FT: Al-Hilal 1-0 Yanga (Agg 2-1), Yanga yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika

FT: Al-Hilal 1-0 Yanga (Agg 2-1), Yanga yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika

Mlijipima nao friendly match,unayakumbuka matokeo?
Wao walikuwa full mkoko kama hivi leo na sisi hatukuwa na key players zaidi ya 8, tulimiliki mpira wakapata goal la mpira wa kutenga.

Nakwambia hivi Al Hilal akikutana na Simba Sc mechi za CAFCL anagongwa nje ndani au labda atoe sare kwake huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
76' Yanga wanamtoa Morrison anaingia Makambo
70' Mchezo umesimama kwa muda, mchezaji wa Al Hilal ameumia
60' Fei Toto anapiga shuti linatoka na kuwa kona
53' Yanga wanamiliki mpira muda mwingi
50' Al-Hilal wanafanya shambulizi kali langoni mwa Yanga
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO
45' Mwamuzi anamaliza kipindi cha kwanza
40' Timu zote zimefanya mashambulizi makali kwa kupokezana
37' Mwamnyeto anacheza faulo, inapigwa kuelekea kwa Yanga
36' Yanga wanaendelea kuweka presha langoni mwa wenyeji wao
30' Kasi inaongezeka na Yanga wanaonekana kujiamini
20' Yanga wanafanya shambulizi lakini mpira unatoka nje
15' Kocha wa Al-Hilal, Ibenge anasimama kutoa maelekezo
10' Yanga wanaonesha utulivu na kujipanga
Mohamed Abdelrahman anaipatia Al-Hilal bao la kuongoza
3' GOOOOO!
2' Wenyeji wanafika langoni mwa Yanga
Mchezo unaanza
Timu zinaingia uwanjani

View attachment 2389396
Kikosi cha Yanga dhidi ya Al-Hilal katika mchezo wa marudio.
========

Ni siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki hapa Tanzania na kule Sudan.

Yanga inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya sare ya 1-1 aliyoipata nyumbani pale uwanja wa Mkapa wiki iliyopita.

Je, hii itakuwa mechi ya mwisho kwa Yanga msimu huu kwenye Klabu Bingwa Afrika au anaenda kuvunja rekodi yake kwa kufuzu makundi tangu 1998?

Tutakuwa hapa tukipeana taarifa mubashara. Mechi inaanza saa tatu kamili usiku.
Kwahiyo Yanga wanashindwa funga kabisaaa...!??
 
Yanga wakisawazisha moja kwa moja nawapa asilimia kubwa ya kupita
 
Hawa wanafungika Yanga wenyewe tu watulize makeke
 
Ngoja nijilalie zangu mimi. Nitarudi asubuhi, kuja kuchungulia kama tumeangukia wapi.
Hehehe, lala tu mkuu[emoji23]
Screenshot_20221011-133309.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom