House wewe Mbowe ni Nani???

 
Yote heri tu ila wawe wamedhamiria kweli na si mihemko ya muda tu.

Kama wanasusia basi hata hiyo 2025 wajue hawatashiriki uchaguzi kwa maana nina uhakika mazingira yatakuwa ni hayahaya tu.

Kwa lugha nyepesi ni heri wakaachana tu na siasa kwa kumwandikia Msajili akawafutia registration.
 
Watu wengine sijui mna akilini gani! Chama chao wamejiwekea utaratibu wao sasa kama wanadhani hakuna haja ya hao wa viti maalum huruma ipi mnaiona nyie? Au mnataka wakawe rubber stamp tu bungeni! Poor mind!
 
Mkuu kuna kitu hujakielewa, kila chama kina sheria zake. Suala la maamuzi ya chadema ni kwa manufaa ya chama na wanachama wake. hivyo basi kwanini ccm alikuwa na mgombea mmoja wa uraisi wakati kuna wengine pia wenye huo uwezo wakuongoza?
 
Nakumbuka Sana uchaguzi wa marudio wa madiwani pale uwanja wa Soweto lilipolipuka bomu na kuuwa watu kadhaa na hata yale maandamano kule Arusha pia watu walikufa na wao wakina Mbowe na Lema walikwenda kula kiapo Cha ubunge Dodoma Sasa kwanini wanataka Kenani asiende Dodoma kuapa Bungeni, wamuache dada wa watu naye akafanye kazi aliyo tumwa na wananchi wake
Nadhani Wana kiubinafsi kutaka kunyanyasa wanawake tu Hawa, pia awamu hii wanawake wa CDM wamejitoa kwa chama na hawajasaliti wananchi ka wanaume, na hata CDM ilipokosa wagombea wanaume kwa uoga wanawake waligombea kwa kujitoa bila kujali siasa za awamu hii za mkono Dola sasa kuzuia viti maalumu inaonyesha ni chama kisichojali wanawake.
 
Nadhani Wana kiubinafsi kutaka kunyanyasa wanawake tu Hawa, pia awamu hii wanawake wa CDM wamejitoa kwa chama na hawajasaliti wananchi ka wanaume, na hata CDM ilipokosa wagombea wanaume kwa uoga wanawake waligombea kwa kujitoa bila kujali siasa za awamu hii za mkono Dola sasa kuzuia viti maalumu inaonyesha ni chama kisichojali wanawake
Wangekuwa wananyanyasa wanawake wanaweza kuteua wanawake zaidi ya 68 kugombea nafasi za uongozi ?
 
Wapinzani wanachelewesha maendeleo. Hatuwataki bungeni asije hata mmoja!
 
Hii issue iko so complicated

ACT mfano wana viti vya zanzibar wameamua kukataaaa

CHADEMA wana viti bara lakini kumbukeni wanahitaji kuweka msimamo wa pamoja

Iwapo italazimika kabisa kukubali ushauri wa kuteuwa wabunge basi wapeleke list ya wabunge wakomavu na walioonyesha msimamo usioyumba ikiwemo kugombea majimboni

Ndani ya muda mfupi ujao serikali ya magufuli inaenda kuukutana na hali ngumu sana kisiasa na kidiplomasia

Sababu ya pili ni wananwake ambao wameonyesha msimao usioyumba kwenye mapambano ...pamoja na maumivu yote best of the best waende

cc Tundu Lissu
freeman mbowe
halima mdeee
John Mnyika
 
Mbowe nimtu mwelewa sana,atafanyia kazi huu ushauri adhimu kabisa kwa maslai mapana ya watanzania hasa kwa ustawi wa demokrasia yetu kama taifa.
 
Una dalili zote za kutumwa kuja ku convince watu sasa wasipo peleka wabunge wewe inakuhusu nini unawashwa na nn au ndio ile propaganda ile tril ngapi sijui ije, makosa mliyafanya bila mahesabu sahihi endeleeni na maisha.
 
CHADEMA waache ubinafsi na ubaguzi kwa wanawake walioshinda viti maalumu, mbona wao walishinda dhidi ya tume hii hii na wakaenda bungeni?
Wangekuwa na ubinafsi Wangepewa majimbo 68 yakugombea ubunge? Seriously Uporwe ubunge kwa mtutu wa Bunduki ulioshinda kihalali, uje kupewa viti Maalumu kihuni. Uwe unajaribu kufikiria kabla ya ku comment.
 
Kuna kifuta machozi cha bil 30 na zaidi mkulu anajaribu kukifikisha kwa chadema ili waachane na yaliyotokea aliyepwa afikishe ujumbe naona imekuwa ngumu kukutana nao.
 
CHADEMA waache ubinafsi na ubaguzi kwa wanawake walioshinda viti maalumu, mbona wao walishinda dhidi ya tume hii hii na wakaenda bungeni?
Ya chadema hayakuhsu ukiwa unapinga mabaya ungeeanza na aliyesema ukichagua upinzani haleti maendeleo ningekuona wa maana na sio hivi mataga
 
Wa Nkasi amesema atakwenda Bungeni kuapishwa ili awatumikie wananchi waliomchagua Sasa hapo Mbowe hataki ....dada nenda Bungeni kawawakilishe waliokuchagua
Kashasema akichanganyiwa hapeleki maendeleo sasa huyu anaenda kuyaleta wapi
 
Kwani kipindi kina mnyika wanaenda bungeni watu hawakufa mfano Yale maandamano ya Arusha. Kwangu mimi acheni ubinafsi, hafu Mimi siko chama chochote ni raia wa kawaida nisiye na mihemkoa
Onesha uraia wako wa kawaida wakati kuna malalamiko ya uchaguzi
 
Nakumbuka Sana uchaguzi wa marudio wa madiwani pale uwanja wa Soweto lilipolipuka bomu na kuuwa watu kadhaa na hata yale maandamano kule Arusha pia watu walikufa na wao wakina Mbowe na Lema walikwenda kula kiapo Cha ubunge Dodoma Sasa kwanini wanataka Kenani asiende Dodoma kuapa Bungeni, wamuache dada wa watu naye akafanye kazi aliyo tumwa na wananchi wake
Raisi alisema hapeleki maendeleo kwa watakao chagua wapinzani vipi huyu atapelekewa.
 
Back
Top Bottom