Freemasons na illuminant

Freemasons na illuminant

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminant

Ni mpango wa Shetani kuangamiza sheria ya Mungu tangu mwanzo. Shetani amekuwa akifanya vita dhidi ya amri 10 za Mungu ambazo ndicho kipimo pekee cha utii kwa Mungu. Katika vita hiyo, Shetani amekuwa akitumia mawakala wa aina mbalimbali kiasi cha kufanikiwa kuwadanganya mamilioni ya watu duniani nao wakaiacha sheria ya Mungu na kufuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Shetani ameanzisha kanisa lake na kuweka amri 11 kinyume cha amri 10 za Mungu. Mbeleni tutaona jinsi waumini wa Shetani kwa dini la Freemasons na Illuminati wanavyotumia namba na ishara katika kazi zao duniani kiasi cha kuwapofusha watu huku wakidhani kwamba wanamuabudu Mungu wa mbinguni kumbe wanamuabudu Shetani mwenyewe.

Tunaishi katika nyakati za hatari. Majanga yameenea kila mahali. Machafuko ya kila aina yameenea ulimwenguni kote. Ubakaji, matetemeko ya ardhi, moto usiowezekana kuzimwa, mafuriko wakati wa kiangazi, migomo ya wafanyakazi, maporomoko ya ardhi, kuyumba kwa uchumi, milipuko ya Volkano na mengine mengi yanazidi kutokea kila kukicha, tena katika mataifa makubwa yaliyoendelea na hata kuitwa ‘mataifa ya ulimwengu wa kwanza’.

Kuongezeka kwa machafuko haya ya asili na kisiasa yanawafanya wanadamu wawe na hofu kuhusu maisha yao ya baadae. Inaonekana kana kwamba tupo katika ncha ya mwisho mbele yetu kukiwa na shimo kubwa tayari kuangukia shimoni. Yote haya ni dalili za mwisho wa wakati kwa wale walio na masikio ya kusikia na macho ya kuona, kwamba ulimwengu hautaendelea kwa muda mrefu ukiwa katika hali hii. Mioyo ya watu inajawa na hofu kwa haya yanayotokea (Luka 21:26). Na watu wanajiuliza maswali:

“kwa nini haya yanatokea?” “Je, Shetani ametawala kikamilifu?”

Hapana, Mungu hajawaacha watu wake waaminifu, lakini maswali hayo yote yanaonyesha kwamba kuna kitu nyuma ya matukio haya kuliko wengi wanavyoweza kuelewa. Kuna vita kali inayoendelea kati ya nguvu za nuru na nguvu za giza —-vita kali kati ya Yesu na Shetani— na matokeo yake ndiyo yanayoonekana kwa wanadamu ikiwa ni matukio hayo. Hata hivyo Mungu wa mbinguni amewaambia watu wake kwamba “muda ubakio si mwingi.” Na anaendelea kusema “Tukijua ya kwamba saa ya kuamka katika usingizi imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.” 1 Wakor 7:29; Warumi 13:11-13. aulo anatueleza kwamba “Tuvae silaha za Mungu,” ndipo tutakapoweza kusimamadhidi ya madanganyo ya Mwovu (Waefeso 6:11). Nilipokuwa nasoma unabii wa Danieli, Ezekieli, Ufunuo nk sikujua jinsi unabii huu utakavyotimia na kwamba kumbe kundi linalofanya kazi zake kwa siri kubwa ndilo linalotimiza unabii huu kwa kiasi kikubwa sana. Wengi hawana habari na madanganyo haya ya Shetani na Mungu ametuagiza kwamba tusiwe wajinga kiasi cha kutotambua mbinu za Shetani na hivyo “Shetani akapata kutushinda” 2 Wakorintho 2:11.

Mafanikio makubwa ya Shetani katika udanganyifu yamepatikana kwa njia ya kuwafanya watu wawe wajinga wa mbinu anazotumia katika kazi yake. Wakati tunapokuwa wajinga au kuchanganyikiwa, ndipo Shetani anapotushinda na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashinda wanaume na wanawake wengiulimwenguni. Hivyo hatupaswi kulala usingizi na kushindwa kutambua kile kinachoendelea katika

ulimwengu wa giza. Kwa nini? Kwasababu “Mshitaki wenu, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8; Ufunuo 12:12. Mwovu anajua kwamba muda wake ni mchache na hivyo halali akiwa anafanya kazi ya kuuongoza ulimwengu kuelekea katika uangamivu wa mwisho. Watu wa Mungu karibu watajaribiwa. Wale wasioshinda kwa damu ya mwana kondoo watapata hofu ya majaribu na hivyo kushindwa.

ITAENDELEA
 
Dalili kuu ya kufilisika kiakili,
Ni kuanza kuamini Aya Mambo ya freemason na illuminati.
 
...................... Lakini ni kwa njia gani Shetani anafanya kazi yake? Anafanya kazi kupitia mawakala gani? Jibu linatolewa na Mungu. kwa upendo mwingi Mungu anatufunulia wahusika wakuu katika mchakato huu wa vita ya mwisho kati ya Kristo na Shetani. Wahusika hawa ndio wanaostahili kulaumiwa kutokana na matokeo tunayoyaona katika ulimwengu wote kama yalivyotajwa hapo juu. Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano ambao ni:

1—Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe

2—Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini

3—Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani

4—Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC

5—Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati, freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..

Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti. Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani, (Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4). Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’ kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana vichwa saba inamaanisha vipindi saba vya viongozi saba wa kanisa. Ufunuo 17:8 anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na katika Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu…”. Mafungu yote hayo yanamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna ufufuo. Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika hamtakufa” Mwanzo 3:4. Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.

Je, kuna watu au kitu kinachoitwa Illuminati? Inaweza kuwa katika kizazi chetu hiki? Baadhi wamekuwa wakidhihaki kuhusu swala zima la Illuminati. Hata hivyo katika kitabu hiki unaweza kupata ufahamu wa kina kuhusu Illuminati na Freemason ndani ya jamii tunayoishi. Je, maneno kama Illuminati au Freemason ni mapya kwako? Hilo linawezekana maana maneno hayo hayafahamiki kwa watu wengi, hata kwa wasomi wakubwa wa elimu ya duniani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wahusika wa maneno hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu mamilioni wasielewe kinachoendelea na hivyo maneno hayo kuendelea kuwa siri kubwa.

“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a Conspiracy, p. 195.)

Kazi hizi za Illuminati zimekuwa zikifanyika duniani kote kwa karne nyingi kiasi kwamba watu wengi hawajui hata kuwepo kwa watu kama hao. Njama hizi za siri zinaweza kuwa na msingi wake tangu wakati wa Nimrodi, mtu yule muovu aliyeanza kazi zake za uasi huko Mesopotamia. Wakati kila mwalimu wa dini anajua kuhusu mnara wa Babeli, ni wachache wanaojua kwamba kanuni za mchakato huo wa zamani wa kujenga mnara wa Babeli ndizo zinazofanya kazi hadi leo katika nyanja za Siasa na Dini.
 
Walokole mnazingua,
Afu hiz habari za freemasoni mmezigeuza Mtaji kwenye makanisa yenu uko.

Mmebaki Kila mwenye mafanikio kwenye jamii, mnamkagua vidole kaviwekaje.

Ili mradi TU mumuite freemasoni roho zenu zilidhike.
 
Mkuu unamini juu ya kitabu cha Henoko?

Pia katika kitabu cha Daniel kuna mstari unasema "Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili mia tatu ndipo patakatifu patakapo takaswa" ulielewa nini?

Na je waamini nini juu ya ule ufalme ulioenda katika nchi ya uzuri?
 
Sometimes naona watu wanaamini kwa sababu wanaogopa moto siku ya mwisho!
NB: kuwa na UPENDO tu duniani ni muhimu sana, habari za wanyama n.k hazinishtui
 
Dalili kuu ya kufilisika kiakili,
Ni kuanza kuamini Aya Mambo ya freemason na illuminati.
Binafsi naona tunazinguana tu unajua haya mambo ndo yanawaibua kina Afande Sele huwez kusema Mungu ana vita na shetani sasa Mungu si muweza wa kila kitu na kama anatutakia mema inakuwaje anaagizaje Jitu kama shetani lije kupambana na sisi huku duniani?nmejitahidi kusoma kiukwl sielewi kabisa
 
...................... Lakini ni kwa njia gani Shetani anafanya kazi yake? Anafanya kazi kupitia mawakala gani? Jibu linatolewa na Mungu. kwa upendo mwingi Mungu anatufunulia wahusika wakuu katika mchakato huu wa vita ya mwisho kati ya Kristo na Shetani. Wahusika hawa ndio wanaostahili kulaumiwa kutokana na matokeo tunayoyaona katika ulimwengu wote kama yalivyotajwa hapo juu. Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano ambao ni:

1—Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe

2—Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini

3—Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani

4—Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC

5—Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati, freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..

Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti. Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani, (Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4). Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’ kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana vichwa saba inamaanisha vipindi saba vya viongozi saba wa kanisa. Ufunuo 17:8 anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na katika Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu…”. Mafungu yote hayo yanamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna ufufuo. Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika hamtakufa” Mwanzo 3:4. Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.

Je, kuna watu au kitu kinachoitwa Illuminati? Inaweza kuwa katika kizazi chetu hiki? Baadhi wamekuwa wakidhihaki kuhusu swala zima la Illuminati. Hata hivyo katika kitabu hiki unaweza kupata ufahamu wa kina kuhusu Illuminati na Freemason ndani ya jamii tunayoishi. Je, maneno kama Illuminati au Freemason ni mapya kwako? Hilo linawezekana maana maneno hayo hayafahamiki kwa watu wengi, hata kwa wasomi wakubwa wa elimu ya duniani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wahusika wa maneno hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu mamilioni wasielewe kinachoendelea na hivyo maneno hayo kuendelea kuwa siri kubwa.

“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a Conspiracy, p. 195.)

Kazi hizi za Illuminati zimekuwa zikifanyika duniani kote kwa karne nyingi kiasi kwamba watu wengi hawajui hata kuwepo kwa watu kama hao. Njama hizi za siri zinaweza kuwa na msingi wake tangu wakati wa Nimrodi, mtu yule muovu aliyeanza kazi zake za uasi huko Mesopotamia. Wakati kila mwalimu wa dini anajua kuhusu mnara wa Babeli, ni wachache wanaojua kwamba kanuni za mchakato huo wa zamani wa kujenga mnara wa Babeli ndizo zinazofanya kazi hadi leo katika nyanja za Siasa na Dini.
Unapoteza muda wako kwa kufanya copy and paste kutoka vyanzo ulivyoamua kuviamini.
 
Binafsi naona tunazinguana tu unajua haya mambo ndo yanawaibua kina Afande Sele huwez kusema Mungu ana vita na shetani sasa Mungu si muweza wa kila kitu na kama anatutakia mema inakuwaje anaagizaje Jitu kama shetani lije kupambana na sisi huku duniani?nmejitahidi kusoma kiukwl sielewi kabisa
Yaani mungu uyu uyu alieumba Kila kitu akiwemo uyo shetani.

Eti leo, anavita na shetani.
Utakua uchizi huu.

Kwaiyo mungu kashindwa kuangamiza kiumbe alichokiumba mwnyw
 
Dalili kuu ya kufilisika kiakili,
Ni kuanza kuamini Aya Mambo ya freemason na illuminati.
Upo Dunia gani watu wanajiunga Freemason wengine wanafanikiwa kutoka wengine wanakufa
 
Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminant

Ni mpango wa Shetani kuangamiza sheria ya Mungu tangu mwanzo. Shetani amekuwa akifanya vita dhidi ya amri 10 za Mungu ambazo ndicho kipimo pekee cha utii kwa Mungu. Katika vita hiyo, Shetani amekuwa akitumia mawakala wa aina mbalimbali kiasi cha kufanikiwa kuwadanganya mamilioni ya watu duniani nao wakaiacha sheria ya Mungu na kufuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Shetani ameanzisha kanisa lake na kuweka amri 11 kinyume cha amri 10 za Mungu. Mbeleni tutaona jinsi waumini wa Shetani kwa dini la Freemasons na Illuminati wanavyotumia namba na ishara katika kazi zao duniani kiasi cha kuwapofusha watu huku wakidhani kwamba wanamuabudu Mungu wa mbinguni kumbe wanamuabudu Shetani mwenyewe.

Tunaishi katika nyakati za hatari. Majanga yameenea kila mahali. Machafuko ya kila aina yameenea ulimwenguni kote. Ubakaji, matetemeko ya ardhi, moto usiowezekana kuzimwa, mafuriko wakati wa kiangazi, migomo ya wafanyakazi, maporomoko ya ardhi, kuyumba kwa uchumi, milipuko ya Volkano na mengine mengi yanazidi kutokea kila kukicha, tena katika mataifa makubwa yaliyoendelea na hata kuitwa ‘mataifa ya ulimwengu wa kwanza’.

Kuongezeka kwa machafuko haya ya asili na kisiasa yanawafanya wanadamu wawe na hofu kuhusu maisha yao ya baadae. Inaonekana kana kwamba tupo katika ncha ya mwisho mbele yetu kukiwa na shimo kubwa tayari kuangukia shimoni. Yote haya ni dalili za mwisho wa wakati kwa wale walio na masikio ya kusikia na macho ya kuona, kwamba ulimwengu hautaendelea kwa muda mrefu ukiwa katika hali hii. Mioyo ya watu inajawa na hofu kwa haya yanayotokea (Luka 21:26). Na watu wanajiuliza maswali:

“kwa nini haya yanatokea?” “Je, Shetani ametawala kikamilifu?”

Hapana, Mungu hajawaacha watu wake waaminifu, lakini maswali hayo yote yanaonyesha kwamba kuna kitu nyuma ya matukio haya kuliko wengi wanavyoweza kuelewa. Kuna vita kali inayoendelea kati ya nguvu za nuru na nguvu za giza —-vita kali kati ya Yesu na Shetani— na matokeo yake ndiyo yanayoonekana kwa wanadamu ikiwa ni matukio hayo. Hata hivyo Mungu wa mbinguni amewaambia watu wake kwamba “muda ubakio si mwingi.” Na anaendelea kusema “Tukijua ya kwamba saa ya kuamka katika usingizi imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.” 1 Wakor 7:29; Warumi 13:11-13. aulo anatueleza kwamba “Tuvae silaha za Mungu,” ndipo tutakapoweza kusimamadhidi ya madanganyo ya Mwovu (Waefeso 6:11). Nilipokuwa nasoma unabii wa Danieli, Ezekieli, Ufunuo nk sikujua jinsi unabii huu utakavyotimia na kwamba kumbe kundi linalofanya kazi zake kwa siri kubwa ndilo linalotimiza unabii huu kwa kiasi kikubwa sana. Wengi hawana habari na madanganyo haya ya Shetani na Mungu ametuagiza kwamba tusiwe wajinga kiasi cha kutotambua mbinu za Shetani na hivyo “Shetani akapata kutushinda” 2 Wakorintho 2:11.

Mafanikio makubwa ya Shetani katika udanganyifu yamepatikana kwa njia ya kuwafanya watu wawe wajinga wa mbinu anazotumia katika kazi yake. Wakati tunapokuwa wajinga au kuchanganyikiwa, ndipo Shetani anapotushinda na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashinda wanaume na wanawake wengiulimwenguni. Hivyo hatupaswi kulala usingizi na kushindwa kutambua kile kinachoendelea katika

ulimwengu wa giza. Kwa nini? Kwasababu “Mshitaki wenu, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8; Ufunuo 12:12. Mwovu anajua kwamba muda wake ni mchache na hivyo halali akiwa anafanya kazi ya kuuongoza ulimwengu kuelekea katika uangamivu wa mwisho. Watu wa Mungu karibu watajaribiwa. Wale wasioshinda kwa damu ya mwana kondoo watapata hofu ya majaribu na hivyo kushindwa.

ITAENDELEA
Wanga huu
 
Back
Top Bottom