TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Sikuona mechi, analysis hii imenipa radha ya mechi. Asante sana.Timu imecheza vizuri na wote wamejituma ila Kibu Denis Prosper naweza kusema kwangu alikuwa man of the match.
KUna muda nilikuwa naona kabisa waarabu wakipagawa pale wanapomiliki mpira halafu pembeni wanamuona Kibu.
Ibrahim Backa kafanya ukatili sana eneo la chini, kazima mashambulizi ambayo yalikuwa na hatari mno.
Huyu kuna press aliifanya kimahesabu it was very quickly maana mpinzani alikuwa anataka kupiga cross kuelekea kwenye box ambapo walikuwa washambuliaji wa Algeria.
Bila Backa kufanya pressing ule mpira pengine tungeongea mengine.
Kakolanya amefanya save nzuri lakini licha ya hiyo save bado alikuwa makini sana kuona mipira na kukaa eneo sahihi kwa ajili ya kuzuia hatari iwapo shuti likipigwa.
Mwisho namsifu kocha, kwanza kwasababu game approach tulifanana mtizamo. Mimi mwenyewe nilitaka tucheze kwa kujilinda na kuanza kukabia chini kwenye eneo letu huku tukiwaacha watawale mpira eneo la juu kuvuka box.
Wakati huo tunakuwa na idadi ndogo ya wachezaji eneo la mbele ambao watakuwa wanaenda kukaba mipira na kujaribu kutengeneza counter attack.
Mwisho tumefuzu na ni kitu cha kujivunia cha muhimu ni kukaza tu na kujitoa.
Hata hizo hatua za mbele uwezekano wa kufanya vizuri pia upo.
Mpira nao ni kama vita sio muda wote unaweza ukaamuliwa kwa ubora wa silaha zako, sometimes morale ina play role yake.
Hivyo hivyo na kwenye mpira, wachezaji wakijitoa kwa asilimia zote basi wanaweza kufanya makubwa kuliko timu yenye wachezaji bora.