From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Kipimo cha kiongozi kukubalika ni uchaguzi halali, sio hizo porojo zako za huko mtaani. Ukiona kiongozi haheshimu uchaguzi ujue hakubaliki, ama kiwango chake cha kukubalika ni kidogo.
Usilazimishe kuhusisha kukubalika kwa mtu na masuala ya uchaguzi, suala la Magufuli kukubalika hata sio la kuleta ubishani hapa.
 
Wanahistoria kabla ya kusoma Historia yoyote huwa wanamsoma mwandishi wa Historia hiyo kwanza.. Alikuwa na Mrengo gani, Elimu yake, Mtazamo wake katika masuala ya maendeleo ya jamii, nk.. Hii inasaidia wanahistoria kuweza kujua kama Historia hiyo imeeleza ukweli, imependelea, au imekandamiza upande fulani kwa sababu ya maslahi binafsi..

Ukiwatazama waandishi wa kitabu hiki wanajulikana wote mrengo wao.. Kwa maana hiyo basi kitabu hiki kitakuwa kimejaa Biasness ya kiwango cha kutisha ili tu kuwaridhisha waliofadhili uandishi wakitabu hiki..

Niseme tu kuwa kitabu hiki kitawafurahisha wachache kwa muda mfupi lakini hakitadumu katika Historia.
 

Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg


Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Miladi chato ivi awa wanakili kweli aya na twiga kupandishwa ndege awakuona awakutunga kitabu
 
Samia huyo hapo fedha za nchi zote anapeleka zanzibar, na hamuongei kwasababu now mashirika yenu ya mashoga now yanawaingizia fedha, Magu alipiga pini lazima mlalame.

Kikwete huyo hapo kapendelea kwao mpaka basi, na waswahili kibao wasio na sifa kawapa vitengo, hamuwezi kuongea kwakuwa mnapata bahasha.

Riporti ya CAG madudu kila kona na hiv mwanamke ndo wanamdharau mpaka basi, Makamba, Nape, Mwigulu wanuka rushwa wamefanya hizo wizara kama za urithi wa ukoo...

Hutomuona Zitto uchambuzi akimgusa kipara kwenye Vyura wala Nishati. Au Nape zaid ya kuandaa ftari TTCL na kuchukua 10% toka makampuni ya simu hakuna anachofanya zaidi ya kuzungusha mtumbo wake mkubwa hapo wizarani.

Mungu anasikia kilio cha watanzania na hajawahi kushindwa, atajibu katika hili... hii sio nchi ya familia, Stupid kabisa in bibi tozo voice.

Anserbt, Meena, E.Kamwaga, Khalifa Said... now watakuja na majarida mengi tu bz now wanakula keki ya taifa wanavyotaka kwa kuwa vibaraka na walamba matako wa system na mabeberu kupitia NGOs uchwara.
Umesema kuajiri maswaiba nikakumbuka mnyikuru wa mkwere
 
Yaan watu wazima Tena wazee na akili zao wanapoteza muda mwingi kwa kufanya vitu vya kijijnga na kipumbavu.Ngurumo kwa umri ni Mzee ,lakin anafanya ujinga mwingi.Sijui maisha yake atayatengeneza lini.
Kweli kuwa mtu mzima hai guarantee kuwa na akili... nimejifunza kutoka kwenye huu uzinduzi wa kitabu!
 
Wapuuzi hao achana nao. Wanajitoa akili wakati ukweli wanaujua. Kwani mtu kujenga anapotokea kavunja katiba au sheria gani?

Kwamba angestaafu urais nae angeanza kumuimba rais aliyepo apeleke barabara, hospital, maji, umeme huko Chato.

Mi sina kupuuza. Maana ulikuwa rais hukufanya kwenu. Huo sio uzalendo ni uhanithi.

Juzi tu hapa tulikuwa tunalalamika mkopo tunagawanaje sawa na visiwani wenye watu laki 5!!!

Kubali majina yote ila sio mtu akuite chawa,ujue amegundua una ucenge mwingi sana.

Hayo mazee ni machawa tu.
 
Kwenye logic hili kosa linaitwa "logical non sequitur".

Yani unaunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano.

Ikiwa utawala wa sasa unaharibu, hilo halina maana Magufuli hakuharibu.

Tena, inawezekana utawala wa sasa unaharibu kwa sababu umejifunza kuharibu kwenye utawala wa Magufuli.

You are creating a false dichotomy, a fake mutual exclusivity.

Nimeona watu wengi wakiwa na huu ujinga kwamba ukimsema Magufuli basi lazima unamtetea Samia, wakati wote wanaweza kuwa walewale tu!

Huwezi muweka magufuli na samia eneo moja.

Hiyo ni dalili kwamba una ajenda chafu.
Kwa maelezo yenu magufuli alikandamiza demokrasia,samia anakandamiza demokrasia???
Magufuli alinunua ndege bila kuitisha vikao,samia amenunua hata kijiko billa kuwataarifu???
Sabaya,makonda na musiba walikuwa ni chawa wa magufuli vipi mama amewatumia???

Ukimsema magufuli wewe ni mnufaika wa utawala wa saaa period.leo kuna mambo kibao ya kipuuzi yanaendelea na yanazidi kuwa hovyo,hatuwezi kubali kupotezwa maboya na historia za mtu aliyekufa tayari.
 
Usilazimishe kuhusisha kukubalika kwa mtu na masuala ya uchaguzi, suala la Magufuli kukubalika hata sio la kuleta ubishani hapa.

Imebidi nicheke sana, awe anakubalika sana huko mtaani, ila ikifika kwenye kipimo halisi cha kukubalika kwake ashindwe kuheshimu zoezi hilo! Hii ni kali ya mwaka.
 
Hao waandishi wanatafuta hela labda na umaarufu. Kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea nakosa lugha nzuri ya kuita kitendo hiko. Labda atokee mtu mwingine wa kuandika kitabu kwa yale mazuri aliyofanya JPM,ni fursa pia. Maiti asipoweza kujitetea walio hai wamsemee.

Uwanja uko wazi, andika kitabu cha kumtetea au kumsifia hakuna mwenye tabu na hilo, ila kitabu hiki kimeandika ukweli wa mabaya yake. Ifahamike alipokuwa hai hakuruhusu kusemwa, acha asemwe sasa.
 
Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!

Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.

Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?

Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?

Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?

Mkapa na kusini?

JK?

Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?

Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.

Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
Umegusa kila mahali mkuu.

Ukweli ni kwamba:
1. JPM alikuwa ni bonge la rais lakini
Mwenye mapungufu mengi lakini;
2. JK, SSH, na Mwinyi ni wadhaifu zaidi.
3. Magufuli ukiondoa ubabe uliopitiliza kwa kweli angekuwa bora sana.

Kwasasa tumerudi nyuma sana kushinda zama za JK.
 
Wanahistoria kabla ya kusoma Historia yoyote huwa wanamsoma mwandishi wa Historia hiyo kwanza.. Alikuwa na Mrengo gani, Elimu yake, Mtazamo wake katika masuala ya maendeleo ya jamii, nk.. Hii inasaidia wanahistoria kuweza kujua kama Historia hiyo imeeleza ukweli, imependelea, au imekandamiza upande fulani kwa sababu ya maslahi binafsi..

Ukiwatazama waandishi wa kitabu hiki wanajulikana wote mrengo wao.. Kwa maana hiyo basi kitabu hiki kitakuwa kimejaa Biasness ya kiwango cha kutisha ili tu kuwaridhisha waliofadhili uandishi wakitabu hiki..

Niseme tu kuwa kitabu hiki kitawafurahisha wachache kwa muda mfupi lakini hakitadumu katika Historia.
Dawa ya moto ni moto! Kiandikwe kitabu kuelezea mema ya JPM kwa taifa. I bet kitanunuliwa saaanaa...
 
Kimeandikwa na puppets pungaz hao waliokuwa "wateswi" wa JPM, wale waandishi waliokuwa wakilipwa kuandika mabaya tu ya utawala wake.

Kumbe kweli alikuwa na mabaya, sasa kuna ubaya gani wa mtu kuandika mabaya yake tu? Nyie si mngejotikeza kuandika mazuri yake tu? Au ni hatua gani walichukuliwa waliokuwa wanaandika mazuri yake tu bila kuchanganya na hayo mabaya yake?
 
Dawa ya moto ni moto! Kiandikwe kitabu kuelezea mema ya JPM kwa taifa. I bet kitanunuliwa saaanaa...

Mnangoja nini kuandika hicho kitabu cha mema yake, au nyie sio wabunifu bali ni watu wa kuiga tu baada ya wabunifu kuanzisha jambo?
 
Hao Wanakagera wawili na askofu wao wangeandika tu kitabu cha kujikwamua na umaskini wa mkoa wao kingeuza sana kwa sababu na wilaya zake ziko bottom kwa umaskini
Hicho cha mkoa wa Kagera kaandike ww ili kiuze sana, acha hicho chao kikose wateja.
 
Back
Top Bottom