From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!

Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.

Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?

Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?

Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?

Mkapa na kusini?

JK?

Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?

Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.

Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
Unajua kinachoendelea kwa sasa huko Zanzibar?,je unajua kua ajira kwa sasa serikalini wanzanzibar wanachukua 1/3 ya ajira zote za Tanzania bara?,punguza ujuaji wewe
 
Hichi kitabu kimeandika nini cha maana kusaidia taifa kuliko hizi fedha zinazoibiwa na mafisadi sasahivi kwani chato sio Tanzania?
 
Ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga!! Kama alipewa sumu na wewe uliyempa sumu utakufa kwa sumu!!

Kitabu kimeandikwa na wapinzani sijaona Cha achabu hapo!

Hata kama angekuwa mwizi mwenye kupendelea kwao alikumbuka pia na kwengine.SGR ,Ndege, Mwalimu nyerere hydrolylic power ,Lami zilitandikwa kila Kona ya Nchi, hospitali zilijengwa kila Kona ya Nchi NK ,nK,nK.

Kwani chato siyo Tanzania au? Acheni upumbavu wa kiwango Cha upumbavu!!

Lakini pia afadhali mwizi mmoja kuliko Nchi inavyoliwa kama mchwa kila Kona ya Nchi kwa sasa.soma ripoti ya CAG ndiyo utaona sasa Nchi inavyoliwa kama mchwa! Maofisini hamna madili ya Kazi tena.

Na kwani kitabubkizindukiwe na askofu Bagonza ambaye tunajua alikuwa mpinzani wake.Ndiyo maana Mtu mmoja kasema bukoba ni maskini japo ni wasomi kwa sababu ya ujuaji na usomi wa kijinga.kitabu hicho kikae kanisani kwake wakasome na masisters zake.

Serikali ikipige marufuku likitabu hilo
Unachekesha!
Eti serikali ipige marufuku.
Wewe ndo ujipige ban usikisoma. Watu twakusaka hicho
 
Alishambuliwa na kutekwa, kuteswa na kuwagiwa tindikali mnamo Machi 2013 kipindi ambacho JPM hakuwa na mamlaka ya kushughulika naye lakini hausemi vibaya utawala uliopo ambao una kivuli cha kiongozi mstaafu aliyetawala Tanzania kati ya 2005-2015. Huyu mwenye miwani kwa maneno yake alitamka kwamba anamwogopa sana kanali Abdulahaman Kinana kwa sababu zake binafsi anazozijua. Hata afanyaje hawezi kujitokeza hadharani kumkosoa kwa vyovyote vile.
Sawa alimwagiwa tindikali, lkn yy mwenyewe hajataka kuyaeleza wewe unataka kumpangia cha kuandika.
Kwake mabaya aloona yafaa zaidi kutueleza sie ni Magufuli. Sasa na wewe andaa kitabu cha mabaya ya JK na mazuri ya Ngosha utapata tu wasomaji
 
Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Pdf yake
 
Tayari kitabu kiko sokoni kama vipi na nyie mifugo ya Magufuli andikeni kitabu cha kumpamba, simple!!!
Mimi nawaona watu wa Aina yetu hamna Akili Kwa Sababu tunajua Magufuli alijenga vitu karibu kila sehemu Tanzania.
 
Naunga mkono ujio wa kitabu kwa vile huo ni mwanzo wa vitabu vitakavyoandikwa kwa ajili ya kuelimisha Watanzania wajinga wapatao 90% juu ya UHAYAWANI wa Magufuli aliotufanyia.

Nategemea kuona wengine wakiandika vitabu vifuatavyo:

1. Magufuli: Mtawala wa Kiimla aliyetawala bila kufuata Katiba aliyoapa.

2. WASIOJULIKANA & TASK FORCE: Namna Magufuli alivyounda magenge ya haramu kwa ajili ya kuua wapinzani na kupora matajiri

3. Namna ya kuwa Rais wa Maisha: Jinsi Magufuli alivyoiba uchaguzi wa S/Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020
 
Kwa kweli hakuna kitabu Bora kama hicho. Ili kuimarisha uzalendo, nashauri kitabu hicho kitumike kufundishia mashuleni elimu ya historia. Hakika watoto watakua wakielewa mambo mengi kwa kina.

Hongereni watunzi
 
Tupe mtunzi,na vile tunaweza kupata kitabu chenyewe🤔
 
Back
Top Bottom