Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Ufaransa hii iliyopigwa ndani ya wiki 6 na Hitler na wanajeshi wao wakavalishwa nguo za kike na kupangwa mstari wakati Hitler anaingia ufaransa huku wakimshangilia kama wao cheerleaders?Hicho kibao kimoja ameshindwaje kumpiga Ukraine..? Tupe ushahidi kwamba majeshi ya Ufaransa tayari yalikuwa yameshaingia Ukraine vinginevyo ni porojo zilezile za masjid ubwabwa za jua kuzama kwenye tope.
-----------------------------
Ikiwa kama itazuka vita ya nuclear baina ya hayo mataifa mataifa ya Nato yatapata hasara zaidi kuliko Russia.
Mosi, Russia ina vichwa vya kubebea mabomu ya nuclear ambayo yanafika kwa haraka zaidi kwa nchi za wenzake kuliko wenzake. Mfano; Sarmat. Kutoka Russia mpaka UK ni dakika 2.
Pili, Eneo kubwa la kijiografia kinchi linampa Russia faida. Nchi za Nato ni ndogo na kwa msingi huo raia wake wamejirundika rundika kwenye miji. Hivyo likipigwa bomu la nuclear maafa ni makubwa zaidi ukilinganisha na Russia. Russia ana eneo kubwa la nchi na raia wake hawajarundikana kama nchi za Nato. Raia wake wametawanyika maeneo tofauti tofauti ya nchi. Hivyo kiathari ataathirika lakini si kama nchi za Nato hususani ulaya ya magharibi.
Tatu, Russia ana silaha nyingi za nuclear kuliko wao. Hii ni hatari nyengine. Na kubwa zaidi Russia wana mfumo unaoitwa dead hand. Ni automatic nuclear weapons-control system ambao hata kama mkilipua kwa kumshutukiza na kuimaliza Russia, huo mfumo automatically utashambulia nchi hasimu za Russia utaji command wenyewe kwa mabomu ya nuclear. Hii siri ilitolewa na makachero wa Russia waliyokimbilia nchi za Nato.
Mambo bado no magumu kwa Nato kujitoa kafara ya namna hiyo!