Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Wewe mwenyewe umepuyanga sana.wengi hamuelewi hili. kuanzia saa sita na madakika ambayo huwa tunaiita mchana (which is a general word), ni muda wa adhuhuri. adhuhuri inaisha saa tisa kamili.
kuanzia saa tisa kamili hadi saa kumi na moja, inaitwa alasiri.
kuanzia saa kumi na moja hadi saa moja, inaitwa "jioni", na hiyo inamaanisha hilo ni "jio la usiku".
nendeni mkawafundishe na wenzenu. kwa bahati mbaya hata maprofesa wa kiswahili pale udsm watashindwa hili swali.
Alasiri Ina masaa mawili tu saa 9 na 10 .
Saa 11 hadi saa 1 ni Jioni
Usiku ni saa 2 hadi saa 6
Saa 7 hadi saa 10 ni usiku wa manane.
Saa 11 na 12 ni Alfajiri
Saa1-5 ni asubuhi
Saa 6 ni adhuhuri
Sa 7-8 ni mchana.