Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru”

Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru”

View attachment 2774302
HISTORIA YA FREEMASONS

Kwa kuanzia tujifunze kidogo historia ya kikundi hicho: Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru” ingawa hawatambuliki kwa jina hilo, lakini kwa asili ni kikundi cha wajenzi. Kikundi hichi kilianzishwa miaka mingi kinadai tangu wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani, japo umaarufu wake umekuja kuwa mwingi katika karne za hivi karibuni

NANI MWANZILISHI WA FREEMASONS

Kikundi hichi kinaamini “kulikuwa kuna siri zimefichika ambazo ndizo zilitumika katika ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani”…Na kama vile wakristo wanavyoamini kuwa Yesu Kristo ndiye Masihi na kiini cha siri zote za Mungu. Vivyo hivyo Na Freemasons wenyewe wanamwamini mtu mmoja anayeitwa HURAMU, Kama Masihi wao, huyu anapatikana katika kitabu cha 1Wafalme 7, ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa mji wa Tiro ambao kwa sasa ni maeneo ya nchi ya Lebanoni. Huyu ndio kama Masihi wao, Na Mwanzilishi wa freemasons kulingana na wao.

MASHARTI YA FREEMASON

Mshirika kabla ya kujiunga ni lazima awe ana imani ya kuwa kuna “nguvu ya Kiungu”….Hiyo ikifunua kwamba tayari hicho ni “kikundi cha rohoni” kama huamini huwezi kuwa mshirika …Wanaojiunga huko ni watu kutoka dini zote duniani, waislamu, wahindu, wakristo-jina, wabudha n.k..Baada ya mshirika mpya kujiunga anatakiwa kukusanyika na wenzake mara kwa mara katika majengo yao maalumu ya ibada yanayoitwa “Grand Lodges”. kujiunga katika kikundi hicho.

NGAZI ZA FREEMASONRY

Sasa vyeo hivyo vimegawanyika katika ngazi kuu 33 wanazoziita “shahada” au “degrees”

Mshirika mpya anayejiunga, kuna viapo anaambiwa aape, moja ya viapo hivyo ni kukiri kuwa mwaminifu, na kutokufichua siri yoyote ya chama hicho, na pia ataambiwa akiri kwamba endapo atafichua basi atakufa, na pia anaambiwa aape kwamba atakuwa mwaminifu, na pia atakuwa tayari kushirikiana na wenzake, na kusaidiana na wenzake kwa hali na mali…
Bado sina uhakika kama kweli unawajua Freemasons, hasa pale ukitumia tafsiri sisi eti maana ya Freemasons ni "Wajenzi huru". Kwenye Kiswahili Wajenzi huru Ina maana gani?
 
Ukitaka kuachana na habari za mtaani na kuijua freemasons nje ndani inabidi uanze mbali sana usome haswa vitabu kama the secret teachings of all ages ,usome kuhusu ancient religions kama zile za Egypt,babylon,usome kuhusiu machimbuko ya philosophy kwa kweli uingie deep sana kuliko kutegemea wikipedia
 
Ukitaka kuachana na habari za mtaani na kuijua freemasons nje ndani inabidi uanze mbali sana usome haswa vitabu kama the secret teachings of all ages ,usome kuhusu ancient religions kama zile za Egypt,babylon,usome kuhusiu machimbuko ya philosophy kwa kweli uingie deep sana kuliko kutegemea wikipedia
Hivyo vitabu tunavipata wapi? Au niende kwenye lodge zao?
 
Niko pale naongea na mlinzi, lakini watu macho kodogo utasema naoga nje vile
Kwa uelewa wangu wao ndo wanakualika wewe ujiunge sio wewe ujipeleke, ukiwa na rafiki ambaye yupo tayar Freemason yeye ndiye atakuharika baada ya hapo watakufanyia mahojiano, hawa watu wapo selective wanachagua watu ambao wanajiweza kiuchumi, na wapo smart kichwan
 
Back
Top Bottom