KUna mason wa Tanzania wakiongozwa na Sir Andy Chande na mmojawapio wa memba maarufu ni.. u guessed it Benjamin William Mkapa.
Kuhusu alama ya vidole. Naona watu mnachanganya alama mbili zisizohusiana ingawa zinaoneshwa vile vile.
Kwa wanamuziki wa Rock na macelebrity mara nyingi alama hiyo inawakilisha mambo yale ya kishetani kutokana na miziki ya bendi za rock ambazo zilikuwa zinadaiwa zina maneno ya kishetani, na hivyo wale wanamuziki walipoanza kutukuza sifa hiyo ya ushetani wakawa wanatumia alama ya pembe za kishetani.
Kwa wale walioko Texas alama hiyo ya vidole uhusiana na timu ya mpira ya Chuo Kikuu cha Texas ambayo hujulikana kama "Texas Longhorns". Ukienda hata kesho kwenye mechi zao utawasikia wakiimba "Hook em horns" Long horns na wakinyanyua alama za pembe za ng'ombe.
Bush anatoka Texas. Picha ambayo inaonesha hapa ya Bush ni wakati bendi ya Chuo Kikuu cha Texas ilipokuwa ikipita mbele ya Rais Bush baada ya kuapishwa kule Washington DC. Na kwa watu wa Texas where Texas is Bigger than America.. usishangae kuwakuta wakisalimiana kwa alama hiyo ya "hook em horns".. !
Natumaini hii itasaidia angalau kwenye angle hiyo.