Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 10,174
- 89,364
Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminant
Ni mpango wa Shetani kuangamiza sheria ya Mungu tangu mwanzo. Shetani amekuwa akifanya vita dhidi ya amri 10 za Mungu ambazo ndicho kipimo pekee cha utii kwa Mungu. Katika vita hiyo, Shetani amekuwa akitumia mawakala wa aina mbalimbali kiasi cha kufanikiwa kuwadanganya mamilioni ya watu duniani nao wakaiacha sheria ya Mungu na kufuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Shetani ameanzisha kanisa lake na kuweka amri 11 kinyume cha amri 10 za Mungu. Mbeleni tutaona jinsi waumini wa Shetani kwa dini la Freemasons na Illuminati wanavyotumia namba na ishara katika kazi zao duniani kiasi cha kuwapofusha watu huku wakidhani kwamba wanamuabudu Mungu wa mbinguni kumbe wanamuabudu Shetani mwenyewe.
Tunaishi katika nyakati za hatari. Majanga yameenea kila mahali. Machafuko ya kila aina yameenea ulimwenguni kote. Ubakaji, matetemeko ya ardhi, moto usiowezekana kuzimwa, mafuriko wakati wa kiangazi, migomo ya wafanyakazi, maporomoko ya ardhi, kuyumba kwa uchumi, milipuko ya Volkano na mengine mengi yanazidi kutokea kila kukicha, tena katika mataifa makubwa yaliyoendelea na hata kuitwa ‘mataifa ya ulimwengu wa kwanza’.
Kuongezeka kwa machafuko haya ya asili na kisiasa yanawafanya wanadamu wawe na hofu kuhusu maisha yao ya baadae. Inaonekana kana kwamba tupo katika ncha ya mwisho mbele yetu kukiwa na shimo kubwa tayari kuangukia shimoni. Yote haya ni dalili za mwisho wa wakati kwa wale walio na masikio ya kusikia na macho ya kuona, kwamba ulimwengu hautaendelea kwa muda mrefu ukiwa katika hali hii. Mioyo ya watu inajawa na hofu kwa haya yanayotokea (Luka 21:26). Na watu wanajiuliza maswali:
“kwa nini haya yanatokea?” “Je, Shetani ametawala kikamilifu?”
Hapana, Mungu hajawaacha watu wake waaminifu, lakini maswali hayo yote yanaonyesha kwamba kuna kitu nyuma ya matukio haya kuliko wengi wanavyoweza kuelewa. Kuna vita kali inayoendelea kati ya nguvu za nuru na nguvu za giza —-vita kali kati ya Yesu na Shetani— na matokeo yake ndiyo yanayoonekana kwa wanadamu ikiwa ni matukio hayo. Hata hivyo Mungu wa mbinguni amewaambia watu wake kwamba “muda ubakio si mwingi.” Na anaendelea kusema “Tukijua ya kwamba saa ya kuamka katika usingizi imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.” 1 Wakor 7:29; Warumi 13:11-13. aulo anatueleza kwamba “Tuvae silaha za Mungu,” ndipo tutakapoweza kusimamadhidi ya madanganyo ya Mwovu (Waefeso 6:11). Nilipokuwa nasoma unabii wa Danieli, Ezekieli, Ufunuo nk sikujua jinsi unabii huu utakavyotimia na kwamba kumbe kundi linalofanya kazi zake kwa siri kubwa ndilo linalotimiza unabii huu kwa kiasi kikubwa sana. Wengi hawana habari na madanganyo haya ya Shetani na Mungu ametuagiza kwamba tusiwe wajinga kiasi cha kutotambua mbinu za Shetani na hivyo “Shetani akapata kutushinda” 2 Wakorintho 2:11.
Mafanikio makubwa ya Shetani katika udanganyifu yamepatikana kwa njia ya kuwafanya watu wawe wajinga wa mbinu anazotumia katika kazi yake. Wakati tunapokuwa wajinga au kuchanganyikiwa, ndipo Shetani anapotushinda na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashinda wanaume na wanawake wengiulimwenguni. Hivyo hatupaswi kulala usingizi na kushindwa kutambua kile kinachoendelea katika
ulimwengu wa giza. Kwa nini? Kwasababu “Mshitaki wenu, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8; Ufunuo 12:12. Mwovu anajua kwamba muda wake ni mchache na hivyo halali akiwa anafanya kazi ya kuuongoza ulimwengu kuelekea katika uangamivu wa mwisho. Watu wa Mungu karibu watajaribiwa. Wale wasioshinda kwa damu ya mwana kondoo watapata hofu ya majaribu na hivyo kushindwa.
ITAENDELEA