Acha tutoke maana haitakuwa sawa na ambaye hakuingia kabisa.
Tutatoka tukiwa tumeionesha dunia mpira wa Tanzania jinsi tulivyo u-inspire.
Tutatoka tukiwa tume wave flag ya Taifa na kuthibitisha kuwa haikuwa makosa kufanya uzinduzi kwenye ardhi ya Tanzania huku mwakilishi akiwa ni Simba.
Tutatoka tukiwa tumeacha alama ambayo itadumu milele na haijikufutika kuwa Simba ambao kikosi chao hakizidi thamani ya 7 Bilioni kilimpeleka putaputa Al Ahly ambaye mchezaji wake mmoja alisajiliwa kwa 12 Bilion.
Tutatoka tukiwa tumeiachia Dunia maswli mengi kwanini Club namba moja Duniani kwa mataji mengi leo hii ikutane na upinzani mkali hivi tena katika ardhi ya nyumbani?
Baada ya hayo yote ndio itapopatikana sababu ya Tanzania kuwa mwenyeji na mfunguzi wa AFCON.