Frustrations: Walitarajia mpaka muda huu CHADEMA iwe imesambaratika na kushindwa hata kutimiza majukumu yake ndani ya Bunge

Frustrations: Walitarajia mpaka muda huu CHADEMA iwe imesambaratika na kushindwa hata kutimiza majukumu yake ndani ya Bunge

Aisee ukiwaangalia wale vijana unaishia kuwasikitikia wao na walio wanunua. Ni sawa na kuchukua demu anaye mpondea ex wake.
Tena ni mayai viza hayo, lipasue uone linavyonuka. Mfano Lijualikali, huyo anatofauti gani na yai viza?
 
Myopia!
Kwani sasa kuna chadema au kutimiza wajibu tu?subirini tarehe ya mwisho kuvunjwa bunge

Cdm sio wabunge, bali ni sisi wananchi tunaoikubali. Hao wabunge hata waondoke wote kwetu sio tatizo. Angalia Slaa aliondoka mkampa Airtime ili ahamishe mitazamo ya wanacdm, lakini watu wakawa wanamchora tu. Itakuwa hao akina Lijualikali?
 
Tena ungemaliza na neno AIBU KUBWA!
Bila shaka haya ndio yalikuwa matumaini yao kuona CHADEMA mpaka kufikia mwisho wa vikao vya Bunge, chama kiwe kimesambaratika mitaani na Bungeni abaki Mbowe labda pengine na wabunge wasiozidi watano ila hali ni tofauti kabisa.

Hadi kufikia leo,CHADEMA bado iko ngangari na leo wamesoma Bajeti mbadala bila mkwamo hivyo wameshinda mtihani wa kuhujumiwa kwa miaka mitano na sasa Bunge linakwenda kuvunjwa na hata kama wako wataohama, bado hakuna kitachoiyumbisha CHADEMA.

Licha ya hujuma zote,CHADEMA iko kila mahali nchi hii kuanzia ngazi za vitongoji mpaka Taifa na iko imara katika ngazi zote kuanzia chini mpaka juu.

CHADEMA ni kama siti ya daladala,akitoka huyu anaingia mwingine tena kwa kuwahi faster asikose siti.

Poleni sana ila angalieni msife kwa frustrations baada ya kushindwa kutimiza azima yenu.

CHADEMA kwa watanzania ni mpango wa Mungu kama ilivyokuwa Mussa kwa wana wa Isreali.

Miaka mitano wanatwanga maji kwenye kinu na bado hawashituki!!!Sijui kama wako timamu!!

Aibuuu!!!!
 
Kufa kqa chama sio jina.bqashee,kufa kwa chama ni zile shughuli za kila siku za kujitanua
TADEA ipo kimaandishi lak i ni.imekufa tu,na chadema.mmeshafika huko mkipata wabunge hata wawili mkachinje kuku

Acha kupanick mpaka unashindwa kuandika vizuri.
 
Juhudi kubwa zinafanyika ila tunapambana na nguvu kubwa ya kutaka kutuvunja moyo kutoka kwa waoga wa kukosolewa
Hongereni sana Wanachadema halisi. Huu ni muda wa kunirudisha chama kwenye uhalisia wake.
 
Kilichobak mlete wagombea Makini na muungane na act_wazalendo kumkomboa mtanzania hii ni safari ya 2025

2020 naona upepo ni mgumu.
 
Ngoja tusubirie takukuru nao labda wataweza maana wengine wameshindwa
 
Chama kimebaki na watu wasio nunulika makapi yote yamechujwa na kurudi ccm

Mbowe kapewa 5billion asigombee uwenyekiti kachomoa, Mnyika, Mde, Bulaya, Matiko Milion 500 na uwaziri wamechomoa wakina Sugu, Lema mil 300 na ubunge wakachomoa.

Watu watakao baki chadema ndio wazalendo na wanatakiwa kupewa nchi

Chadema inaenda kuwa imara zaidi ya 2015 kwenda nyuma ambapo ilikuwa na watu watiifu na wafia chama na ambao wapo tayari kwa lolote..
Bora nibakie na dhiki zangu nikiwa na cdm.
 
Nyalandu nadhani ndiye mwenye uchungu na demokrasia ya kweli maana yeye aliamua kujiuzuru ubunge wa ccm ili kulinda anacho kiamini.

Aliwachia ubunge baada ya wana ccm kumuandama kisa alienda Nairobi kumjulia hali baada ya kupigwa risasi na wasiyo julikana.
Uchaguzi huu tuweke Chadema Halisi sio hawa fake kina nyalandu
 
Back
Top Bottom