FT: AFL: Mamelodi Sundowns 1 Vs 0 Al Ahly | Stadium: Loftus Versfeld | 29.10.2023

FT: AFL: Mamelodi Sundowns 1 Vs 0 Al Ahly | Stadium: Loftus Versfeld | 29.10.2023

Masandawana aka bafana style wameupigwa mwingi hakika tumeona mechi ya kusisimua .
Hata hivyo bado kuna udhaifu umefanyika wa refa pale mendieta wa mamelodi aliposukumwa Kwenye eneo la penalti , var ikaandika checking for foul lakini refa akapeta , hawa waarabu wabebwa sana .
Kulikuwa na mawasiliano pale na waliokuwa wanacheck ni watu waliopo kwenye chumba cha V.A.R
 
Mechi ya kwanza ya nusu fainali inayowakutanisha wapinzani wawili Al Ahly na Mamelody.

Kwenye h2h takwimu zinambeba Mamelody

Mechi 5 za mwisho walizokutana, Al Ahly hajapata ushindi wowote zaidi ya kuambulia sare.

Mamelody kashinda mechi 3 huku mechi 2 zikiisha kwa sare

Leo tutaenda kuona kama Al Ahly ataendeleza uteja kwa kukubali kipigo au atafuta uteja kwa kumpiga Mamelody.

Mechi ni saa 10:00 jioni
Huyu kocha mjanja alipowapiga bao waarabu akawaachia wacheze mpira ila marufuku kusogea kwake.
Ahly ni wazuri sana ila game yao pale nyumbani Mokwane anaimaliza mapema sana kwa kuwa level ya beki zake ni nzuri sana na wana viungo wenye kasi.
Dieng na Percy ndiyo game changer na wakibanwa hao timu inapotea mazima.
Nawapa Mamelod 55% kusonga mbele.
 
Al ahly wakifikaga Kwao huwa wanabadilika kabsa na Sioni tena nafasi ya Mamelod kusonga Mbele
Si tungeona dhidi ya Simba wakibadilika? Kuna hatari ya kufungwa kule kule kwao kwasababu Al Ahly wakiwa wanashanbulia ni rahisi sana kuwafunga kwa counter attacks, leo walipaki bus muda mwingi sana. Tunaenda kushuhudia mechi iliyochangamka Misri.
 
Al ahly hawez kufungwa kwao wala kutoa Draw Lazima atashinda Tu, nina wasiwas hii Game itaamuliwa kwa Penati na Al ahly kuingia Fainali,.... Screenshot hii Comment.
 
Al ahly hawez kufungwa kwao wala kutoa Draw Lazima atashinda Tu, nina wasiwas hii Game itaamuliwa kwa Penati na Al ahly kuingia Fainali,.... Screenshot hii Comment.
Sababu ya kutofungwa wala kutoa sare ipi? Kuna sababu ya kiufundi umeona au ni utabiri wako?
 
Hawa Mamelod wameshindwa kutumia nafasi vizuri na home ground ilitakiwa wapate goli zidi ya mmoja wajue kabisa shughuli ya Egypt haitakuwa rahisi
Kwani ndiyo wanaanza kwendako safari hii?
 
Back
Top Bottom